18 Aprili, 2013 - Saa 07:05 GMT
Zaidi ya watu 100 wamejeruhiwa
katika mulipuko uliotokea kwenye kiwanda cha mbolea kilichoko Kaskazini
Magharibi mwa eneo la Waco, jimbo la Texas. Wengi wamekwama ndani ya
majengo yanayendelea kuteketea kufuatia mulipuko huo.
Meya wa Mji kulitokea mulipuko huo, Tummy Muska
ameelezea kutokea moto mkubwa uliolipuka sawa na bomu. Mulipuko huo
umeharibu majengo ya kiwanda hicho, makaazi ya karibu kikiwemo kituo
kimoja cha afya.Majengo kadhaa yameendelea kuteketea karibu na kiwanda hicho cha mbolea.Taarifa ambazo hazijathibitishwa zinasema zinasea kuna watu waliopoteza maisha.
Amesema kufikia sasa hawezi kuthibitisha vifo vyovyote. Watu 38 wameripotiwa kua katika hali mahututi. Makundi ya wokozi yameanza kufika nyumba hadi nyingine kuwaokoa majeruhi na kutoa huduma ya kwanza.
Kituo cha Dharura kimewekwa kwenye uwanja wa mpira ulioko karibu.Gavana wa Texas amesema afisi yake imetoa raslimali zake kusaidia katika juhudi za wokozi.
No comments:
Post a Comment