SIRA YA MTUME (SAW)
Sira ni
fani inayojishughulisha kuelezea maisha ya Nabii Muhammad tangu
kuzaliwa mpaka kufa kwake, ikiwa ni pamoja na malezi na makuzi yake,
wasifu wake wa kimaumbile, tabia zake, harakati zake katika
kuufikisha ujumbe wa Uislamu kwa ummah, mahusiano yake na watu na
mataifa mbalimbali. Pia sira inaelezea hali ya ulimwengu kijamii na
kiitikadi kabla na baada ya kuja Nabii Muhammad, kadhalika inataja
maisha na utawala wa Makhalifa waongofu baada ya Mtume.
Fani ya Sira inalenga kumfahamisha Muislamu:-
- Taswira na mfumo mzima wa Uislamu unatolewa na kutafsiriwa na maisha ya Mtume.
- Maisha ya
Nabii Muhammad ndio kigezo na mfano mwema wa kuigwa na kufuatwa ili
kuweza kupata mafanikio Duniani na Akhera. Mwenyezi Mungu
atuambia:-"BILA SHAKA MNAO MFANO MWEMA KWA MTUME WA MWENYEZI
MUNGU…"(33:21)
- Muislamu
apate katika maisha ya Nabii Muhammad kitu kitakachomsaidia kuifahamu
Qur-ani kwani aya nyingi za Qur-ani zinafasiriwa na kuwekwa wazi
na matukio yaliyotokea katika uhai wa Mtume.
- Sira
inaonyesha ni njia na mbinu zipi alizozitumia Mtume mpaka akaweza
kuusimamisha Uislamu katika ulimwengu uliokuwa umefunikwa na
kiza totoro cha ushirikina.
- Sira
inaonyesha ni jinsi gani Mtume alivyoyatatua matatizo na vikwazo
mbalimbali vya ndani na nje alivyokumbana navyo katika
kumfikisha ujumbe wa Allah kwa watu wote.
Hizi ni baadhi tu ya faida zinazopatikana katika kuisoma na kuifuata sira ya Bwana Mtume.
i )BARA ARABU WAKATI WA MTUME NA WAKAZI WAKE
Bara Arabu
lipo upande wa kusini wa Bara la Asia. Bara hili ndilo makazi ya
Waarabu tangu kale na mpaka sasa kinaishi humo kizazi cha Waarabu.
Maelfu ya miaka Waarabu wa kale wliishi maisha yaliyofanana na
maisha yetu ya leo ukiondoa tofauti chache zilizokuwepo. Walikuwepo
miongoni mwao wakazi wa mijini waliostaarabika na kuendelea.
Ama zile
tofauti chache zilizokuwepo kati ya maisha ya Waarabu wale wa kale na
maisha yetu ya leo ni kwa upande wa kidini (kiitikadi) na kijamii.
Waarabu wa kale waliishi katika enzi/zama za viza zilizotawaliwa na
itikadi potofu za kidini na desturi mbaya. Baada ya kudhihiri
Uislamu hali mbaya hizi zilibadilika na Waarabu wakaanza kuishi katika
zama za uchanuzi wa dini ya Kiislamu katika mji wa Makkah kisha
ikaenea katika pande zote za Bara Arabu Uislamu ulizibadilisha hali
na kupigiwa mfano.
Mji wa
Makkah ndio kitovu na chimbuko la kuenea dini ya Kiislamu. Mji huu
upo katika nchi ya Hijazi, nchi ambayo imechukua eneo kubwa la Bara
Arabu. Nchi hii ya Hijazi ilikaliwa na makabila mengi ya Kiarabu,
kabila mashuhuri zaidi lilikuwa ni Qurayshi.
