Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud alizindua siku ya Jumatano
(tarehe 17 Aprili) mpango wa matumizi ya mkaa unaosaidiwa na mashirika
matatu ya Umoja wa Mataifa.
Robo milioni ya tani za mkaa husafirishwa kwenda nchi za Ghuba kila
mwaka, kwa mujibu wa ofisi ya UN Somalia. Ili kuzalisha kiasi hicho,
idadi ya miti milioni 4.4 hukatwa katika ardhi iliyosafishwa ya hekta
72,900, na kuzidisha uwezekano wa uharibifu kutokana na ukame na
mafuriko.
Mohamud aliahidi wajibu wa serikali yake ya kusimamisha kabisa usafirishaji nje wa mkaa.
"Kuna sheria katika nchi hii ambazo zilipitishwa miaka ya 1970 na
serikali ya Somalia. Pia kumekuwepo na maazimio ya UN kuhusu upigwaji
marufuku mkaa," Mohamud alisema katika taarifa fupi ya kuadhimisha Siku
ya Miti. "Licha ya hali ya sasa, lazima tuziimarishe sheria hizi."
Shirika la Chakula na Kilimo, Mpango wa UN wa Mazingira na Mpango wa
Maendeleo wa UN yanasaidia juhudi za serikali ya Somalia za kuwezesha
ushirikiano wa kikanda, kutengeneza vyombo vya udhibiti na taratibu za
utekelezaji, kuanzisha vyanzo mbadala vya nishati na kuwasaidia
wafaidikaji wa biashara ya mkaa kutafuta njia mbadala za kujipatia
riziki.
Uzalishaji mkaa unaharakisha mchakato wa kuenea kwa jangwa, kupungua
kwa ardhi ya kilimo au malisho ya wanyama na kuwasukuma wakaazi kutoka
maeneo yao kwa vile haikaliki. Al-Shabaab pia wamekuwa wakitegemea usafirishaji haramu wa mkaa ili kugharamia shughuli zao za kigaidi.
"Nataka niseme hivi, usafirishaji mkee nje ni kosa la jinai,
" Mohamud alisema. "Ardhi yetu na urithi wa kilimo vinategemea miti
yetu. Lazima tuyalinde mazingira yetu kuimarisha sheria za ndani za
kimataifa."
Rais wa Somalia alipanda mti katika ikulu ya rais ya Villa Somalia na
kuwahamasisha wananchi kupanda miti katika vitalu vyao na ardhi yao
pia.
No comments:
Post a Comment