Thursday, April 18, 2013

Mazishi ya Bi Kidude yafanyika Zanzibar

 18 Aprili, 2013 - Saa 14:08 GMT

Inasemekana Bi Kidude alikuwa na zaidi ya umri wa miaka mia moja
Viongozi wa Tanzania na Zanzibar walikuwa miongoni mwa waombolezaji waliohudhuria mazishi ya mwanamuziki mkongwe wa Kisiwani Zanzibar Fatma binti Baraka, aliyesifika kama Bi Kidude.
Mwandishi wa BBC Tulanana Bohela anasema kuwa watu wengi, walikuwa na majonzi kwani wengi walimuona kama bibi au nyanyao
Wengi walitaka kujionea ili kuthibitisha habari za kifo chake.
Inaaminika alikuwa na zaidi ya miamoja na alikuwa mtumbuizaji wa nyimbo za Taarabu
Aliendelea kutumbuiza wengi licha ya umri wake.
Mnamo mwaka 2005, alituzwa kwa mchango wake katika fani ya muziki wakati wa mkusanyiko mkubwa wa wanamuziki duniani
Mamia ya wanawake waliomboleza nyumbani kwake kabla ya mwili wake kupelekwa kwa maombi kisha mazishi.
Alizikiwa kijijini kwao Kitumba, ambako rais Jakaya Kikwete alitoa heshima zake za mwisho.
Duru zinasema Bi Kidude alitumbuiza wengi na watu walimpenda kwa miondoko yake.
Inaarifiwa Bi Kidude alianza kuimba taarabu mwaka wa 1920
Siku rasmi ya kuzaliwa kwa Bi Kidude haijulikani lakini kuna tetesi liwa alizaliwa mwaka 1910.

No comments:

Post a Comment