Monday, May 13, 2013

Waondoka katika makao ya wizara Libya

 13 Mei, 2013 

Watu waliokuwa wamejihami na ambao wanataka washirika katika utawala wa aliyekuwa rais Muamar Gaddafi, kufurushwa kutoka serikalini, hatimaye wameondoka katika makao ya wizara mbili za serikali mjini Tripoli.
Waziri wa sheria Salah al-Marghani alithibitishia BBC kuwa watu hao waliweza kuondoka kutoka ofisi za wizara hizo, ile ya mambo ya nje na na ile ya sheria.
Watu hao walizingira majengo hayo wiki mbili zilizopita wakiwa wamejihami kwa zana nzito za kivita.
Bunge ilipitisha sheria mpya wiki jana inayozuia waliokuwa washirika wa Gaddafi kutoshikilia nyadhifa zozote za kisiasa.
Takriban watu 1,000 waliandamana nje ya makao ya wizara ya mambo ya nje mnamo siku ya Ijumaa lakini baadhi walishambuliwa na kuchapwa , huku mabango yao yakiraruliwa na watu hao waliokuwa wamejhihami.

Ombi la Waziri

Bwana Marghani alisema kuwa wizara yake sasa iko chini ya polisi wa idara za mahakama na kuwa wafanyakazi walirejea kazini siku ya Jumamosi kwa masaa machache.
''Tunatumai kuwa hili halitatokea tena na kuwa ni funzo kwetu kuwa hatupaswi kuingilia shughuli za taasisi za kitaifa,'' alisema waziri huyo.
Alisema kuwa mwafaka umefikiwa kuwa wizara ya mambo ya nje itaweza kukabidhiwa kwa maafisa wakuu ifikapo Jumapili.
Nia ya watu hao ilikuwa kutaka serikali kuwatenga waliokuwa washirika wa Gaddafi na kutowapa nyadhifa kuu serikalini.
Tangu kutokea kifo cha Gaddafi, mji wa Tripoli pamoja na miji mingine, imekumbwa na ghasia pamoja na makabiliano.
Serikali imekuwa ikijaribu kuvunja magenge ya wahalifu ambayo yaliundwa wakati wa vita vilivyoiangusha serikali ya Muamar Gaddafi.
Mswaada uliopitishwa na bunge ulikosolewa kwa kutokuwa ingawa imekubalika kuwa sheria na huenda ikaathiri mamafisa kadaa wa serikali wanaohudumu kwa sasa.

No comments:

Post a Comment