Monday, February 11, 2013

MTOTO WA AJABU MWENYE MACHO MATATU AZALIWA

 
 
 
 
 
 
Rate This

MTOTO wa ajabu amezaliwa kijijini Kidegembye, wilaya ya Njombe, mkoani Njombe, akiwa na macho matatu na kichwa mfano wa uyoga.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mama mzazi  wa mtoto, Martha Kitago (28), alisema  kuwa hadi sasa anamwachia Mungu ambaye ndiye amempa zawadi hiyo.

Alisema kuwa Januari 13 mwaka  huu, alishikwa na uchungu na hivyo akapelekwa katika  kituo cha afya cha Kidegembye kisha akapelekwa Hospitali ya Wilaya ya Njombe Kibena kwa matibabu zaidi.

Baada ya kufanyiwa upasuaji na kupata mtoto  huyo alimpa jina la Zawadi Godfrey japo anadai kuwa aliogopa  sana baada ya  kuonyeshwa  mtoto  mwenyewe.

Martha ambaye ana watoto watatu  sasa akiwemo  Zawadi, alisema  kuwa mtoto  wa kwanza wa kiume ana miaka tisa, wa  pili wa kike ana miaka minne  na kwamba wote alijifungua vizuri bila  kufanyiwa  upasuaji.

Baba  wa  mtoto  huyo, Godfrey Mwingune, alisema  kuwa baada ya  kupata mtoto huyo  wa ajabu aliamua  kurejea nyumbani kwa wazazi wake Igengeza  Ismani  ili  kuwaonyesha japo anatambua ni zawadi  kutoka kwa Mungu.

“Kweli  nilipompeleka kwa  wazazi  kijijini, nao  walibaki  wakishangaa kuona mtoto  wa ajabu hivyo ila sasa tutafanyaje  yote ni mipango ya Mungu,” alisema.

Mwingune  alisema  kuwa hali ya afya ya mtoto  huyo si nzuri kwani mbali ya kuzaliwa akiwa na kilo nne na nusu, bado ana tatizo la uvimbe katika paji lake la uso pia  kichwani kuna kovu kubwa ambalo ni kama ncha mbili hivi ambalo linatoa usaa mwingi.

Alisema kuwa  jeraha hilo alizaliwa nalo na kwamba katika  jicho lake la  kushoto kwa  juu  kuna jicho la pili na kufanya  mtoto huyo kuwa na macho matatu.

Alisema  kuwa  tayari mtoto  huyo amepata  kutibiwa  Hospitali ya  Kibena Njombe na Hospitali ya  Rufaa Mbeya  ila imeshindikana na  madaktari  wamemtaka ampeleke Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu zaidi au nje ya nchi.

Hata  hivyo, mzazi huyo alisema kwa  sasa fedha ya haraka inayohitajika  ni sh milioni 1.5 ili kumwezesha  kwenda  kuanza matibabu Muhimbili japo gharama  za matibabu  zinaweza  kuongezeka.

Aliomba msaada kwani hana uwezo wa kupata kiasai hicho, huku akiwashukuru  wakazi wa Isimani ambao  walimchangia sh 300,000.

No comments:

Post a Comment