Historia
ya mji wa Makkah na kuanzishwa kwake inaanzia pale alipofika katika mji
huo kwa mara ya kwanza Nabii Ibrahimu – Amani na Rehma za Allah
zimshukie - akitokea nchi ya Palestina akiwa pamoja na mkewe
Haajira na mwanawe Ismail. Wakati huo mji wa Makkah ulikuwa ni
jangwa tupu lililozungukwa na majabali. Nabii Ibrahimu akamuacha
mkewe na mwanawe katika jangwa hilo tupu lisilo na mimea na kurejea
Palestina. Kabla ya kufunga safari ya kurudi Palestina Nabii
Ibrahimu alimuomba Mola wake Mtukufu rehema zake ziyatawale maisha
mapya ya mkewe na mwanawe jangwani hapo na Mola Muumba aliipokea na
kuikubali dua ya Mtume wake kama tunavyosoma ndani ya Qur-ani. Mwenyezi
Mungu akamchimbulia mama Haajira na mwanawe Ismail chemchem ya
Zamzam katika ardhi kame ya jangwani.
Wasafiri
wapitao njia ile walipokiona kisima cha Zamzam walikwenda mahala pale na
kuamua kuishi kandokando ya chemchem ile, hii ni kutokana na shida
sugu ya maji jangwani. Tangu wakati huo kitongoji hicho kikaanza
kustawi mpaka kikawa ndio kitongoji mama cha nchi ya Hijazi. Mtoto
Ismail alipofikia umri wa kuoa alioa katika makabila yale ya Waarabu
waliokuja kukaa pale na kuuanzisha mji wa Makkah. Akajaaliwa kupata
watoto.
Ibrahimu
baba yake Ismail akawa anafanya ziara za mara kwa mara kujulia hali
mkewe, mwanae na wajukuu zake. Katika mojawapo ya ziara zake hizi
ndipo Mwenyezi Mungu alipompelekea wahyi wa kuijenga A-kaaba.
Ibrahimu na mwanawe wakaitekeleza amri ya Mola wao wakaijenga
Al-kaaba. Mwenyezi Mungu akamuamrisha Nabii Ibrahimu awaite watu kuja
kuhiji na kufanya ibada katika nyumba yake hiyo tukufu. Ujenzi huu wa
nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu na ibada tukufu ya Hijjah ndivyo
vilivyoufanya mji wa Makkah kuwa ni mji mtakatifu. Hii ndio historia
fupi ya kuasisiwa mji wa Makkah.
Makabila
mengi yalipatikana kutokana na kizazi cha Ismail mwana wa Nabii
Ibrahimu katika nchi ya Hijazi, kabila la Qurayshi ndilo lililokuwa
mashuhuri zaidi. Baadhi ya makabila haya yalikuwa yakimuabudu
Mwenyezi Mungu kupitia mafundisho ya dini ya Nabii Ibrahim- Amani ya
Allah imshukie. Uongozi wa kidini na kibiashara ulitawaliwa na
Maqurayshi kwa sababu ya ushujaa na ufasaha waliokuwa nao, sifa hizi
ndizo zilizolipelekea kabila la Qurayshi kuyatawala makabila mengine
yote. Mji wa Makkah na Maqurayshi walizidi kupata utukufu pale Mzee
Qusway Bin Kilaab-babu wa nne wa Mtume aliposhika hatamu za uongozi
wa mji wa Makkah. Mzee huyu alikuwa ni mtu mwenye busara, fikra na
hekima. Alianzisha mpango mji, bunge ili watu wote wa Makkah waweze
kukutana humo na kushauriana/kujadili mambo yao, pia aliijenga upya
Al-Kaaba baada ya kuanza kuonyesha athari za kubomoka. Kadhalika
alianzisha utaratibu wa kuwasaidia masikini kwa kuwapa chakula na
maji. Baada ya kupita vizazi vingi, taratibu Maqurayshi walianza
kuyatupa mafundisho ya dini ya Nabii Ibrahimu na kuanza kuyaabudu
masanamu yaliyotengenezwa na mikono yao wenyewe. Ibada ya msanamu
ilikuwa ni matokeo ya safari ya mmoja wa viongozi wa Maqurayshi
alipokewenda Shamu na kuwakuta watu wa huko wakiyaabudia masanamu na
akapendezwa na kuvutiwa na ibada hiyo. Akarejea Makkah na sanamu moja,
akaliweka ndani ya Al-kaaba na kuanza kuliabudia. Watu wa Makkah
kuona hivyo nao wakamuiga kiongozi wao, wakatengeneza masanamu yao
wakayaweka ndani ya Al-kaaba na kuyaabudia na huo ukawa ndio mwanzo
wa kuiacha na kuitupa mila ya Nabii Ibrahimu.
