Tuesday, August 6, 2013

Juhudi za amani zashika kasi Misri


Wafuasi wa Mohammed Morsi
Maseneta wawili wa Marekani John McCain na Lindsey Graham wamewasili mjiniCairo, wakati jitihada zikishika kasi kuutatua mzozo wa kisiasa nchini Misri uliozuka baada ya kupinduliwa rais aliyechaguliwa kidemokrasia Mohammed Morsi.
Wasiwasi unazidi kutanda baada ya serikali mpya inayoungwa mkono na jeshi kutangaza mpango mpya wa kuyasitisha maandamano, ambako wafuasi wa Morsi wanataka arudishwe madarakani.
Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na wageni mashuhuri wa kiimataifa wanaozuru Misri, wanaotarajia kusaidia kusimamia kupatikana suluhu ya amani katika hali ya suitofahamu iliopo kati ya wafuasi wa rais aliyepinduliwa na serikali inayoungwa mkono na jeshi.
Lakini mpaka sasa hakuna taarifa zaidi zimetolewa kuhusu hatua zilizopigwa.
Kwa wakati mmoja kulikuwa na ripoti kwamba baraza jipya la mawaziri lilikuwa tayari kuwaachia viongozi wa vuguvugu la Muslim Brotherhood kutoka gerezani na kuwapatia nyadhifa za mawaziri iwapo watasitisha maandamano mjini Cairo.
Hata hivyo mshauri wa rais amekana tuhuma hizo na wafuasi wa Morsi wamesisitiza hawatokubali chochote isipokuwa kurudishwa Morsi madarakani.

Kiongozi wa upinzani Burundi arejea nchini


Rwasa alitoroka Burundi baada ya uchaguzi wa mwaka 2010
 akihofia maisha yake
Kiongozi rasmi wa upinzani na zamani akiongoza waasi nchini Burundi Agathon Rwasa ametoka mafichoni baada ya miaka mitatu ya kuwa nje ya nchi.
Alikanusha madai kuwa alikuwa anaishi katika nchi ya kigeni muda huo wote na kusema kuwa atagombea uchaguzi wa mwaka 2015
Maafisa wa serikali walimzuia kuhutubia wafuasi wake wakisema kuwa hana ruhusa kufanya hivyo , na kwa hivyo akahutubia waandishi wa habari nyumbani kwake.
Bwana Rwasa alimaliza uasi wake mwaka 2009 lakini akatoweka kabla ya uchaguzi wa mwaka 2010 kufanyika akisema alihofia maisha yake.
Uchaguzi huo ulikuwa wa pili kufanyika tangu kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu miaka 12.
Aliambia BBC kuwa yeye anaunga mkono demokrasia hasa kwa kuwa uchaguzi mkuu unatarajiwa kufanyika mwaka 2015.
"Wakati wa silaha umekwisha,'' alisema.
alikanusha ripoti kuwa alikimbia nchi jirani ya Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo, akisema kuwa muda wote alikuwa nchini Burundi.
Hata hivyo alisema kuwa angali ana wasiwasi kuhusu usalama wake.
Rais Pierre Nkurunziza na Bwana Rwasa waliongoza makundi ya waasii wa Kihutu waliokuwa wanapigana dhidi ya jeshi lililokuwa na watu wengi wa kabila la wa Tutsi waliokuwa wachache,wakati wa vita vya wenyewe kwa wnyewe vilivuosababisha vifo vya watu laki tatu.
Chama cha Rwasa cha FNL kilikataa kumaliza uasi wakati makundi mengine yaliyokuwa yanapigana kuungana na kuunda serikali ya muungano iliyofuatiwa na uchaguzi wa mwaka 2005.

Wednesday, July 31, 2013

UN yaamrisha M23 kusalimisha silaha


Waasi wa M23

Umoja wa Mataifa umewapa wapiganaji wa M23 walioko Mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia
saa 48 kusalimisha silaha, la sivyo watakabiliwa kijeshi.
Kikosi maalum cha Umoja wa Mataifa cha wanajeshi 3000 kitasaidiana na jeshi la Congo kuweka eneo la usalama mjini Goma.Kikosi hicho kimekubaliwa kutumia nguvu dhidi ya waasi wanaolaumiwa kwa kuwaua raia katika maeneo karibu na mji wa Goma.
Mapema mwezi huu mapigano kati ya M23 na jeshi la Congo yalizuka mashariki mwa nchi ambapo Umoja wa Mataifa ulilaumu waasi wa M23 kwa kuwaua kiholela raia katika eneo la Mutaho viungani mwa Goma.
Taarifa ya Umoja wa Mataifa umewataka waasi wote na raia walioko Mashariki mwa Congo kusalimisha silaha walizonazo katika kambi ya jeshi la Umoja wa Mataifa ifikapo Alhamisi jioni.Onyo hilo limeongeza yeyote atakayepatikana na silaha atachukuliwa kuwa mpiganaji.
Hali ya usalama imeendelea kudorora Mashariki mwa nchi na onyo la sasa linanuia kuzuia waasi dhidi ya kukaribia mji wa Goma. Takriban watu 70,000 wamekimbia makwao, kufuatia mapigano kati ya jeshi na waasi. Umoja wa Mataifa unasema Wengi wamekimbilia nchi jirani ya Uganda.

