Wednesday, November 21, 2012

KIFO CHA MTOTO CHAMWAGA SIMANZI MTANDAONI

Monday, November 19, 2012

KIFO CHA MTOTO KILIVYOMWAGA SIMANZI MTANDAONI


KIFO CHA MTOTO KILIVYOMWAGA SIMANZI MTANDAONI





Kifo cha mtoto wa mwanahabari aliyekuwa na umri wa miezi 11 huko Ukanda wa Gaza siku ya Jumatano kimesababisha mafuriko ya ujumbe wenye uchungu mtandaoni, pale picha za Jihad Misharawi, ambaye ni mhariri wa video wa kituo cha BBC ya Kiarabi, zilipomuonesha akiwa amebeba mwili wa mwanaye aliyefariki dunia.

Mtoto huyo wa Mishrawi, aitwaye Omar, aliuawa baada ya mashambulizi ya ndege za Israeli mjini Gaza yalipotua kwenye makazi yake mjini humo. Hayo ni kwa mujibu wa duru za BBC.


Omar ni miongoni mwa watu 16 waliouawa huko Gaza tangu Jumatano alasiri, wakiwemo watoto wanne, kama ilivyoripotiwa na kituo cha Televisheni cha Al Arabiya. Mapigano yalianza baada ya Israeli kumlenga kiongozi wa kijeshi wa Hamas Ahmed Ja'abari siku ya Jumatano. Tokea hapo, wapambanaji wa Kipalestina wamekuwa wakirusha makombora kuelekea Israeli.

Awali kifo cha mtoto wa Mishrawi kilisababisha hasira kwa wachangiaji wa mtandaoni na blogu mbalimbali, hususani pindi tukio hilo lilipokwenda kwenye mitandao ya kijamii, na BBC yenyewe ikaonekana kutoripoti vya kutosha juu ya mauaji hayo.


“BBC inapopuuza mauaji yanayofanywa na Israeli dhidi ya mpiga picha wao wenyewe, Wapalestina wategemee nini?" makala moja kwenye blog ya Intifada ilihoji ikidai kuwa kwenye taarifa ya habari ya usiku mtangazaji "alipuuza kabisa" mauaji yaliyofanywa siku ya Jumatano.

Wakati huo huo, mtandao wa haari wa Mashariki ya Kati wa Al-Bawaba uliishambulia tovuti ya BBC, ukidai kuwa mtangazaji aliripoti mtandaoni kuwa mashambulizi ya Israeli "yalilenga wapiganaji wa Gaza," huku akishindwa kuyataja mauaji ya mtoto wa miezi 11 aliyeuawa pamoja na watoto wengine.


Lakini BBC ikazungumza kwa haraka kuhusu kifo cha mtoto Omar. Mwanzo habari zilitangazwa ndani kwa ndani. 

Mhariri wa BBC World Jon Williams aliwatumia wenzake ujumbe mfupi kuhusu kifo cha mtoto huyo. kwa mujibu wa gazeti la Telegraph ujumbe huo ulisema:

Fikra zetu ziko pamoja na mwenzetu Jihad na wenzetu wengine walioko Gaza.
Hiki ni kipindi kigumu sana kwa ofisi nzima ya Gaza.
Tuna bahati kuwa na timu yenye kujituma na yenye ujasiri. Ni ukumbusho muhimu juu ya changamoto zinazowakabili wenzetu wengi walioko huko.


Vile vile makala moja kwenye tovuti ya habari ya BBC iliyorushwa siku ya Alhamisi ilijumuisha video ya mwandishi wa BBC wa idhaa ya Kiarabu, Misharawi, ikiwa na maneno yaliyosomeka: "Mwanangu amefanya nini mpaka afe namna hii?"


Kwa mujibu wa mkuu wa ofisi ya BBC ya mashariki ya Kati,
Paul Danahar, kombora la Israeli liliipiga nyumba ya Misharawi yenye vyumba vinne mjini Gaza siku ya Jumatano na kumua mwanaye, shemeji yake na kumjeruhi kaka yake.

Danahar alizungumza na mwandsihi wa gazeti la Washington Post, akisema kuwa pindi kombora hilo lilipotua, hapakuwepo na mapigano jirani na makazi yake.

“Sote ni timu moja hapa Gaza,” Danahar alimwambia Max Fisher, akisema kuwa Misharawi ni mhariri wa video na picha wa BBC.

Baada ya kutumia "saa kadhaa" pamoja na mwenzake huyo mwenye simanzi, aliandika kwenye mtandao wa Twitter: "Swali linaloulizwa hapa ni kuwa: kama Israeli inaweza kumshambulia mtu aliyepanda pikipiki (kama walivyofanya mwezi uliopita) mtoto wa Jihad aliualiwaje?" aliandika Fisher

No comments:

Post a Comment