Uwanja wa michezo wa ndani ( Indoor) wanukia Pemba
Mratibu wa Kamisheni ya Utamaduni na Michezo Pemba, Juma Ali
David, (kulia) akiwapa maelezo wajumbe kutoka Ubalozi wa Japan Nchini
Tanzania, juu ya eneo litakalojengwa uwanja wa Michezo ya ndani, huko
Gombani Chake Chake Pemba jana, wapili kulia ni Rais wa chama cha Judo
Zanzibar,Tsuyoshi Shimahoka (Abdulhalim),akifuatiwa na Afisa Miradi
kutoa ubalozi wa Japan Sayaka Morita,
MSHAMBULIAJI Ali Ahmed Shiboli, aliyepata umaarufu katika
mashindano ya Chalenji mwanzoni mwa mwaka huu jijini Dar es Salaam akiwa
na timu ya Zanzibar Heroes, sasa amesajiliwa na Jamhuri ya Pemba.
Shiboli pia aliwahi kuichezea Simba ya Dar es Salaam, Kagera Sugar na Coastal Union ya Tanga.
Jamhuri imeweza kuzipiku klabu za Duma na Chipukizi ambazo pia zilikuwa zikiwania saini ya mwanandinga huyo.
Shiboli amemuhakikishia mwandishi wa habari hizi kuwa, tayari
ameshamalizana na Jamhuri na kuahidi kujitahidi ili pamoja na wachezaji
wenzake waweze kuiletea mafanikio.
“Ingawa nimepitia klabu tafauti Bara na hapa visiwani, lakini
nilikuwa na ndoto za siku nyingi kuichezea Jamhuri ambayo ni timu yenye
historia kubwa Afrika Mashariki, nashukuru sasa zimetimia”, alisema
Shiboli.
Aidha, alisema kuwa katika klabu hiyo yenye maskani yake Wete Mkoa
wa Kaskazini Pemba, ameshafika na kuwaomba viongozi, wanachama na
wapenzi wa timu hiyo wampe ushirikiano ili aweze kuisaidia katika
mashindano ya kitaifa na kimataifa.
Uongozi wa klabu hiyo itayoshiriki ligi ya mabingwa Afrika mwakani
ikianza na St George ya Ethiopia, umesema kusajiliwa kwa Shiboli
kutazidi kukiimarisha kikosi hicho na kwamba ataongeza nguvu katika
jitihada za kutwaa ubingwa wa Zanzibar na kufanya vyema kwenye michuano
ya CAF.
Katika hatua za kujiimarisha ili kurejesha hadhi yake, hivi
karibuni, Jamhuri iliajiri kocha mpya Sebastian Mkomo, ambaye jana
alitarajiwa kuanza kibarua chake kwa pambano la kirafiki kati ya timu
hiyo na maafande wa Hard Rock
Na Masanja Mabula, Pemba
No comments:
Post a Comment