Saturday, May 18, 2013

Marekani ina wasiwasi kuhusu Nigeria

 18 Mei, 2013

Wakati wanajeshi wa Nigeria wanaendelea na operesheni yao dhidi ya wapiganaji wa Kiislamu kaskazini mashariki mwa nchi, Marekani imesema ina wasiswasi sana kuhusu raia katika eneo hilo.
Wanajeshi wa Nigeria wakiingia kwenye kijiji kuwasaka Boko Haram
Katika taarifa ya Waziri wa Mashauri ya Nchi za Nje wa Marekani, John Kerry, amesema ana wasiwasi kuhusu madai ya kuaminika kuwa wanajeshi wa Nigeria wamekiuka vibaya haki za binadamu.
Bwana Kerry alisema hayo yatazidisha ghasia na kuchochea msimamo mkali.
Nigeria inafanya mashambulio dhidi ya kundi la wapiganaji wa Kiislamu, Boko Haram, katika majimbo matatu ya kaskazini-mashariki.

No comments:

Post a Comment