Imeelezwa kuwa ziara ya Rais wa China nchini Tanzania imeleta mafanikio mengi kwa Zanzibar ikiwa ni pamoja na Makampuni ya Kichina kupanga kuwekeza katika sekta tofauti Zanzibar.
Balozi Mdogo wa China anayefanya
kazi Zanzibar Bi Chen Qiman ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na
Waandishi wa Habari Ofisini kwake Mazizini kuhusiana na matokeo ya ziara
ya Rais Jinping aliyofanya karibuni nchini Tanzania.
Amesema Zanzibar imeweza
kunufaika moja kwa moja na zira hiyo ikiwa ni pamoja na kusainiwa Miradi
mitatu ya maendeleo kwa ajili ya Visiwa vya Unguja na Pemba.
Bi Chen amesema Rais wa China pia
amemualika Rais Shein kwenda China kwa ziara ya kikazi ambapo pia
atapata fursa zaidi ya kupanga mambo mengi ya kimaendeleo nchini huko.
Ameongeza kuwa Ziara hiyo
inayotarajiwa kufanyika mwaka huu itakuwa fursa adhimu kwa Rais Shein
kujifunza mengi na kukuza mahusiano zaidi kati ya Zanzibar na Jamhuri ya
China.
Akizungumzia mikakati iliyowekwa
na China ya kuisadia Zanzibar Bi Chen amesema Ofisi yake itaendelea
kuitangaza Zanzibar katika nchi yake ili kuwavutia Wananchi wa China
kuja kutembelea Zanzibar na kuimarisha Sekta ya Utalii.
katika kufanikisha hilo Bi Chen
ameshauri Wazanzibari kuijifunza Lugha ya Kichina ili kurahisisha
mawasiliano iwapo Wageni hao watakuja kutalii nchini hapa.
Mikakati mingine waliyoipanga ni
pamoja na kuyahamasisha Makampuni kufanya uwekezaji katika Viwanda vya
kusindika Matunda na kuwekeza katika Bahari jambo ambalo litasaidia sana
maendeleo na kupunguza ukosefu wa Ajira.
Ziara ya Rais Jinping nchini
Tanzania aliyoifanya karibuni imezidi kuimarisha mahusiano mema kati ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya China ambapo katika ziara
hiyo jumla ya Miradi 17 ya kimaendeleo iltiwa saini.
No comments:
Post a Comment