Siasa
"WANAWAKE WANAOPENDA KUTEMBEA UCHI
WAENDE IRINGA KWA MBUNGE WAO AMBAYE NI MCHUNGA
NGURUWE".....KAULI YA MBUNGE JANA
Akichangia Bungeni jana jumatatu-15/04/2013 jioni,Mbunge wa Iringa
mjini,Mchungaji Msigwa,amewalaumu viongozi wa serikali ya CCM kwa
kupuuzia mambo nyeti kama matatizo ya udini Zanzibar.
Msigwa alimlaumu vikali
waziri Mkuu kwa kutoa jibu jepesi kwa swali alilouliza juu ya udini
Zanzibar.Alisisitiza kwamba,kuwa na cheo kikubwa serikalini au kusoma
hakumfanyi mtu mpumbavu awe mwelevu.
Akinukuu vifunguu kadhaa vya
Biblia,Msigwa amesisitiza kuwa,"hata ukiutwanga upumbavu na mbegu kwenye
kinu,upumbavu utabakia upumbavu".
Amedai kitendo cha viongozi wenye
akili ndogo kuongoza watu wenye akili kuwazidi ndiko kulikopelekea
mauaji ya kidini Zanzibar na migogoro mingine ya kidini ikiwepo tukio la
mtu mmoja kukamatwa na bunduki ya kivita yenye risasi ndani ya kanisa
la Anglikani jana.
Hoja hiyo iliamsha hasira za wabunge wa Zanzibar ambao licha ya
kumtukana na kumwita Msigwa kuwa ni mchungaji wa nguruwe,walisisitiza
kuwa serikali ya Zanzibar inaenzi dini ya kiislam na haiwezi kuruhusu uhuru
wa mavazi kwa wanawake.
Huku akishangiliwa kwa nguvu na wabunge wa CCM
na wale wa CUF, Mbunge mmoja toka Zanzibar alisisitiza :"wanawake
wanaopenda kutembea uchi,waende Iringa,sio Zanzibar,Zanzibar inaongozwa
kwa misingi ya dini ya kiislamu".
Baada ya kuruhusiwa na naibu spika,kuwasilisha MWONGOZO WA SPIKA,Msigwa
aliwalaumu wazanzibari kwa kutokukubali ukweli kuwa SERIKALI HAINA
DINI.
"Mnajidanganya,nchi hii haitakuja ongozwa na sheria za kidini,maana
serikali haina dini" alisisitiza Msigwa.
No comments:
Post a Comment