Tuesday, November 13, 2012

HADITHI ZA MTUME (SAW) 20-24

Hadithi Ya 20: Ikiwa Huna Haya Basi Fanya Utakavyo



الحديث العشرون
“إذا لم تستح فاصنع ما شئت”

عن أبي مَسْعُودٍ عُقْبَةَ بن عمرو الأَنْصَارِيّ البَدْرِيّ رضي اللهُ عنه قال : قالَ رسُولُ الله صلى الله عليه وسلم: ((إِنَّ مما أَدْرَكَ النَّاسُ مِنْ كَلامِ النُّبُوَّةِ الأولَى: إِذا لمْ تَسْتَحِ فاصْنَعْ ما شِئْتَ)).
رَوَاهُ الْبُخَارِيُّ
HADITHI YA 20
IKIWA HUNA HAYA BASI FANYA UTAKAVYO
Kutoka kwa Abu Mas’ud ‘Uqbah Ibn ‘Amr Al Ansariy Al Badriy رضي الله عنه  ambaye amesema kuwa  Mtume صلى الله عليه وسلم  kasema: “Katika maneno ambayo watu waliyapata kutoka kwa Mitume wa mwanzo (waliotangulia) ni haya: “Ikiwa huna haya basi fanya utakalo.”
Imesimuliwa na Al-Bukhari
——————————————————————————-


Hadithi Ya 21: Sema Namuamini Allah Kisha Kuwa Mwenye Msimamo



الحديث الحادي والعشرون
“قل آمنت بالله ثم استقم”
عن أبي عَمْرو، وَقِيلَ: أبي عَمْرَةَ، سُفْيَانَ بْنِ عَبْدِ اللهِ  رَضيَ اللهُ عَنْهُ قَال: قُلْتُ: يا رَسُولَ الله، قُلْ لي في الإِسْلاَمِ قَوْلاً، لاَ أَسْأَلُ عَنْهُ أَحَداً غَيْرَكَ. قَال: ((قُلْ: آمَنْتُ باللهِ ثُمَّ اسْتَقِمْ)).
رَوَاهُ مُسْلِمٌ
HADITHI  YA 21
SEMA NAMUAMINI ALLAH KISHA KUWA MWENYE MSIMAMO
Kutoka kwa Abu ‘Amr, vile vile (anajulikana kama)  Abu ‘Amra Sufyaan Ibn Abdillah رضي الله عنه   ambaye amesema:
Nilisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyeezi Mungu, niambie kitu kuhusu Uislamu ambacho siwezi kumuuliza mtu yeyote ila wewe.  Akasema (Mtume صلى الله عليه وسلم )  : Sema;  Namuamini Allaah , kisha kuwa mwenye kunyooka. (kwa kuendelea kufanya ibada na kuwa na msimamo madhubuti katika dini)
Imesimuliwa na Muslim.
————————————————————————————-

Hadithi Ya 22: Je, Nikiswali Swalah Za Fardhi, Nikafunga Ramadhaan…



الحديث الثاني والعشرون
“أرأيت إذا صليت المكتوبات وصمت رمضان”
عَنْ أبي عَبْدِ اللهِ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اللهِ الأنْصَارِيِّ رَضي اللهُ عَنْهُما أَنَّ رَجُلاً سَأَلَ رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم فَقال: أَرَأَيْتَ إذَا صَلَّيْتُ  الْمكْتُوباتِ، وَصُمْتُ رَمَضانَ، وَأَحْلَلْتُ الْحَلاَلَ، وَحَرَّمْتُ الْحَرَامَ، وَلَمْ أَزِدْ على ذِلكَ شَيْئاً، أَأَدْخُلُ الْجَنَّةَ ؟ قال: ((نَعَمْ))
رَوَاهُ مُسْلِمٌ
HADITHI YA  22

