Muhammad Faraj Salem Al Saiy
Maisha ya Mtume
wa Mwenyezi
Mungu (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa
sallam) ni somo ‘adhimu sana
baada ya somo la Qur-aan tukufu, na hii
ni kwa sababu
ndani yake tunapata faida nyingi sana, zikiwemo
zifuatazo:-
1.
Kujuwa sababu za kuteremshwa kwa aayah
mbali mbali za Qur-aan jambo
litakalotuwezesha kukifahamu
vizuri kitabu cha Mwenyezi Mungu pamoja na kuzifahamu
hukmu zake na Hadiyth zake,
na kuifahamu vizuri Sunnah iliyotakasika
ya Mtume wa Mwenyezi Mungu
Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi
wa sallam).
2.
Kufahamu namna gani Mtume wa
Mwenyezi Mungu (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi
wa sallam) alivyoshirikiana na Swahaabah zake watukufu (Radhiya Allaahu ‘anhum) walivyoipigania diyn ya Mwenyezi
Mungu kwa hali na mali
na kuieneza kila pembe ya
dunia, na pia mafundisho ya hikmah, pamoja
na maarifa mbali mbali aliyowafundisha
Maswahaabah wake kwa ajili ya majukumu
hata wakaweza kusubiri na kustahamili
mashaka na
tabu mbali mbali mpaka pale Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Ta’ala)
Alipowapa yale Aliyowaahidi kwa kuitiisha dunia yote ikawa chini
ya amri yao.
3.
Maisha ya Mtume
wa Mwenyezi
Mungu (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa
sallam) ni muujiza katika miujiza ya Mwenyezi
Mungu, kwani katika kuidurusu Siyrah yake, tutaona
namna gani alivyozaliwa na kulelewa katika mazingara ya kiajabu
na ya kimiujiza
na pia namna
alivyoelimishwa na kulindwa na Mola
wake (Subhaanahu wa Ta’ala).
4.
Tunapata kuwajuwa zaidi watu wa
nyumba ya Mtume wa Mwenyezi
Mungu (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa
sallam) na namna gani walivyoshirikiana
na Maswahaabah wake watukufu (Radhiya Allaahu ‘anhum), tokea siku za
mwanzo, wakahuzunika na kufurahi pamoja,
na wakati huo huo msomaji
wa Siyrah anafurahi kwa furaha
zao na anahuzunika
kwa huzuni zao.
5.
Katika somo hili,
tunaweza kujuwa namna gani Maswahaabah
walivyojifunza katika Madrasah ya Mtume
wao mtukufu (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi
wa sallam), akawalea vizuri na kuwafanya
wawe Ummah bora kuliko Ummah
zote zilizowahi kuteremshiwa watu. Kwani wao ndio
walioisimamia diyn hii na kupiga mifano mema
katika kujitolea nafsi zao mhanga
kwa ajili ya kuutetea Uislamu,
kupigana jihadi na kuwalingania watu katika njia
ya Mwenyezi Mungu, kuonyesha ushujaa, ustahamilivu na uadilifu mbele
ya adui, pamoja na mapenzi
na huruma na ukarimu na
kila sifa njema mbele ya
wenzao.
6.
Katika kuyadurusu maisha ya Mtume
wa Mwenyezi Mungu (Swalla Allaahu
‘alayhi wa aalihi wa sallam)
tutaweza pia kuona na kuonja
ladha ya jihadi na namna
gani Mtume wa Mwenyezi Mungu
(Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi
wa sallam) pamoja na Swahaabah
zake watukufu (Radhiya Allaahu ‘anhum) walivyosimama kidete katika kuipigania
diyn hii tukufu na namna
walivyoweza kusubiri mbele ya adui
na kuvumilia mateso na shida
mbali mbali.
7.
Tutaweza pia kuujuwa
ucha Mungu wao na namna
gani Mtume wa Mwenyezi Mungu
(Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi
wa sallam) Alivyoweza kuzibadilisha na kuzijenga nyoyo
na nafsi zao kwanza, kabla ya kuziendea nyoyo
na nafsi nyingine, na hii
ni tafisiri ya kauli ya
Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Ta’ala)
isemayo:
إِنَّ اللّهَ لاَ يُغَيِّرُ مَا بِقَوْمٍ حَتَّى
يُغَيِّرُواْ مَا بِأَنْفُسِهِمْ
No comments:
Post a Comment