Tuesday, April 30, 2013

Barua ya wazi kwa kiongozi wa al-Shabaab yaonyesha: 'Ndiyo, kuna matatizo'

Barua iliyo na ukali iliyotumwa kwa kiongozi wa al-Shabaab Ahmed Abdi Godane kutoka kwenye moja ya kikundi cha wapiganaji wa nje wa ngazi ya juu imeonyesha kuongezeka kwa kutoaminiana na kukatika kwa mawasiliano kati ya vikundi mbalimbali vilivyojitenga ndani ya kikundi hicho chenye ushirika na al-Qaeda.
  • Askari wa Jeshi la Taifa la Somalia wakiwalinda washukiwa wawili wanachama wa al-Shabaab waliokamatwa tarehe 3 Oktoba, 2012, siku moja baada ya vikosi vya Somalia na Umoja wa Afrika kuingia kwenye iliyokuwa ngome ya kikundi cha wanamgambo hao bandari ya Kismayu. [Stuart Price/AFP]. Askari wa Jeshi la Taifa la Somalia wakiwalinda washukiwa wawili wanachama wa al-Shabaab waliokamatwa tarehe 3 Oktoba, 2012, siku moja baada ya vikosi vya Somalia na Umoja wa Afrika kuingia kwenye iliyokuwa ngome ya kikundi cha wanamgambo hao bandari ya Kismayu. [Stuart Price/AFP].
Mambo machache yanajulikana kuhusu mwandishi -- al-Zubayr al-Muhajir -- lakini kutokana na barua hiyo ni ushahidi kwamba ni ofisa mwenye cheo cha juu katika al-Shabaab mwenye uhusiano wa karibu na muhajireen (wapiganaji wa kutoka nje).
Katika barua hiyo, al-Muhajir alielezea namna Godane, ambaye pia anajulikana kama Mukhtar Abu al-Zubayr, alimteua kuwa mwanachama wa baraza la Shura la al-Shabaab na kuwa mwenyekiti wa mahakama maalumu ya sharia ambayo iliwasuluhisha Godane na viongozi wengine watatu wa ngazi ya juu wa harakati -- Ibrahim al-Afghani (ambaye jina lake halisi ni Ibrahim Haji Jama Meeaad na pia anajulikana kama Abu Bakr al-Zaylai), Sheikh Mukhtar Robow Ali (au Abu Mansur) na Fuad Mohamed Khalaf.
Katika barua hiyo ya kurasa 12 ya al-Muhajir ambayo ilitumwa kwenye tovuti mbalimbali za jihadi tarehe 20 Aprili na yenye kichwa cha habari "Ndiyo, kuna matatizo", alisema madhumuni yake katika kuandika barua hiyo ilikuwa ni "kujitoa mbele za Mungu na kwa taifa kwa uchokozi na ukiukaji wa sheria unaofanywa na baadhi yetu […na ] kuwaonya wapenzi wote wa jihad miongoni mwa muhajireen ndani na nje ya nchi kwamba hali haiko kama inavyoonyeshwa na harakati".

