Saturday, May 25, 2013

Viongozi wa AU wasowera tamashani

 25 Mei, 2013 


Mkutano maalumu wa kilele kuadhimisha miaka 50 ya Umoja wa Afrika (OAU/AU) ulianza Jumamosi asubuhi mjini Addis Ababa.
Mkutano wa kilele wa AU
OAU ilipoanza mwaka wa 1963 ilikuwa na nchi zanachama 33.
Sasa ni jumuia ya nchi 54.
Nembo ya mkutano ni muibuko wa Afrika na mwenyekiti wa mkutano, Waziri Mkuu wa Ethiopia, Hailemariam Desalegn, alisema umoja wa Afrika na chipuko jipya ndio utaamua ajenda ya Afrika katika miaka 50 ijayo.
Sherehe zitaendelea Jumamosi jioni katika ukumbi wa Addis Ababa's Millennium Hall ambapo waziri mkuu wa Ethiopia anaandaa halfa ya usiku huku sherehe zikiendelea kwa muziku na dansa.
Papa Wemba, Salif Keita wa Mali na kikundi cha reggae cha Uingereza, Steel Pulse, wanatarajiwa kutumbuiza wageni.
Tamasha hilo litaonekana kwenye televisheni kubwa zilizosambazwa mjini Addis Ababa.

No comments:

Post a Comment