-----------------------------------------------------------------------------------------------
SOMO LA PILI
SOMO LA PILI |
|
i) HALI YA KIDINI KATIKA BARA ARABU KABLA YA UISLAMU
Kabla ya kudhihiri kwa Uislamu Bara arabu halikuwa na dini moja
bali lilisheheni dini nyingi. Baadhi ya wakazi wake walikuwa wakifuata
dini ya Nabii Musa nao ni mayahudi na wengine waliifuata dini ya
Nabii Isa, nao ni Manasara. Mbali na hawa walikuwepo pia waliokuwa
wakiyaabudia masanamu. Qur-ani Tukufu imeyataja baadhi ya masanamu
yaliyofanywa miungu kama vile Laata,Uzzah, Yaghuuth, Yauuqa na Nasrah.
Kadhalika lilikuwepo kundi dogo lililokuwa likifuata dini ya haki
likimuabudu mola wa haki kupitia mafundisho yaliyoletwa na Nabii
Ibrahimu kutoka kwa Mwenyezi mungu.
Mwenyezi Mungu Mtukufu alipompa utume Muhammad na kumpa kazi nzito na
jukumu kubwa la kutangaza dini ya Kiislamu aliinuka na kuanza
kuwalingania watu wamuabudu Mungu mmoja asiye na mshirika na waache
kuyaabudu masanamu waliyoyatengeneza wao wenyewe. Jawabu la
Maquraysh lilikuwa ni kumkadhibisha Mtume na kumpinga vikali sana.
Isitoshe walimuadhibu adhabu kali sana kila aliyemuamini na kumfuata
Mtume ili iwe ni onyo kwa wengine. Hawakukomea hapo tu bali
waliwazuia watu kuonana na kumsikiliza Mtume lakini kwa sababu ya
subira, jihadi, imani yake na msaada wa Mwenyezi Mungu alifanikiwa
kuwashinda maadui wa Uislamu na kuieneza dini ya Mwenyezi Mungu
miongoni mwa Waarabu na watu wa mataifa mengine.
ii) IBADA YA MASANAMU
Kabla ya Uislamu waarabu walizama mno katika ibada ya masanamu
mpaka wakaijaza Al-Kaaba masanamu ambayo idadi yake ilifikia masanamu
mia tatu na sitini (360). Kila kabila lilikuwa na sanamu lake pekee
na kila kaya/familia ilikuwa na sanamu malum kwa ajili ya familia
hiyo tu. Mtu alipotaka kusafiri, alilichukua safarini sanamu moja
ilikufanikiwa safarini na walikuwa wakiyatakasa na kuyatukuza masanamu
haya kiasi cha kuyatolea Qurubaani na dhabihu (sadaka za
kuteketeza). Waarabu walipokuwa wakitaka ushauri katika mambo yao
mfano ndoa, biashara au safari basi uliendea "Hubal" sanamu
lililokuwa ndani ya Al-kaaba wakampa ngamia na dir-ham mia mshika kete
ambazo moja ilikuwa imeandikwa juu yake maneno"Mungu wangu
amenikataza" na ya pili "Mungu wangu ameniamrisha" ya tatu
"Naam/Ndiyo" ya nne "Hapana". Jumla kete zilikuwa ni saba, mshika
kete huzizungusha na kuzichanganya kisha akaitoa moja na
kilichoandikwa juu yake ndio huwa amri iliyotoka kwa Mungu sanamu.
HALI YA KIDINI KATIKA BARA ARABU KABLA YA UISLAMUKabla
ya kudhihiri kwa Uislamu Bara arabu halikuwa na dini moja bali
lilisheheni dini nyingi. Baadhi ya wakazi wake walikuwa wakifuata dini
ya Nabii Musa nao ni mayahudi na wengine waliifuata dini ya Nabii
Isa, nao ni Manasara. Mbali na hawa walikuwepo pia waliokuwa
wakiyaabudia masanamu. Qur-ani Tukufu imeyataja baadhi ya masanamu
yaliyofanywa miungu kama vile Laata,Uzzah, Yaghuuth, Yauuqa na Nasrah.
