NASAHA
المعاصي تؤثر حتى على الدواب، والأشجار، والأرض وعلى المخلوقات.
MAASI HUATHIRI MPAKA WANYAMA,MITI,NA ARDHI NA KILA KILICHO KATIKA ARDHI.
Baada ya kumshkuru Allah na kumtakia rehma Bwana mtume saw yatulazim kila saa,dakika,sekunde,kumshukuru,kumsifu,kumtukuza
Allah kwani hakika tuna tumia maelfu kwa maelfu ya neema za Allah swt
kiasi amabacho hatuwezi kuzidhibiti ni neema ngapi tunazotumia.
Ndugu zangu hakika Bora ya neema ni kumtii Allah na kujiepusha na
makatazo yake,kwani hakika ya binadamu atakapomuasi allah huwa ni sababu
ya kuathirika kila kilicho katika mgongo wa Ardhi ikiwa
Wanyama,wadudu,Mimiea,na vingi vyenginevyo.kwani Maasi ndiyo chanzo cha
kila kitu.
Swahaba wa Mtume saw Ibin Abbas ambaye ni ndugu yake
mtoto wa Ami yake Habru wa Umma huu anasema: قال عبد الله بن عباس رضي
الله عنهما: "إن للحسنة ضياء في الوجه، ونورا في القلب، وسعة في الرزق،
وقوة في البدن، ومحبة في قلوب الخلق، وإن للسيئة سوادا في الوجه، وظلمة في
القلب، ووهنا في البدن، ونقصا في الرزق، وبغضة في قلوب الخلق"
hakika
ya kutenda mambo mema ni Mwangaza katika uso,na ni Nuru katika moyo,na
ni ukunjufu wa rizki,na nguvu katika kiwiliwili,na ni
mahaba(mapenzi)katika nyoyo za watu(viumbe).
Ama hakika ya Uovu ni
weusi katika uso,na giza katika moyo,na umyonge katika kiwiliwili,na
upungufu wa rizki,na kuchukiwa katika nyoyo za watu(viumbe).
hakika tumeona tofauti ya kufanya wema na utakapotenda uovu(kufanya
maasi) hakika kufanya maasi ni jambo baya kwako wewe mwenyewe kwani
inasababisha kupungukiwa na rizki na kuchukiwa na hata viumbe vya
m/mungu,na huathiri maasi hayo ardhini na baharini na vilivyomo kati ya
ardhi na bahari kama anavyotuthibitishia Allah katika Quran
قال اللٰه تعالى: "ظهر الفساد في البر والبحر بما كسبت أيدي الناس ليذيقهم بعض الذي عملوا
لعلهم يرجعون" (الروم آية 41)
41. Ufisadi umedhihiri bara na baharini kwa iliyo yafanya mikono ya watu, ili
Mwenyezi Mungu awaonyeshe baadhi ya waliyo yatenda. Huenda wakarejea kwa kutubu.
Kutokana ubaya wa maasi ulivyokuwa ni mbaya na huathiri kila kiumbe Bwana mtume saw anatueleza katika hadithi hii
عن أبي قتادة بن ربعي أنه كان يحدث أن رسول الله صلى الله عليه وسلم مر
عليه بجنازة فقال "مستريح ومستراح منه" قالوا يا رسول الله ما المستريح
والمستراح منه فقال "العبد المؤمن يستريح من نصب الدنيا والعبد الفاجر
يستريح منه العباد والبلاد والشجر والدواب" (متفق عليه)
hadihi
imetokana Abaa Qataadah bin Raabiiy hakika alikuwa anahadithia ya kuwa
mtume saw ilipita mbele yake jeneza akasema amestaehe,na Amestarehesha
vilivyo ardhini.Masahaba wakamuuliza nini maana yake Amestarehe na
Amestarehesha ewe Mjumbe wa Allah?
Mtume saw akasema Mja Muumini
aliye mwema anapofariki hustarehe kutokana na matatizo na mitihani ya
dunia.Ama Mja Muovu anapofariki hustarehe kwa kuondoka kwake
Binadamu,Miji,miti,Wanyama na Wadudu.
Ndugu zangu hii ndiyo
athari ya maasi inavyokuwa,yatulazimu kurudi kwa Allah haraka kabla
hajatushukia mjumbe wa mauti,kwani huwa mtu anajiangamiza yeye mwenyewe
na anaangamiza na chengine kisicho husika na maasi yale.Taabii na
Mwanachuoni anayeitwa Mujaahid amrehemu Allah anasema maneno haya:
قال مجاهد رحمه الله : إن البهائم تلعن عصاة بني آدم إذا اشتدت السنة – أي
: القحط - وأمسك المطر , وتقول : هذا بشؤم معصية ابن آدم ."
hakika ya
wanyama humlani Asi wa kibinadamu pindi unapozidi ukame ikawa ni sababu
ya kuzulika kwa mvua na husema :ubaya huu (ukame huu)ama matatizo haya
yamesabibishwa na maasi ya Binadamu.
Hakika maneno haya ni yenye
ukweli kabisa kwani Allah anapoteremsha mvua kwa sababu ya utiiji wa
watu huwa ni neema kwa kila kilicho katika mgongo wa Ardhi na
Baharini,mimea hustawi wanyama wakapata malisho,wadudu hufarajika na
mvua hiyo husababisha kuzalika samaki wengi baharini na ikawa ni sababu
ya maisha mazuri ya binadamu. na kinyume chake ni balaa kwa mwenye
kufanya maasi na viumbe vyengine na hili Allah amelithibitisha katika
kitabu chake kitukufu aliposema:
فلينظر الإنسان الى طعامه,اناصببناالماء صبا,ثم شققناالأرض شقا,فانبتنافيها حبا,وعنباوقضبا,وزيتوناونخلا,وحدائق غلبا,وفاكهةوابا,متاعالكم ولانعامكم.
24. Hebu mtu na atazame chakula chake.
25. Hakika Sisi tumemimina maji kwa nguvu,
26. Tena tukaipasua pasua ardhi kwa nguvu,
27. Kisha tukaotesha humo nafaka,
28. Na zabibu, na mimea ya majani,
29. Na mizaituni, na mitende,
30. Na bustani zenye miti iliyo songana baraabara,
31. Na matunda, na malisho ya wanyama;
32. Kwa manufaa yenu na mifugo yenu.
Hakika imetosha kuonyesha ya kwamba kumtii Allah itanufaisha mwenye
kutii na vilivyomo Ardhini na vile vile kumuasi Allah ni sababu tosha ya
kujiathiri wewe mwenyewe na kuathiri na vinginevyo vilivyomo katika
mgomgo wa Ardhi. Hakika amesadikisha Allah na Amesadikisha mtume ya
kwamba Maasi huathiri wanyama,wadudu,mimea,hata majiwe na kila kitu
unachokijuwa na usichokijuwa.
TUMUOMBE ALLAH AZILAINISHE NYOYO ZETU ILI TUPATE KUMTII YEYE NA ASITUJAALIE USUSUAVU WA MOYO IKWA NI SABABU YA KUMUASI YEYE
No comments:
Post a Comment