Aliyekuwa Kiongozi wa zamani Mali aongoza kwa Kura


Ibarhim Boubakar Keita
Waziri Mkuu wa zamani nchini Mali Ibrahim Boubakar Keita anaongoza kwa kura za Urais, katika uchaguzi unaonuia kurejesha utawala wa demokrasia nchini humo. Duru za serikali zinasema aliyekua Waziri wa Fedha, Soumaila Cisse anafuata bw keita, huku thuluthi moja ya kura ikiwa imehesabiwa.
Upande wa Bw. Cisse imepinga matokeo hayo na kutaka tume ya kimataifa kuhesabu kura za uchaguzi huo wa Jumapili. Mali ilikumbwa na mapinduzi ya kijeshi mwaka jana pamoja na maasi Kaskazini mwa nchi. Ufaransa ilituma kikosi cha wanajeshi 4,000 kuyakomboa maeneo ya kaskazini kutoka kwa wanamgambo wa kiisilamu.
Vuguguvu la Ukombozi wa jamii ya Tuareg ikisaidiana na wapiganaji wa kiisilamu walitwaa eneo nzima la Kaskazini, kabla ya muungano huo kusambaratika. Makundi hayo yalifanikiwa kunyakua Kaskazini mwa nchi baada ya jeshi kuipindua serikali ya kiraia ikilalamikia kutopata ufadhili kukabiliana na maasi Kaskazini mwa nchi.
Mapema mwezi huu, kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa kilitumwa Mali ili kusaidia katika shughuli za uchaguzi na kurejesha utawala wa kidemokrasia.Ufaransa umepongeza uchaguzi wa Mali, huku Muungano wa Ulaya ukisema shughuli hiyo ilifanyika bila visa vyovyote. Bw Keita maarufu kama "IBK" ana sifa ya kuwa na mabavu.
Mwanasiasa huyo aliendesha kampeini yake kwa ujumbe wa kurejesha hadhi kwa Mali akisema taifa liliisha hadhi yake kwa kuomba msaada wa Ufaransa ili kuinusuru dhidi ya kuporomoka.Viongozi wa kidini wengi wakiwa Waisilamu waliwaomba raia kumpigia kura, pia anaonekana kuungwa mkono na jeshi. Bw. Cisse aliunda chama cha Union for the Republic and Democracy (URD) mwaka wa 2003 na ametaka jeshi kutojihusisha na siasa.Jumla ya wagombea 27 walichuana Urais, huku watu milioni 6.8 wakijiandikisha kupiga kura nchini Mali.

Afya ya Mandela yaendelea kuimarika


Mandela alitaka sana kuona kuwa kombe la dunia 
linachezewa nchini humo
Rais mstaafu nchini Afrika Kusini , Nelson Mandela aliyelazwa hospitalini tangu tarehe nane mwezi Juni, anaonyesha dalili za afya yake kuimarika.
Hii ni kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa serikali. Hata hivyo Mandela mwenye umri wa miaka 95 angali hali mahututi ambayo inadhibitiwa na madaktari.
Rais Jacob Zuma amewataka watu kuendelea kumuombea Mandela na kuwashukuru wale waliotenda mema kwa niaba ya Mandela.
Mandela ambaye ni rais wa kwanza wa nchi hiyo kuchaguliwa kidemokrasia, anatazamiwa na wengi kama baba wa taifa.
Alifungwa jela miaka 27 baada ya kuanzisha vita dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi.
Anajulikana na ukoo wake kwa jina Madiba, na alichaguliwa kama rais wa Afrika Kusini mwaka 1994 baada ya wazungu kumaliza utawala wao na kisha akaondoka mamlakani baada ya miaka mitano ya kutawala nchi.
Katika taarifa yake, bwana Zuma alitoa wito kwa wafanyabiashara kuunga mkono mradi unaofadhiliwa na wakfu wa Mandela kujenga hospitali ya watoto.
"Madiba anapenda sana watoto, na anawatakia afya nzuri. Anatutaka tuhakikishe kuwa wanaishi maisha mazuri katika siku za baadaye,'' alisema Zuma.
Wakfu wa Mandela , ungependa kujenga hospitali yenye uwezo wa kuwashughulikia watoto 238 wa kulazwa pamoja na kuwatibu watoto kote nchini Afrika Kusini.

Thursday, July 18, 2013

AMISOM yakutana kuhusu kuchangia taarifa

 
Harakati za AMISOM Somalia
Ujumbe wa Muungano wa Afrika nchini Somalia (Amison), kwa ushirikiano na wahisani wake, umeanza mkutano hii leo na washirika wake mjini Mombasa Pwani ya Kenya kuhusu kuchangia habari na taarifa muhimu.
Lengo la mkutano huo ni kubuni mpango utakaowezesha nchi zilizochangia wanajeshi kwa AMISOM kuchangia taarifa mara kwa mara kati ya Amisom, mashirika ya usalama nchini Somalia na mashirika mengine ya kikanda .
Mkutano huo wa siku tatu, umehudhuriwa na maafisa kutoka mashirika ya usalama nchini Somalia, viongiozi wa nchi zilizo na vikosi vyao nchini Somalia, waakilishi kutoka Ethiopia, Sudan Kusini, Mali, Chad, IGAD , AU na wengineo.
Akiongea wakati wa sherehe ya ufunguzi wa mkutano huo, mjumbe maalum wa muungano wa Afrika nchini Somalia,Mahamat Saleh Annadif aliwakumbusha washirika kuwa vitendo vya kigaidi vinavyofanywa nchini humo havina mpaka.
Kwa hivyo, vita dhidi ya ugaidi lazima vifanywe kwa mpangilio unaofaa. Baada ya kukabiliwa na changamoto nyingi, kundi la Al-Shabab limeanza kubuni njia mbadala za kupambana na maadui wake kwa kukusanya taarifa za kijasusi.
Mkutano huu unatarajiwa kuangazia kwa kina hali inayokumba Somalia hususan vitendo vya kigaidi, uhalifu wa kupangwa na kuongezeka kwa idadi ya silaha ndogondogo
Pia unalenga kuimarisha miundo mbinu ili kuwezesha nchi kuchangia taarifa wakati wote pamoja na mengi mengineyo.