Kadhalika lilikuwepo kundi dogo lililokuwa likifuata dini ya haki
likimuabudu mola wa haki kupitia mafundisho yaliyoletwa na Nabii
Ibrahimu kutoka kwa Mwenyezi mungu.
Mwenyezi
Mungu Mtukufu alipompa utume Muhammad na kumpa kazi nzito na jukumu
kubwa la kutangaza dini ya Kiislamu aliinuka na kuanza kuwalingania
watu wamuabudu Mungu mmoja asiye na mshirika na waache kuyaabudu
masanamu waliyoyatengeneza wao wenyewe. Jawabu la Maquraysh lilikuwa
ni kumkadhibisha Mtume na kumpinga vikali sana. Isitoshe walimuadhibu
adhabu kali sana kila aliyemuamini na kumfuata Mtume ili iwe ni onyo
kwa wengine. Hawakukomea hapo tu bali waliwazuia watu kuonana na
kumsikiliza Mtume lakini kwa sababu ya subira, jihadi, imani yake na
msaada wa Mwenyezi Mungu alifanikiwa kuwashinda maadui wa Uislamu
na kuieneza dini ya Mwenyezi Mungu miongoni mwa Waarabu na watu wa
mataifa mengine.
Kabla ya
Uislamu waarabu walizama mno katika ibada ya masanamu mpaka
wakaijaza Al-Kaaba masanamu ambayo idadi yake ilifikia masanamu mia tatu
na sitini (360). Kila kabila lilikuwa na sanamu lake pekee na kila
kaya/familia ilikuwa na sanamu malum kwa ajili ya familia hiyo tu.
Mtu alipotaka kusafiri, alilichukua safarini sanamu moja
ilikufanikiwa safarini na walikuwa wakiyatakasa na kuyatukuza masanamu
haya kiasi cha kuyatolea Qurubaani na dhabihu (sadaka za
kuteketeza). Waarabu walipokuwa wakitaka ushauri katika mambo yao
mfano ndoa, biashara au safari basi uliendea "Hubal" sanamu
lililokuwa ndani ya Al-kaaba wakampa ngamia na dir-ham mia mshika kete
ambazo moja ilikuwa imeandikwa juu yake maneno"Mungu wangu
amenikataza" na ya pili "Mungu wangu ameniamrisha" ya tatu
"Naam/Ndiyo" ya nne "Hapana". Jumla kete zilikuwa ni saba, mshika
kete huzizungusha na kuzichanganya kisha akaitoa moja na
kilichoandikwa juu yake ndio huwa amri iliyotoka kwa Mungu sanamu
HALI YA KIJAMII NA TABIA ZA WAARABU |
|
Tumeeleza huko nyuma kwamba
yalipatikana makabila mengi ya kiarabu kutokana na kizazi cha Nabii
Ismail. Kila kabila liliundwa kutokana na kaya/familia kadhaaa
zilizojiunga pamoja. Kila kabila liliongozwa na kiongozi aliyekuwa mtu
mzima anayeheshimika, kukubalika na kutiiwa na wote. Ukabila ulikuwa
ndio sera ya kila kabila, na kila kabila lilikuwa tayari kuilinda
sera yake hiyo ya ukabila dhidi ya uadui wa wote ule kutoka makabila
mengine kwa gharama yoyote ile. Msimamo huu na sera hii ya ukabila
ilisababisha mizozo, ugomvi na mapigano ya mara kwa mara baina ya
makabila haya. Kugombea vyanzo vya maji, machungo na kujifakharisha
kwa nasabu pia vilichochea kwa kiasi kikubwa mizozo na mapigano.
Kama ambavyo watu hutofautiana katika vyeo/hadhi, kazi na hali za
kimaisha, Waarabu pia waligawanyika katika matabaka yafuatayo:-
- Mabwana/Viongozi: hawa ndio waliokuwa na mamlaka juu ya wengine na hatamu za uongozi zilikuwa chini yao.
- Makuhani: hawa walikuwa ndio viongozi wa kidini wakiyatawalia mambo
yote yanayohusu dini ikiwa ni pamoja na ibada, sherehe za kidini
na mengineyo.
- Wafanyabiashara: hawa walijishughulisha na usambaji na uuzaji wa bidhaa mbalimbali ndani na nje ya maeneo yao.