JE, NIKISWALI SWALAH ZA FARDHI, NIKAFUNGA RAMADHAAN…
Inatoka kwa Abu ‘Abdillaah Jaabir bin ‘Abdillaah Al-Answaariy رضي الله عنه  alisema:
Mtu alimuuliza Mtume ,صلى الله عليه  وسلم  Unafikiri nikiswali Swalah za fardhi, nikafunga Ramadhaan, nikafanya halali kilicho halali na nikaharimisha kile kilichoharimishwa, na nisifanye  jambo lolote lingine, je? Nitaingia peponi? Mtume صلى الله عليه  وسلم  akamjibu: Ndio.
Imesimuliwa na Muslim
———————————————————————————

Hadithi Ya 23: Tohara Ni Nusu Ya Imaan



الحديث الثالث والعشرون
“االطهور شطر الإيمان”
عن أبي مالكٍ الحارِثِ بنِ عاصِمٍ الأَشْعَرِيِّ رضي اللهُ عنهُ قال : قال رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم: ((الطُّهُورُ شَطْرُ الإِيَمانِ، والحمدُ لِلهِ تَمْلأُ الْمِيزَانَ، وسُبْحانَ اللهِ والحمدُ لِلهِ تَمْلآنِ – أو تَمْلأُ – ما بَيْنَ السَّمآءِ والأرضِ، والصَّلاةُ نورٌ، والصَّدَقَةُ بُرْهانٌ، والصَّبْرُ ضِيَاءٌ، والْقُرآنُ حُجَّةٌ لَكَ أو عَلَيْكَ، كُلُّ النَّاسِ يَغْدو، فَبائعٌ نَفْسَهُ، فَمُعْتِقُها أَو مُوبِقُها))
رَوَاهُ مُسْلِمٌ
HADITHI YA  23
TOHARA NI NUSU YA IMAAN
Kutoka kwa Abu Malik Al-Harith Ibn ‘Asim Al-Ash’ariyy رضي الله عنه  alisema, kasema Mtume wa Allahصلى الله عليه  وسلم
Tohara ni nusu ya Imaan. Na AlhamduliLlahi inajaza mizani, na SubhaanaAllah Wal-hamduliLlah inajaza baina ya mbingu na ardhi.  Swala ni nuru, Sadaka ni ushuhuda, Subira ni mwangaza, na Qur’aan ni hoja yako au dhidi yako.   Kila mtu anaianza siku yake akiichuuza nafsi yake, aidha huiacha huru au anaisambaratisha.
Imesimuliwa na Muslim
————————————————————————————-

Hadithi Ya 24: Enyi Waja Wangu Nimeikataza Nafsi Yangu Dhulma




الحديث الرابع والعشرون
“يا عبادي إني حرمت الظلم على نفسي”
عن أبي ذَرٍّ الْغِفاريِّ رضي الله عنه، عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم فيما يَرْويهِ عن رَبِّهِ عَزَّ وجَلَّ أَنَّهُ قال:
(( يا عِبادي إنِّي حَرَّمْتُ الظُلْمَ على نَفْسِي وَ جعَلْتُهُ بَيْنَكُمْ مُحَرَّماً فلا تَظَالَمُوا.
يا عِبادي كُلُّكُمْ ضالٌّ إلا مَنْ هَدَيْتُهُ، فاسْتَهدُوني أهْدِكُمْ.
يا عِبادِي كُلُّكُمْ جائعٌ إلا مَنْ أطْعَمْتُهُ، فاسْتَطْعِمُوني أُطْعِمْكُم.
يا عِبادِي كُلُّكُمْ عَارٍ إلا مَنْ كَسَوْتُهُ، فاسْتكْسوني أَكسُكُم.
يا عِبادِي إِنَّكُمْ تُخْطِئُونَ بالليْلِ والنَّهارِ، وأنا أَغْفِرُ الذُّنُوبَ جَميعاً، فاسْتَغْفِرُوني أُغْفِر لكُمْ.
يا عِبادِي إِنَّكُمْ لنْ تبْلغُوا ضُرِّي فتَضُرُّوني، ولن تبْلُغُوا نفْعي فَتَنْفعُوني.
يا عِبادِي لوْ أَنَّ أَوَّلَكُمْ وآخِرَكُمْ وإنْسَكُمْ وجِنَّكُمْ كانُوا عَلَى أَتْقَى قَلْبِ رَجُلٍ واحدٍ مِنْكُمْ ما زادَ ذلك في مُلْكي شَيئاً.
يا عِبادِي لوْ أَنَّ أَوَّلكُمْ وآخِرَكُمْ وإنْسَكُمْ وجِنَّكُمْ كانُوا عَلَى أَفْجَرِ قَلْبِ رَجُلٍ وَاحدٍ مِنْكُمْ ما نَقَصَ ذَلِكَ مِنْ مُلْكي شَيئاً.
يا عِبادِي لوْ أَنَّ أَوَّلَكُمْ وآخِرَكُمْ وإنْسَكُمْ وجنَّكُمْ قاموا في صَعِيدٍ وَاحِدٍ، فَسَأَلُوني، فأَعْطَيْتُ كلَّ واحدٍ مَسْأَلَتَهُ ما نَقَصَ ذلك مِمَّا عِنْدِي إلا كما يَنْقُصُ الْمِخْيَطُ إذا أُدْخِلَ الْبَحْرَ.
يا عِبادِي إنَّما هي أعمَالُكُمْ أُحْصِيها لَكُمْ ثُمَّ أُوَفِّيكُمْ إيَّاها، فَمَنْ وَجَدَ خيْراً فَلْيَحْمَدِ اللهَ، ومَنْ وَجَدَ غَيْرَ ذلك فَلا يَلومَنَّ إلا نَفْسَه))
رَوَاهُ مُسْلِمٌ
HADITHI YA 24
ENYI WAJA WANGU NIMEIKATAZA NAFSI YANGU DHULMA