Mzee Nelson Mandela afikisha miaka 95

 
Leo ni siku ya kimataifa ya shujaa wa kupinga Ubaguzi wa Rangi Afrika Kusini, Nelson Mandela.
Rais mstaafu wa Afrika Kusini Nelson Mandela pia anaadhimisha siku ya kuzaliwa leo akitimiza miaka 95 akiwa bado amelazwa hospitalini.
Mandela amelazwa hospitalini kutokana na matatizo ya kupumua.
Serikali ya Afrika Kusini imewaomba wananchi wake kusaidia watu wasiojiweza na kutenda mema kama heshima kwa Madiba.
Rais Barack Obama alimtakia kila la heri Mandela anayetambulika kama shujaa wa vita dhidi ya ubaguzi wa rangi.
Madiba anasalia hospitalini mjini Pretoria, lakini madaktari wake wamethibitisha kuwa afya yake inaendelea kuimarika.
Naye rais Jacob Zuma amemtakia kila la heri Mandela katika sherehe za siku ya kuzaliwa kwake.
Watoto kwenye shule kote nchini humo walitarajiwa kuanzisha sherehe hizo kwa kumuimbia Mandela wimbo wa kusherehekea siku ya kuzaliwa kwake katika siku ambayo pia iliadhimishwa miaka kumi na mitano ya ndoa yake kwa mke wake wa tatu Graca Machel.
Mwanawe Mandela wa kike, Zindzi, alisema Jumatano kuwa afya ya Mandela imeimarika pakubwa na kwamba alimpata akiwa anatazama televisheni huku akiwasiliana kwa macho yake na mikono alipomzuru wiki jana.
''Nina matumaini kuwa atarejea nyumbani wakati wowote sasa'' Zinzi aliambia shirika la habari la Uingereza Sky News.
Siku ya kimataifa ya Mandela iliwekwa na umoja wa mataifa kama njia ya kumkumbuka mshindi huyo wa tuzo ya amani ya Nobel kwa juhudi zake za kupatanisha watu.
Mandela anasifika kote duniani kwa juhudi zake za kumaliza vita vya ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini. Baadaye alichaguliwa kama rais wa kwanza mwafrika wa nchi hiyo mwaka 1994.
Chama cha kitaifa cha (ANC) kimesema kuwa katika siku hii ya kusherehekea siki ya kimataifa ya Mandela, ni heshima kwa miaka yake 95 kwa maisha yake aliyoishi vyema na ambayo ameitumia kupigania wananchi wa Afrika Kusini.

Mashahidi 2 wajiondoka kwa kesi ya Kenyatta


Fatou Bensouda
Kiongozi wa mashtaka katika mahakama ya kimataifa ya ICC Fatou Bensouda, amesema kuwa mashahidi wawili wametupilia mbali ushahidi wao katika kesi dhidi ya rais wa Kenya Uhuru Kenyatta
Bi Bensouda alisema mashahidi nambari 5 na 426 wamefutilia mbali ushahidi wao kwa sababu za waswasi kuhusu usalama wao.
"kwa kifupi, inaonekana kuwa wasiwasi wa shahidi nambari tano, wameogopa sana kuhusu usalama wao na kuwa athari za kutoa ushahidi wake huenda zikawa na madhara makubwa kwa maisha yake na kwa hivyo akaamua kufutia mbali ushahidi wake.'' alisema Bensouda kwa ujumbe wake kwa majaji mnamo Jumanne.
Aliongeza kuwa upande wa mashtaka, ulikuwa umefanya mashauriano na shahidi nambari 426 kumtaka abadili msimamo wake, lakini mazungmzo hayakufua dafu.
"upande wa mashtaka umefanya mazungumzo na shahidi 426 kujua ikiwa hatua zozote zinaweza kuchukuliwa kuodnoa wasiwasi wake pamoja na kumwezesha kuhudhuria kesi. Mazungumzo hayo, hata hivyo hayakufua dafu baada ya kusisitiza kuwa hayuko tayari kutoa ushahidi wake, '' aliongeza kusema Bi Bensouda said.
Hata hivyo mwendesha mashtaka aliwaaambia majaji kuwa ushahidi wao sio muhimu tena kwa ushahidi wake dhidi ya mtuhumiwa.
Kesi dhidi ya Uhuru Kenyatta itaanza kusikilizwa Novemba 12.

Friday, July 12, 2013

Malema azindua chama cha kisiasa


Julius Malema kiongozi wa chama cha EFF
Aliyekuwa kiongozi wa vugu vugu la vijana la chama tawala nchini Afrika Kusini cha ANC, Julius Malema amezindua kundi la kisiasa litakalojulikana kama Wapiganiaji wa Uhuru wa Kiuchumi au Economic Freedom Fighters, EFF.
Malema, ambaye alitimuliwa kutoka kwa chama cha ANC, mwaka wa 2012, amesema chama chake cha EFF kinataka zoezi la kugawanya mashamba kuanzisha upya na pia kutaifishwa kwa migodi yote ya madini.
''Tutagawana ardhi sisi zote ukiwa mweusi au mweupe. Lakini ukikataa kugawanya itamaanisha kuwa utalazimishwa kufanya hivyo'' Alisema Bwana Malema.
Ametaja dhamira kuu ya vugu vugu hilo kuwa kupamabana mfumo wa kipebari.
Akiwa amevalia kofia nyekundu iliyo na maandishi ''Amirijeshi Mkuu wa EFF'' Bwana Malema amewaambia waandishi wa habari kuwa chama chake kimebuniwa ili kutetea maslahi ya raia wanaoteseka katika maeneo ya mashinani.

EFF kukupambana na ANC katika uchaguzi mkuu

Rais wa Afrika Kusini na Kiongozi wa chama cha ANC Jacob Zuma
Malema ambaye alikuwa mmoja wa washirika wa karibu wa rais Zuma, kwa sasa ni mmoja wa wakosoaji wakubwa na aliongoza mikakati ya kumuondoa kama kiongozi wa chama cha ANC wakati wa mkutano wa baraza kuu la chama hicho mwaka wa 2012.
Malema ameshutumu rais Zuma kwa kutoimarisha juhudi za kuwasaidia raia weusi wa nchi hiyo ambao ni masikini na waliompigia kura.
Hata hivyo haijabainika ikiwa atawania kiti chochote katika uchaguzi mkuu utakaoandaliwa mwaka ujao, akisema kuwa uamuzi huo utatolewa baada ya mkutano wa baraza kuu la chama hicho cha EFF utakaofanyika mwisho wa mwezi huu.
Wachanganuzi wa kisiasa wanasema idadi kubwa ya raia wa Afrika Kusini, wamepoteza imani na chama cha ANC, ambacho kimekuwa madarakani tangu mwaka wa 1994.
Rais wanasema maafisa wengi wa chama hicho ni wafisadi na hawana nia ya kuimarisha hali ya maisha.