- Wachungaji: hawa ndio waliokuwa wakijishughulisha na uchungaji wa wanyama na kazi ya kilimo kwa kiasi fulani.
Ama kwa upande wa kitabia,Waarabu za jahilia kama walivyo watu wa
zama hizi walikuwa na tabia nzuri na nyingine mbaya. Miongoni mwa
tabia njema walizokuwa nazo ni kama vile ukarimu, murua, ushujaa na
utekelezaji wa ahadi. Tabia mbaya zilizoitawala jamii ile ni pamoja
na ulevi, uchezaji wa kamari, ulaji riba na kuwazika watoto wa kike
wakiwa hai kama ilivyoelezwa na Qur-ani:
"NA MTOTO MWANAMKE ALIYEZIKWA HALI YAKUWA YU HAI ATAKAPOULIZWA. KWA MAKOSA GANI ALIUAWA. (81:8-9)
SOMO LA TATU
i/NASABU YA MTUME KUUMENI KWAKE
Nasabu ya Bwana Mtume – Allah amrehemu na kumshushia amani – kwa upande wa baba yake ni kama ifuatavyo:-
Yeye ni Muhammad Bin Abdillah Bin Abdil – Mutwalib Bin Haashim Bin
Abdi Manaf Bin Qusway Bin Kilaab Bin Murrah Bin Kaab Bin Luayyi Bin
Ghaalib Bin Fihr Bin Maalik Bin Nadhr Bin Kinaanah Bin Khuzaymah Bin
Mudrikata Bin Ilyaas Bin Mudhwar Bin Nizaar Bin Maad Bin Adnaan.
Huu Adnaan ni katika kizazi cha Nabii Ismail Bin Ibrahim – Amani iwe juu
yao.
ii/NASABU YA MTUME KUKENI KWAKE
Nasabu yake Bwana Mtume – Allah amrehemu na kumshushia amani – kwa upande wa mama yake:-
Yeye ni Muhammad Bin Aaminah Bint Wahab Bin Abdi Manaf Bin Zuhrah Bin
Hakiym. Huyu Mzee Hakiym ndiye Kilaab ambaye ni babu wa tano wa
Mtume kwa upande wa baba yake.
Tumekwishaeleza huko nyuma kwamba huyu Mzee Qusway ambaye ni babu wa
nne katika mlolongo wa babu zake Mtume ndiye aliyeweka mpango wa mji
wa Makkah na akawaunganisha pamoja Waarabu kwa kuondosha ukabila.
Baada ya kifo cha Mzee Qusway, hatamu za uongozi wa mji wa Makkah
zilishikwa na babu wa pili wa Mtume Mzee Haashim. Huyu alikuwa
tajiri na ndiye aliyeasisi mfumo wa biashara za Kusi na kaskazi kama
ulivyoelezwa na Qur-ani:-
"ILI KUWAFANYA MAKURESHI WAENDELEE. WAENDELEE NA SAFARI ZAO ZA WAKATI WA
KUSI (kwenda yaman) NA WAKATI WA KASKAZI (kwenda Shamu, ndio maana
tukajaalia jeshi la ndovu kushindwa) (102:1-2)
Pia Mzee huyu ndiye aliyesimamia usambazaji wa maji na chakula kwa
wageni wote wanaokuja kufanya ibada katika Al-kaaba na hili
linaashiria ukarimu walikuwa nao Waarabu. Naye ndiye mtu wa mwanzo
aliyeanzisha uokaji na usambaji wa mikate katika mji wa Makkah na
hili linaonyesha ni jinsi gani alivyowajibika kwa jamii iliyompa dhamana
ya uongozi.
Mwenyezi Mungu aliitakasa nasabu ya Mtume kutokana na uchafu wa
kijahilia. Mababa zake wote walikuwa ni watu watukufu na viongozi
kama ambavyo mamama zake pia walikuwa ni wanawake
waungwana,watakasifu wasio na uchafu wowote.
Lifuatalo ni jedwali na kielelezo kinachoonyesha nasabu ya Mtume
kuanzia kwa babu wake wa nne Mzee Qusway. Jedwali hili litatusaidia
kuelewa koo za Maqureshi huko mbele.
|
|
|
|
|
|
No comments:
Post a Comment