Kutoka kwa Abu Dharr Al-Ghifariy رضي الله عنه   naye kutoka kwa Mtume صلى الله عليه وسلم  akisimulia yale aliyopokea kutoka kwa  Bwana wake   عَزَّ وَجَلَّ   ni:
Enyi waja Wangu, Nimeikataza nafsi Yangu dhulma na Nimeiharamisha kwenu (hiyo dhulma), kwa hivyo msidhulumiane.
Enyi waja Wangu, nyote mumepotea isipokuwa wale Niliowaongoza, kwa hivyo tafuteni muongozo kutoka Kwangu Nitakuongozeni.
Enyi waja Wangu nyote mna njaa isipokuwa wale Niliowalisha, kwa hivyo tafuteni chakula kutoka Kwangu na Nitakulisheni.
Enyi waja Wangu, nyote muko uchi isipokuwa wale niliowavika nguo, kwa hivyo tafuteni vazi kutoka Kwangu nitakuvisheni.
Enyi waja Wangu, mnafanya  makosa usiku na mchana, na ninasamehe dhambi zote, kwa hivyo tafuteni msamaha kutoka Kwangu nitakusameheni.
Enyi waja Wangu hamuwezi kunidhuru Mimi wala kuninufaisha.
Enyi waja Wangu, ingekuwa wa mwanzo wenu na wa mwisho wenu, binaadamu katika nyinyi na majini katika nyinyi akawa mcha Mungu kama moyo wa mcha Mungu yeyote katika nyinyi, haitaongeza  chochote katika ufalme Wangu.
Enyi waja Wangu, angelikuwa wa mwanzo wenu na wa mwisho wenu, binaadamu katika nyinyi na majini katika nyinyi akawa mbaya kama moyo mbaya wa mtu miongoni mwenu (mtu mbaya kupita kiasi) haitonipunguzia chochote katika ufalme Wangu.
Enyi  waja Wangu ingelikuwa wa mwanzo wenu na wa mwisho wenu, binaadamu katika nyinyi na majini katika nyinyi mukasimama pahala pamoja na mkaniomba, na nikawapa kila mmoja alichoomba, haitonipunguzia katika nilicho nacho zaidi kuliko sindano inavyopunguza bahari inapochovya.
Enyi waja Wangu, ni vitendo vyenu ninavyovihesabu, kwa ajili yenu nikakulipeni.  Kwa hivyo anayekuta wema amshukuru Allaah na yule anayekuta yasiokuwa mema (basi) ajilaumu mwenyewe.
Imesimuliwa na Muslim

No comments:

Post a Comment