IMEWEKWA NA HAMED MAZROUY
Jumla ya Wanafunzi 11,195
wamechaguliwa kujiungia Kidatu cha Tatu kwa mwaka wa masomo 2013 katika
Skuli mbalimbali za Unguja na Pemba ambapo kati yao wasichana ni 6,768
na wavulana ni 4,427.
Aidha Wanafunzi 17,511 wamefaulu kuingia kidato cha kwanza mwaka huu ambapo kati yao Wasichana ni 9,652 na Wavulana 7,859 .
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya
Amali Zanzibar Ali Juma Shamhuna amebainisha hayo leo wakati alipokuwa
akitoa tathimini ya matokeo ya mitihani hiyo huko ofisini kwake Mazizini
nje kidogo ya Mji wa Zanzibar
Amesema kuwa Wanafunzi waliofanya
mtihani wa kuingilia Kidato cha Tatu walikuwa 19,679 ambapo kati yao
Wasichana walikuwa 11,045 na wavulana 8644 sawa na asilimia 93.6 %.
Aidha ameongeza kuwa ufaulu wa kidato cha Tatu umeongezeka kwa asilimia 0.8 ikilinganishwa na mwaka uliopita.
Kwa upande wa Mtihani wa Darasa
la Saba Waziri Shamhuna amesema jumla ya Wanafunzi waliofanya mtihani
huo walikuwa 23,039 kati yao wasichana walikuwa 12,236 na wavulana
10,803.
Akielezea Skuli zilizoshika
nafasi ya juu kwa matokeo ya Darasa la Saba Waziri Shamhuna amesema ni
pamoja na Kizimbani iliyopo Wilaya ya Wete Pemba na Skuli za Wazazi na
Mkunazini zote za Wilaya ya Mjini Unguja.
Aidha amezitaja Skuli zilizofanya vibaya matokeo ya Darasa la Saba kuwa ni Kojani, Ukunjwi na Makoongwe zote za Kisiwani Pemba.
Kwa upande wa Matokeo ya Kidato
cha Pili skuli zilizofanya vyema kuliko nyingine ni Mtoni iliyopo Wilaya
ya Magharibi Unguja na Skuli za Msuka na Kiuyu zote za Wilaya ya
Micheweni Pemba.
Akielezea Skuli zilizofanya
vibaya mtihani wa Kidato cha Pili Waziri Shamhuna amesema ni Skuli za
Mwenge iliyopo Wilaya ya Magharibi na Skuli za Mfuru matonga na
Kinyasini zote za Kaskazini A Unguja.
Waziri Shamhuna amezitaja pia
Skuli ambazo zitalazimika kufungwa kutokana na kupasisha idadi ndogo ya
Wanafunzi ambazo ni Bwefum, Umbuji, Uzi, Ubago,Pongwe Pwani,
Michanvi,Mtende,Kisiwa Panza,Makongwe na Ndagoni.
Ameongeza kuwa jumla ya Kesi za udanganyifu 12 ziliripotiwa kwa
wanafunzi wa Kidato cha pili ambapo Wizara imeamua kwafutia matokeo
wanafunzi waliohusika na Udanganyifu huo
No comments:
Post a Comment