Serikali yarejesha mawasiliano ya Simu


Ramani ya Nigeria
Serikali ya Nigeria imesitisha mpango wake wa kuzuia mawasiliano ya simu katika jimbo moja kati ya majimbo matatu ambayo hali ya hatari imetangazwa kwa sababu ya mashambulio ya mara kwa mara kutoka kwa wanamgambo.
Jimbo la Adamawa halijaadhiriwa pakubwa na mashambulio hayo yanayofanywa na wapiganaji wa Kiislamu wa Boko Haram.
Wiki iliyopita, afisa mmoja mwandamizi wa serikali alisema kuwa ukosefu wa mawasiliano ya simu, ulizuia raia kutoa habari kwa serikali wakati shule moja ilipovamiwa.
Lakini jeshi la nchi hiyo limesema, uamuzi huo ulichukuliwa ili kuzuia wanamgambo hao kupanga mashabulio hayo.
Kundi la Boko Haram linadaiwa kuwaua zaidi ya watu elfu mbili tangu ilipoanzisha mashambulio yake mwaka wa 2009.
Wizara ya Ulinzi nchini Nigeria, limesema hali ya ulinzi imeimarika katika jimbo hilo la Adamawa.
Mwandishio wa BBC nchini Nigeria, alifanikiwa kuwasiliana na mkaazi mmoja wa jimbo hilo la Adamawa mapema siku ya Ijumaa.
Hata hivyo mawasiliano katika majimbo jirani ya Yobe na Borno bado yamekatizwa.
Mwezi Juni mwaka huu jeshi la nchi hiyo lilitangaza kuwa mtu yeyote atakayepatikana na simu ya Satellite katika jimbo la Borno atakamatwa.
Baadhi ya simu zilizopigwa marufuku Nigeria
Wiki iliyopita, Gavana wa Jimbo la Yobe Ibrahim Gaidam aliagiza shule zote za sekondari kufungwa baada ya wanafunzi ishirini na wawili kuuawa na shule yao kuteketezwa na wapiganaji wa Boko Haram.
Gavana huyo hata hivyo alitoa wito kwa serikali kurejesha mawasiliano ya simu ili kusaidia raia kutoa habari kwa utawala wakati kunapotokea mashambulio.
Mawasiliano ya simu za nyaya nchini Nigeria mara nyingi hazifanyi kazi nje ya miji mikuu ya Abuja na Lagos.
Wanajeshi zaidi wametumwa katika majimbo ya Kaskazini mwa Nigeria tangu serikali ilipotangaza hali ya tahadhari.
Kundi la Boko Haram, ambalo majina yake yanamaanisha Elimu ya mataifa ya Magharibi hairuhusiwa, inataka sheria za Kiislamu kutumika katika eneo la Kaskazini lenye idadi kubwa ya waumini wa dini ya Kiislamu.

Mwana Mfalme akamatwa California


Meshael Alayban
Mama mmoja ambaye ametajwa kuwa mwana mfalme kutoka Saudi Arabia amekamatwa katika jimbo la California nchini Marekani na kutuhumiwa kuhusika na ulanaguzi wa watu.
Meshael Alayban, 42, anakabiliwa na mashtaka ya kumlazimisha mama mmoja kutoka Kenya kufanya kazi kwa zaidi ya masaa kumi na sita kila siku, na kumlipa kiasi kidogo cha pesa kuliko walivyokuwa wameafikiana.
Utawala wa eneo hilo, umesema kuwa Bi Alayban alichukua pasi ya kusafiria ya mama huyo, hatua iliyomfanya atoroke.
Mawakili wa mwana mfalme huyo wametaja kesi hiyo kuwa mzozo kuhusu hali ya utendaaji kazi.
Novemba mwaka uliopita, wapiga kura katika jimbo la California, waliidhinisha sheria kali dhidi ya watu watakaopatikana na hatia ya kuhusika na ulanguzi wa watu.
Ikiwa atapatikana na hatia, Bi Alayban, huenda akahukumiwa kifungo cha miaka kumi na miwili gerezani, adhabau ambayo ni asilimia mia moja zaidi kuliko ilivyokuwa kabla ya wapiga kura kuidhinisha mageuzi sheria hiyo mpya.
Waendesha mashtaka wanasema Bi Alayban, ni mmoja wa wake sita wa Mwana Mfalme Abdulrahman bin Nasser bin Abdulaziz al-Saud, mmoja wa wanawe wa kiume wa familia moja ya kifalme nchini Saudi Arabia.

Mtumwa

Mama huyo kutoka Kenya ambaye jina lake halijatolewa, aliajiriwa na Bi Alayban miaka miwili iliyopita, baada ya kusaini mkataba na shirika moja la kutoa uajiri nchini Saudia.
Mama huyo alihaidiwa kulipwa dola elfu moja mia sita kila mwezi na kuwa atafanya kazi masaa manane kila siku kwa siku tano.
Lakini, Bi Alayban amekuwa akimlipa dola mia mbili ishirini kila mwezi na kulazimishwa kufanya kazi kwa zaidi ya masaa kumi na sita kila siku.
Mama huyo kutoka Kenya vile vile amedai, kupokonywa pasi yake ya kusafiria na alikabithiw muda mfupi tu kabla ya wao kusafiri kwenda Carlifonia na Bi Alayban.
Akiwa California, alilazimishwa kufanya majukumu mengi zaidi ya kinyumbani kwa familia ya watu wanane waliokuwa katika vyumba vinne tofauti, ambako amedai alizuiliwa mateka.
Wakati alifanikiwa kutoroka, alisimamisha basi moja na kwenda moja kwa moja hadi kituo cha polisi.
Biu Alayban alikamatwa siku ya Jumatano na kufikishwa mahakamani siku ya Alhamisi.
Aliachiliwa huru kwa dhamani ya dola milioni tano na kuamriwa kurejesha pasi ya kusafiria ya amama huyo kutoka Kenya.
Aidha Bi Alayban sasa atavalia chombo maalum ambacho kitatoa maelezo ya mahala aliko na hataruhusiwa kuondoka Marekani hadi kesi hiyo itakapokamilika.
Viongozi wa Mashtaka walitaka jaji kumuachilia kwa dhamani ya dola milioni Ishirini au anyimwe dhamana kwa kuwa yeye ni tajiri mkubwa na aweza kutoweka.

