Saturday, April 20, 2013

Marathon ya Madrid itakuwa kubwa

 20 Aprili, 2013 - Saa 12:38 GMT

Watu wengi zaidi wamejiandikisha kushiriki kwenye marathon ya Madrid, Uspania, ya Jumapili ya mwisho wa Aprili baada ya shambulio la bomu kwenye marathon ya Boston siku ya Jumatatu.
Bendera ikipeoea nusu mlingoti  bunge la Marekani siku ya bomu la Boston marathon
Waandalizi wa mbio hizo wanasema watu waliojiandikisha ilizidi mara nne baada ya shambulio la Boston.
Mkuu wa kamati ya Olimpiki ya Uspania ambayo inajitayarisha kuomba kuandaa Olimpiki ya mwaka wa 2020, alisema wanaoshiriki kwenye marathon wakiongezeka ndio sifa kubwa ambayo watu wa Madrid wanaweza kuupa mji wa Boston.

No comments:

Post a Comment