Monday, December 10, 2012


Majambazi yapora mradi wa maji Z’bar

Majambazi yamevamia kituo cha mradi wa maji vijijini na kuiba fedha taslim Shilingi milioni tisa na vifaa mbalimbali katika kijiji cha Kiashange Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Majambazi hao walivamia kituo hicho juzi wakiwa katika gari mbili aina Escudo.
Mbali ya fedha taslim, pia waliiba kompyuta za mkononi mbili, mashine za DVD mbili, simu za mkononi saba na kamera za mradi huo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, ameutaka uongozi wa Mamlaka ya Maji Zanzibar, (Zawa) kuimarisha ulinzi katika miradi ya maendeleo kama hiyo.
Alisema wakati umefika kwa Zawa kuhakikisha walinzi wenye sifa ndiyo wanapewa dhamana ya kulinda miradi mikubwa wakiwa na silaha za moto badala ya kuweka askari wa korokoroni wakiwa na virungu.
Balozi Seif alitoa agizo hilo wakati akiwapa pole watendaji wa kituo hicho cha mradi maji safi vijijini.
Alisema kutokana na mabadiliko ya dunia, ipo haja ya kuimarishwa zaidi ulinzi wa uhakika na kuachana mfumo wa ulinzi wa kutumia virungu ambavyo vimepitwa na wakati hasa katika miradi mikubwa inayofadhiliwa na wafadhili ukiwamo mradi huo.
Aidha, Balozi Seif alivitaka vyombo vya ulinzi kuwasaka majambazi hao mpaka wapatikane na kufikishwa katika vyombo vya sheria.
Awali Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Zanzibar (Awa), Dk. Mustafa Ali Garu, alisema mradi wa maji safi vijijini wa Kiachange ni miongoni mwa miradi mikubwa mitatu inayotarajia kutumia dola milioni 47 za Marekani chini ya ufadhili wa Benki ya Maendeleo ya Afrika.
Mradi huo pia utasadia kuimarisha upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama katika Mkoa wa mjini Magharibi na kisiwani Pemba ambapo SMZ itachangia asilimia 10 ya gharama za ufanikishaji wa mradi huo.
CHANZO: NIPASHE

Rais Kikwete amkabidhi nishani Bikidude

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mrisho Jakaya Kikwete akimkabidhi tunzo Mwimbaji mkongwe wa Zanzibar Bi kidude

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mrisho Jakaya Kikwete akimkabidhi tunzo Mwimbaji mkongwe wa Zanzibar Bi kidude
Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete,akimtunuku Nishani ya Sanaa na Michezo Bi Fatma Baraka Khamis,(Kidude) kupitia Basaza katika sherehe za kutunuku nishani mbali mbali katika viwanja vya Ikulu Dar des Salaam,katika kusherehekea maadhimisho ya miaka 51 ya Uhuru wa Tanganyika

Mazishi ya Mama Jussa yafanyika

Baadhi ya wanafamilia wakiongozwa na Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe Ismail Jussa Ladhu, wakisubiri mwili wa mama yao marehemu Bi Zaynab Suleiman kwa ajili ya kumzika katika makaburi ya Mwanakwerekwe. Mazishi hayo yamehudhuriwa na viongozi mbali mbali wakiwemo Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad na Mwenyekiti wa CUT Taifa Prof. Ibrahim Lipumba.

No comments:

Post a Comment