Friday, June 7, 2013

Maandamano sharti yakome'', Erdogan


Maandamano yamekumba mji wa Istanbul kwa zaidi ya waiki moja sasa
Waziri Mkuu wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan ametaka maandamano yanayoendelea nchini humo kumalizika mara moja.
Akiwahutubia maelfu ya wafuasi wake waliomlaki katika uwanja wa ndege wa Istanbul,kiongozi huyo amesema maandamano hayo sio halali.
Lakini alipokuwa akiongeza maelfu ya waandamanaji wanaopinga serikali walikuwa wanakusanyika mjini Istanbul katika bustani ya Taksim.
Maandamano hayo yalianza kama maandamano madogo kuhusu bustani moja mjini Istanbul ingawa yakaongezeka na kuwa maandamano makubwa.
Wafuasi 10,000 wa chama cha Bwana Erdogan, walikwenda uwanjani kumkaribisha baada ya ziara yake ya Kaskazini mwa Afrika.
Akisimama kando ya mkewe na mawaziri wa serikali, aliwaambia wafuasi wake kuwa maandamano hayo ni kinyume na sheria na lazima yakomeshwe mara moja.
"sisi hatujawahi kuunga mkono mgawanyiko katika jamii lakini hatuwezi kuunga mkono watu wenye nia ya kuwagawanya watu.''
Erdogan aliwasihi wafuasi wake kuwa watulivu baada ya kuelezea nia yao ya kutaka kulipiza kisasi.
"mmekuwa watulivu , mmeonyesha ukomavu na kutumia akili zenu, sote tutakwenda nyumabi kutoka hapa.''
Bwana Erdogan alijibu wito wa watu kutaka ajiuzulu akiwakumbusha uchaguzi wa mwaka 2011 ambapo alishinda uchaguzi huo kwa asilimia hamsini.
''Wanasema kuwa mimi ni waziri mkuu wa asilimia hamsini ya nchi. Tumewahudumia watu milioni 76 kutoka Mashariki hadi Magharibi,'' alisema Erdowan
Ilikuwa mara ya kwanza wafuasi wa Erdogan wamemuunga mkono, kufuatia wiki moja ya maandamano ambayo yamemtaka aondoke mamlakani.
Mwandishi wa BBC Mark Lowen mjini Istanbul, anasema kuwa kukaribishwa kwa waziri mkuu,kwa namna hiyo ni ishara ya uungwaji mkono alionao kutoka kwa wafuasi wake.
Hata hivyo,baadhi wanasema kuwa matamshi ya Bwana Erdogan huenda yakachochea maandamano hayo zaidi.
Migawanyiko nchini Uturuki, inaonekana kukithiri zaidi katika siku zijazo na huenda hali ikawa ya hatari kubwa.

US harvesting data from Facebook, Google and other internet giants


America's secret surveillance state was dragged further out of the shadows on Thursday as it emerged that the US is reaching directly into the servers of Facebook, Google and other internet companies to harvest data.
Facebook Mark Zuckerberg
Facebook is among at least nine tech companies that make up the NSA's PRISM programme. 
The National Security Agency's (NSA) classified PRISM programme reportedly allows the government to collect virtually limitless amounts of information from emails, pictures and social media accounts.
The disclosure of the programme comes one day after it emerged that the government has been tracking the phone calls of millions of Americans for the last seven years, sparking accusations the Obama administration is trampling civil liberties.
Unlike the phone tracking programme, where telecom companies are forced to hand over records, PRISM appears to allow the NSA to freely search the tech firms' networks at any time.
PRISM also allows the government access to the content of online accounts, whereas the phone programme provides data on the time and location of a call but does not tell investigators what was said.
A secret slide show obtained by The Guardian and The Washington Post appear to indicate that the nine companies are willing participants in the programme, beginning with Microsoft in 2007.

Tuesday, June 4, 2013

Evidence that chemical weapons have been used in Syria attacks reaches UN

Chemical weapons have been used in at least four attacks Syria as crimes against humanity are perpetrated every day, according to a UN inquiry.
Free Syrian Army fighters preparing  to fire on Syrian army positions in the old city area of Aleppo
Free Syrian Army fighters preparing to fire on Syrian army positions in the old city area of Aleppo Photo: EPA
The UN Commission of Inquiry on Syria said in a report that both sides were deliberating breaking the rules of war against millions of victims.
"War crimes and crimes against humanity have become a daily reality in Syria," the Commission of Inquiry on Syria said in a report delivered to the UN Human Rights Council in Geneva, adding it had "reasonable grounds to believe that chemical agents have been used as weapons.
The regime of President Bashar al-Assad was accused of a "concerted policy" of massacre and forced displacement of civilians against the nationwide rebellion it faced. Meanwhile rebels could also have used chemical weapons as well as the regime.
In their latest report, based on interviews with victims, medical staff and other witnesses, they said they had received allegations that Syrian government forces and rebels had used the banned weapons, but that most testimony related to their use by state forces.
"There are reasonable grounds to believe that limited quantities of toxic chemicals were used. It has not been possible, on the evidence available, to determine the precise chemical agents used, their delivery systems or the perpetrator," Paulo Pinheiro, who chairs the U.N. commission of inquiry, told a news conference in Geneva.