Kukatika kwa mawasiliano ndani ya al-Shabaab

Al-Muhajir alielezea kwamba aliamua kutuma barua ya wazi kwenye intaneti kwa sababu njia nyingine za mawasiliano zilishindwa.
Miezi kadhaa iliyopita alisema alituma ujumbe mrefu kwa Godane kupitia kwa wanachama wa Baraza la Shura "kuweka bayana baadhi ya masuala yanayohusiana na kukamatwa kwa baadhi ya ndugu wa mujahedeen pamoja na mashitaka yasiyokuwa bayana wakati familia zao hawajui chochote kuhusu hali zao au hata sehemu walikofungwa."
Baada ya kutopata majibu, al-Muhajir alisema alikwenda msikitini ambapo maofisa wa al-Shabaab walikuwa wazungumze na "mujahedeen na Waislamu na kuwaonya juu ya matokeo mabaya ya dhambi na ubaya wetu, wakiogopa kwamba, pamoja na mashambulio mengine, ingekuwa sababu ya kushindwa kwao", lakini nilisimamishwa kabla ya kumaliza na kupigwa marufuku msikitini.
Kwa mujibu wa barua hiyo, al-Muhajir alijaribu kupanga mikutano ya ana kwa ana na Godane, lakini ilikataliwa, na mwishoni alijaribu kukutana na ofisa aliyeteuliwa na Godane kuwawakilisha muhajireen, bado ilikataliwa pia.
"Sikuwa na chaguo lingine lolote," aliandika akirejelea Godane, "isipokuwa kubaki kimya wakati nikiangalia hali mbaya ya mujahedeen na waislamu. Hili halikubaliki katika sharia."

Shinikizo lawasikitisha wapiganaji wa kigeni

Al-Muhajir aliendelea kuorodhesha msururu wa matatizo yanayowakabili muhajireen huko Somalia, ikiwa ni pamoja na:
  • "Msemaji wa jeshi alisema kwamba muhajirina yeyote ambaye anaondoka Somalia bila ya ruhusa kutoka [Godane] anachukuliwa kama muasi."
  • "Wewe [Godane] haujaonana kwa miaka mingi, hata mara moja, na muhajirina wote kuzungumza nao na kuangalia mazingira yao moja kwa moja bila ya kuingiliwa kati."
  • "Wewe [Godane] unawakamata baadhi ya muhajirina bila ya kuwashitaki na hamziambii familia au ndugu zao kuhusu mahali waliko au masharti. Mnapiga marufuku wasitembelewe na mtu yeyote na kukataa kuwasomea mashitaka mbele ya mahakama za umma."
  • "Wewe [Godane] ulifanya uamuzi wa siri wa kutowapokea muhajireen wanaotoka nchi za nje, iwe mmoja mmoja au familia, lakini haukutangaza uamuzi huu … na wangeweza kusafiri na kupata matatizo ya uhamiaji, na kuishia tu ama kutoshiriki katika jihadi au katika magereza ya makafiri."
  • "Uliwakamata baadhi ya muhajireen, ukiwatuhumu kwa kufuata waasi wa dini. Licha ya uamuzi wa mahakama ya siri ambao ulithibitisha kutokuwa na hatia kwao, bado unachukulia kama wahalifu. Umewafukuza baadhi yao katika ardhi za makafiri wakati unawatafuta wengine."
Al-Muhajir aliwatuhumu hata viongozi wa usalama wa al-Shabaab kwa kuwabaka wake za muhajireen ambao waliondoka kwenda kwenye mapigano. Alielezea kwamba katika tukio moja, kiongozi wa muhajir aliwasilisha madai ya ubakaji dhidi ya mwanachama wa al-Shabaab kwa mmoja wa viongozi wa Godane ambaye "alisisitiza kwamba akubali kushindwa kesi na kufuta malalamiko. Ndugu aligundua kwamba hicho ni kikwazo cha hukumu za Mungu, hivyo aliondoka nchini kutokana na hofu."
"Baadhi ya wageni wamekuwa wakiteswa hadi kufa katika magereza yenu ya siri na hamkuwashitaki wanachama wenu wa usalama ambao walifanya makosa hayo," al-Muhajir aliendelea kusema.
Al-Muhajir alikamilisha barua yake kwa kusema, "Hii ni hali halisi ya wageni, ewe Emir, na kama hujui hali hii, basi ni balaa, na kama unalijua hili, basi ni janga kubwa."
"Msiwakandamize watu hata kama mnaweza, kwa sababu muda mwingi, kutotenda haki kunasababisha majuto. Utalala wakati anayenyanyaswa akiwa macho akimuomba Mungu amlipie kisasi. Mungu hawatelekezi wanaonyanyaswa."

No comments:

Post a Comment