Thursday, December 13, 2012
OFISI
ya Makamu wa Kwanza wa Rais imemuahidi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti
wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein kuwa itashirikiana nae
katika kusimamia majukumu yake kwa uadilifu na bidii kubwa ili iwepo
jamii iliyosalimika na utumiaji wa dawa za kulevya, UKIMWI, uharibifu wa
Mazingira na kuwajumuisha watu wenye ulemavu.
Maelezo
hayo yametolewa leo na uongozi wa Wizara hiyo, wakati wa mkutano kati
ya uongozi huo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dk. Ali Mohamed Shein, katika kuangalia utekelezaji wa Malengo Makuu
ya Wizara hiyo kwa kipindi cha Aprili- Juni 2011-2012 na Julai-
Septemba 2012-2013.
Katika
mkutano huo uliofanyika Ikulu mjini Zanzibar ambapo pia, Makamu wa
Kwanza Rais Maalim Seif Sharif Hamad na Katibu Mkuu wa Baraza la
Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dk. Abdulhamid Yahaya Mzee walishiriki
kikamilifu.
Akisoma
taarifa ya utangulizi ya utekelezaji wa Malengo makuu hayo ya Wizara,
Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Fatma Fereji alitoa shukurani kwa Rais
pamoja na Makamu wa Kwanza wa Rais ambaye ndiye msimamizi mkuu wa Ofisi
hiyo pamoja na na Makamu wa Pili wa Rais kwa miongozo wanayowapa
katika kutekeleza majukumu yao.
Waziri Fereji, alisema
kuwa juhudi za Dk. Shein ndizo zinazoupelekea uongozi wa Ofisi hiyo
kuwa na msukumo na hamasa katika kufanikisha malengo waliyojiwekea.
Ofisi
hiyo ilimuahidi Dk. Shein kuwa itaendelea kumuunga mkono katika
kufanikisha juhudi hizo ili Zanzibar iwepo bila ya dawa za kulevya, na
kuwa mfano katika uhifadhi wa mazingira, udhibiti wa maambukizi mapya
ya UKIMWI na kuwa na jamii jumuishi.
Akieleza
mafanikio yaliopatikana katika Wizara hiyo, Mhe. Fereji alisema kuwa
ni pamoja na kukamilika kwa tovuti ya Ofisi ya Makamu wa Kwaza wa Rais,
kukamilika kwa Kanuni ya Mifuko ya plastiki na kuchapishwa katika
Gazeti Rasmi la Serikali Namba 113 la mwaka 2011.
Mafanikio
mengine ni pamoja na kukamilika kwa muongozo wa kuanzisha nyumba za
makaazi kwa wanaotaka kuacha kutumia dawa za kulevya yaani sober houses,
muongozo huu ambao utasaidia katika kuleta ufanisi na uwiano wa utoaji
wa huduma za makaazi kwa vijana wanaoacha matumizi ya dawa za kulevya.
Kuundwa
kwa kamati za kitaalamu na usimamizi ya mabadiliko ya tabia nchi, pia,
ni miongoni mwa mafanikio ambapo kamati hizo pamoja na mambo mengine
zitakuwa zinaratibu usimamizi wa masuala ya mabadiliko ya tabianchi
ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kwamba mkakati wa kukabiliana na
mabadiliko ya tabianchi unaandaliwa.
Mafanikio
mengine ni pamoja na kumalizika kwa usajili wa watu wenye ulemavu
katika mikoa yote miwili ya Pemba na Mkoa wa Kaskazini Unguja, taarifa
ambazo zitaweza kusaidia taasisi mbali mbali za Serikali, zisizokuwa za
serikali na mashirika binafsi katika kupanga mipango ya kimaendeleo.
Kuanzisha
maafisa waratibu wa masuala ya Watu Wenye Ulemavu pamoja na kukamilika
na kuzinduliwa kwa Mkakati wa pili wa Taifa wa UKIMWI, mkakati huu
ndio unaotoa muongozo wa utekelezaji wa mapambano dhidi ya ya UKIMWI
kwa kipindi cha miaka mitano.
Mbali
ya mafanikio hayo, Ofisi hiyo pia ilieleza changamoto zake
inazozikabili huku ikieleza jinsi juhudi inazozichukua katika kupambana
nazo ikiwa ni pamoja na namna ya kuwa na matumizi endelevu ya kuvuna
maliasili zisizorejesheka pamoja na uingizaji wa bidhaa chakavu
uliokithiri.
Kutofuata
utaratibu wa uchunguzi wa athari za kimazingira kabla ya kuanza miradi
pamoja na athari za mabadiliko ya tabianchi na kuathiri shughuli za
wananchi kwenye kilimo, huduma ya maji ya kunywa na uvuvi.
Aidha,
Wizara hiyo ulieleza changamoto iliyopo katika uingizaji na utumiaji
wa dawa za kulevya pamoja na udhalilishaji wa watu wenye ulemavu,
unyanyapaa kwa watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI pamoja na makundi
maalumu ambao unajitotokeza katika kutumia huduma za kinga na tiba
ipasavyo.
Nae Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein
alitoa pongezi kwa kwa Ofisi hiyo kutokana na mafanikio iliyoyapata katika utekelezaji wa Mpango kazi.
Aidha, Dk. Shein alisisitiza haja ya kuzifanyia kazi changamoto zilizopo kwa kuwashirikika miongoni mwa wadau husika.
Na Rajab Mkasaba, Ikulu
No comments:
Post a Comment