Monday, June 3, 2013

SMZ: Muungano ukivunjika Tanganyika na Zanzibar zitayumba

Balozi Seif Ali Iddi akimnadi mgombea nafasi ya Ubunge kupitia chama cha Mapinduzi (CCM) Nd. Mattar Sarhan Said. Hii ilikuwa ni kwenye uzinduzi wa kampeni ya uchaguzi mdogo wa Jimbo la Chambani.
Balozi Seif Ali Iddi akimnadi mgombea nafasi ya Ubunge kupitia chama cha Mapinduzi (CCM) Nd. Mattar Sarhan Said. Hii ilikuwa ni kwenye uzinduzi wa kampeni ya uchaguzi mdogo wa Jimbo la Chambani.
Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd amewataka Wazanzibari kutafakari kwa kina na kutokubali kushabikia kuvunjika kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar bila ya kuangalia hasara na tija za kiuchumi na kimaendeleo.Balozi Seif alitoa tamko hilo kufuatia kampeni zilizoibuka Zanzibar za kutaka kuvunja Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kuratibiwa na baadhi ya wanasiasa, wafanyabiashara na jumuiya za kidini kupitia mjadala wa mabadiliko ya katiba unaoendelea nchini.
Akihutubia mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo Chambani huko Pemba, Balozi Seif alisema wako wanasiasa wanaopigania maslahi binafsi wakiwa na lengo na kuisambaratisha misingi ya Mapinduzi na Muungano.
Alisema Tume ya mabadiliko ya Katiba haikuundwa kwa malengo ya kuvunja muungano na kuwataka wananchi kujiepusha pia wakitafakari kwa umakini na utulivu kwa vile athari za kuvunjika kwa muungano ni kubwa kuliko inavyotazamiwa.
“Tume ya mabadiliko ya katiba haina hadidu ya rejea ya kuvunja muungano, wanachotakiwa wazanzibari kuainisha kasoro zote zilizopo na kuzipatia ufumbuzi bila ya kuongozwa na jazba ya kuvunja muungano uliopo,”alisema Balozi Seif.
Akionekana kushagazwa na matamshi ya baadhi ya wanasiasa wanaotaka muungano wa mkataba bila ya kuonyesha mfumo wa uendeshaji wake, alisema iwe ni mwiko kwa watu hao kutumia jina la wazanzibari wote kwamba hawataki muungano uliopo.
Alisema kuna kikundi cha watu ambao mawazo yao kwa miaka mingi ni kuukataa muungano na si Wazanzibari wote huku akisema kwamba muungano huo umeleta tija na faida zaidi kwa Wazanzibari kuliko Watanganyika.
“Wenye maduka makubwa, wafanyabiashara, wakulima na majumba ya kifakhari huko Tanzania Bara ni Wazanzibari tena wenye asili ya Pemba, kuvunjika kwa muungano kutawapa athari na hasara badala ya faida zinazopatikana sasa,”aliasa Balozi Seif.
Alisema maneno hayo ya kishabiki ni sawa na kuwakaangia mbuyu watu waliojijenga kiuchumi, kimiradi na kimaendeleo kwasababu alisema anaamini nje ya muungano lolote lenye hasara na mtikisiko linaweza kutokea.
“Amani na umoja wa kitaifa ukivurugika, kina mama na watoto ndiyo waathirika wakubwa, amani ni mfano wa mke ukimpa talaka ni taabu kumpata tena, tumezishudia  nchi za Sudan Kusini na Kaskazini, Ethiopia na Eritrea, zimeyumba na kukosa utulivu wa ndani,”alisema.
Aidha  alisema inashangaza kusikia baadhi ya watu hasa wanasiasa wakisema Wazanzibari wote hawataki muungano bila ya kutoa takwimu na ushahidi wa maneno hayo, walikutana wapi, waliazimia mambo gani kuhusu jambo hilo hadi kujumuishwa na kudaiwa hawataki muungano.
Msimamo huo wa Serikali umekuja kufuatia kongomano lililokuwa likijadili mwelekeo wa Muungano wakati huu wa mjadala wa katiba mpya ambalo lilifunguliwa na Makamo wa kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad katika ukumbi wa Bwawani mjini Zanzibar mwishoni mwa wiki.

Waingereza pia wana “Kero za Muungano”

Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron akihutubia katika mkutano wa EU mwezi Mei 2012 huko Ubelgiji
Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron akihutubia katika mkutano wa EU mwezi Mei 2012 huko Ubelgiji
Licha ya kupita miaka 40 tangu Uingereza ijiunge na Muungano wa Ulaya ( wakati huo jina lilikuwa Jumuiya ya Uchumi ya Ulaya), bado mabishano yangaliko miongoni mwa raia wa visiwa hivyo kuhusu „kero“ ndani ya Muungano huo, na kama ni bora hivi sasa nchi hiyo ijitoe. Hali hiyo imezifanya nchi nyingine shirika ndani ya Muungano huo kulalamika kwamba Uingereza ni korofi, inazuwia mwenendo wa kuzidi kuiunganisha Ulaya itakayokuwa imara zaidi na huenda siku moja kuwa na serikali moja.
Licha ya kwamba Januari mwaka huu waziri mkuu wa Uingereza, David Cameron, alitangaza kwamba huenda, baada ya uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015, na pindi yeye atashinda katika uchaguzi huo, Waingereza wakatakiwa wapige kura ya maoni hapo mwaka 2017 kama wanataka nchi yao ibakie ndani ya Muungano wa Ulaya, bado kuna wabunge kutoka chama chake mwenyewe cha Conservative walioonesha hawajatosheka tu na ahadi hiyo ya kiongozi wao. Walitaka zaidi, na kumbinya Cameron aweke wazi- kupitia sheria itakayotungwa- kwamba kura hiyo ya maoni hakika itafanyika, na isitegmee chama chake kushinda uchaguzi ujao au yeye kubakia madarakani hadi wakati huo. Pia wala isitegemee matokeo ya mashauriano ambayo Uingereza inataka yafanyike ili ijipatie masharti mepya yalio bora kuweza kubakia katika Muungano huo.
Wiki iliopita wabunge 130, wengi wao wakiwa kutoka Chama cha Conservative ambao wanakerwa na mfumo wa Muungano wa Ulaya na namna nchi yao inavotendwa, waliwasilisha bungeni mswada uliolaumu msimamo wa serikali yao kuelekea Muungano huo. Ilikuwa kama kumpiga kibao cha usoni David Cameron. Mswada huo ulishindwa kupita bungeni, lakini ulitoa ishara muhimu ya kisiasa.
Ni wazi kwamba hisia za Waingereza wengi kupinga nchi yao kubakia ndani ya Muungano wa Ulaya  zinazidi, japokuwa wachache kati yao ni kutokana na uzalendo kuliko kuangalia hali halisi ya mambo. Mada juu ya werevu wa kuitisha kura ya maoni inabakia katika vichwa vya habari, na hata katika chaguzi za karibuni za serikali za mitaa chama cha Ukip, kinachotaka Uingereza itoke kutoka Muungano wa Ulaya, kilifanikiwa kupata kura nyingi za kutoka wanachama wa chama tawala cha Conservative. Chama hicho cha Ukip katika uchaguzi ujao huenda kikaweza kukipotezea ushindi chama cha Conservative, na kuwacha njia wazi kwa chama cha Labour kuingia madarakani. Wanachama wengi wa Chama cha Conservative hivi sasa wanataka viongozi wao watamke wazi na bayana kuhusu nchi yao kubakia ndani ya Muungano.
Kilichowaudhi wabunge hao waliowasilisha mswada wao ni kwamba katika hotuba ya karibuni alioitoa malkia bungeni- ambayo ni programu ya serikali kwa siku zijazo- hakujatajwa kwamba serikali itawasilisha rasimu ya sheria bungeni kuhusu kuitishwa kura ya maoni. Kwa hakika David Cameron asingepinga serikali yake kuwasilisha rasimu ya aina hiyo. Lakini ana tatizo. Nalo ni kwamba serikali yake ni ya mseto ambapo ndani yake kuna chama cha Liberal Democratic kinachopinga au mara nyingine kutia na kutoa kuhusu suala la kuitishwa kura ya maoni. Kwa hivyo, Cameron alijitafutia njia ya katikati, kuihifadhi nafasi na heshima yake ya kisiasa katika chama chake na, wakati huo, angalau, kuwaridhisha wabunge wa chama chake. Aliwakubalia kichinichini wabunge hao wawasilishe mswada wao, akijuwa wazi kwamba hautapita, kwani utapingwa na kura nyingi za wabunge wengine wa chama chake cha  Conservative, wale wa chama kikuu cha upinzani cha Labour na pia wa chama cha Liberal Democratic. Na hilo ndilo lilotokea.
Kama yalivyo mabishano miongoni mwa raia, hali ni vivyohivyo ndani ya vyama vikuu vya kisiasa huko Uingereza. Chama kikuu cha upinzani cha Labour, licha ya kufurahia mabishano yaliozuka ndani ya chama cha Conservative, nacho kina wasiwasi na wazo la kuitishwa kura ya maoni, kikihofia hali itakayochomoza pindi wananchi wengi wataipa mgongo Ulaya. Chama hicho kinaiona taswira ya Uingereza itakayozidi kutengwa na Ulaya. Na japokuwa matokeo ya kura ya maoni yatabidi yaheshimiwe kwa vyovyote, lakini hakitaki kubeba dhamana wa mustakbali usiojulikana. Chama cha Labour kinapendelea Uingereza ifanye mashauriano zaidi hivi sasa na izidi kuzibinya nchi nyingine za Muungano huo ziyaridhie matakwa yake na kuziondoa zile inazoziita „kero“ za Muungano. Baadhi ya viongozi wa Chama cha Labour wameweka wazi kwamba pindi patakuweko mabadiliko ya mkataba wa sasa wa Muungano ambayo yatabadilisha wizani wa nguvu, ambapo matakwa ya Uingereza yatakubalika, basi huenda wao wataunga mkono iitishwe kura hiyo ya maoni. Na suala muhimu ni kama kura hiyo ya maoni itakuwa ni kujibu suali moja tu- nalo: Uingereza ibakie ndani ya Muungano wa Ulaya au itoke?
Waingereza kadhaa wanaziona faida za Muungano wa Ulaya kama taasisi yenye kuendeleza utandawazi na uchumi wa kiliberali ndani ya soko la watu milioni 500. Lakini wana wasiwasi juu ya mipango ya Muungano huo ya kuziwekea kanuni kali taasisi za fedha na mabenki ambayo mengi yanafanya shughuli zao mjini London, hivyo mji huo kuwa kituo muhimu cha shughuli za fedha duniani. Pia chama cha Conservative hakiridhishwi na sheria za ajira za  Muungano huo, hasa zile zinazohusu masaa ya kufanya kazi, ambazo inaona zinazibana shughuli za kibiashara za Uingereza. Malalamiko yamezagaa huko Uingereza kwamba Uingereza huwekwa pembeni yanapokuja masuala muhimu ya siasa ya fedha, kwamba Tume ya Umoja wa Ulaya huko Brussels hujititimua na kuonesha misuli kama vile ni serikali ya Ulaya, inajiingiza katika mambo ambayo ni dhamana za serikali za nchi wanachama, licha ya kuwa pia na bajeti kubwa inayopita kiasi.
Licha ya kwamba asilimia 70 ya watu wa visiwa hivyo wanataka iitishwe kura ya maoni kuhusu mustakbali wa nchi yao ndani ya Ulaya, wako baadhi yao wanaotambua kwamba kuna mambo mengi ya kuwashughulisha zaidi- madeni ya serikali yanayozidi, uchumi kukwama na kashfa za kisiasa zisizokwisha. Pia wanakumbusha kwamba nusu ya uekezaji wa moja kwa moja nchini humo unatokea nchi nyingine za Muungano wa Ulaya, na nusu ya bidhaa ambazo London inasafirisha ng’ambo zinakwenda katika nchi za Muungano. Wanadai kwamba kujitoa kutapunguza nafasi za ajira, kutafanya uhusiano wa kimataifa wa nchi yao unywee na kutapunguza utajiri wa nchi yao.
Manung’uniko hayo ya Uingereza yanawakumbusha watu wa Ulaya juu ya shakashaka alizokuwa nazo rais wa Ufaransa, marehemu Charles de Gaulle, pale Uingereza ilipoomba kuwa mwanachama wa Muungano wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Ulaya. Yeye aliashiria kwamba Waingereza, kama wanavisiwa, wana hamu kubwa ya kulinda uhuru na heshima ya utawala wao. Kinachoonekana sasa ni kwamba kwa Waingereza kwao Muungano wa Ulaya ni njia tu ya kufikia lengo walilokusudia na si kwamba Muungano huo ni makusudio na lengo lao la mwisho.
Kuna nchi ndani ya Muungano ambazo haziko tayari kuikubalia Uingereza kile inachotaka. Zinahoji kwamba nchi hiyo iliingia ndani ya klabu na ikakubaliana na mashrati ya klabu hiyo pale ilipojiunga, hivyo si haki kutaka kanuni za klabu kutoka sasa zipindwe ili kuiridhisha. Haiwezekani, na kama haitaki basi ina hiyari ya kujitoa. Na yaonesha Waingereza nao huenda wakaamua kutafuta njia mbadala.
Kwa baadhi ya wachunguzi wa mambo ni kwamba Waingereza wanautaka Muungano wa Ulaya, lakini  kwa bei wanaojiwekea wenyewe, na sio kwa bei inayokubaliwa na wanachama wengine. Waingereza wanausahau ule usemi wao wenyewe kwamba mtu hawezi kubakia na keki yake huku anaila. Pia, lakini, wananchi wana kila haki ya kutaka wapige kura ya maoni, licha ya kile kitisho cha msemo wa  Kiswahili: Mtoto akililia wembe mpe.
Othman Miraji Othman
Cologne/Ujerumani
Nambari ya simu: 0653-466577 au +49-2233-21721

e-mail:  mwinjuu@hotmail.com
Chanzo: Mwananchi

MAAJABU,SAMAHIKI HUYU AMEVULIWA HUKO UNGUJA..YAWEZEKANA NDIO KWANZA DUNIANI KUONEKANA

Samaki huyu alivuliwa maeneo ya ''mchangamle kizimkazi Unguja kusini, Watu wengi walikusanyika kumshangaa samaki huyu wa ajabu ambae wavuvi na wakaazi wa maeneo hayo hawakuwahi kumwona, Ndugu msomaji wa

Saturday, June 1, 2013

Syria has become the theatre for international jihad

Analysis: the fate of Ali al-Manasfi provides vivid proof that Syria's revolt is drawing in volunteers from across the world.

Syria identifies British man 'killed fighting with rebels'
Image 1 of 2
Syrian state television showed this passport and identified Ali al-Manasfi from London as having died while apparently fighting with the rebels 
Manasfi's motives for joining the struggle against President Bashar al-Assad are unknown, but Syria has become the number one theatre for international "jihad".
During the 1980s, radical Muslims travelled to Afghanistan to fight the Soviet occupation; later their spotlight fell variously on Chechnya, Kashmir, Iraq and Afghanistan again.
Today, their prime goal is Mr Assad's downfall. As a secular dictator who leads a regime dominated by the Alawite sect – which radical Sunnis regard as heretical – he ranks high in the catalogue of infamy for any follower of al-Qaeda's ideology.
The fact that this places al-Qaeda on the same side as the West is uncomfortable but not unprecedented: the same was true in Afghanistan during the anti-Soviet struggle.
Al-Qaeda leader Ayman al-Zawahiri (AFP)

Iran presidential election debate 'comical'

Iranian newspapers gave a resounding thumbs down to the first televised debate between the candidates for this month's presidential election, echoing criticism from the hopefuls themselves of a format they said stifled real discussion.

Iranian presidential candidates (L to R), former parliament speaker Gholam-Ali Haddad Adel, former first vice president Mohammad Reza Aref, former chief of the Revolutionary Guards Mohsen Rezai and former chief nuclear negotiator Hassan Rowhani attend a live debate on state TV in Tehran: Iran presidential election debate 'comical'
Iranian presidential candidates (L to R), former parliament speaker Gholam-Ali Haddad Adel, former first vice president Mohammad Reza Aref, former chief of the Revolutionary Guards Mohsen Rezai and former chief nuclear negotiator Hassan Rowhani attend a live debate on state TV in Tehran Photo: AFP/GETTY
Conservative candidate Mohsen Rezai, a former commander of the elite Revolutionary Guards, told his own Tabnak website that he would boycott the other two debates scheduled for next Wednesday and Friday if the format does not change.
The reformist Bahar newspaper said the quality of the debate had been "comical".
Another reformist daily, Etemad, commented: "Television has turned the most important political event into an entertainment programme."
Even the hardline Kayhan newspaper said the debate had "failed to live up to expectations".
All eight candidates who secured the approval of Iran's conservative-led electoral watchdog to stand in the June 14 election took part in the four-hour debate.

Wednesday, May 29, 2013

North Korea to safeguard 'priceless' nuclear weapons

North Korea vowed on Wednesday to tighten its hold on its "priceless" nuclear deterrent, confounding reports that it might be willing to resume multilateral talks on denuclearisation.

North Korea vowed on Wednesday to tighten its hold on its
North Korean leader Kim Jong-un and (right) and the Sohae launching station in Tongchang-ri  Photo: AFP/Getty Images
A lengthy front-page editorial in the North's ruling party daily Rodong Sinmun said a strong nuclear deterrent was the only guarantee of a "final victory" against the forces of imperialism.
"We will tighten our grip on this priceless nuclear treasure sword and carry out battles against imperialists with greater vigour," it said.
The editorial appeared days after Chinese state media said North Korean leader Kim Jong-un had informed Chinese president Xi Jinping that Pyongyang would consider resuming six-party denuclearisation talks.
The Xinhua news agency said the message was sent in a letter that was hand delivered to Xi by Kim's personal envoy during a visit to Beijing last week.
North Korean state media had confirmed delivery of the letter but made no mention whatsoever of a dialogue proposal.