Tuesday, December 11, 2012

Shirdon atembelea café ya Mogadishu kusikiliza wasiwasi wa wananchi

Desemba 10, 2012

Waziri Mkuu wa Somalia Abdi Farah Shirdon alikutana katika njia isiyo rasmi na wananchi wa Mogadishu katika café moja ya Mogadishu siku ya Jumamosi (tarehe 8 Disemba) uliripoti mtandao wa Shabelle Media Network.
Shirdon alijiunga na wateja katika mkahawa ambayo haikutaja awali kusikiliza mashaka ya watu na kujibu maswali kuhusu usalama, vituo vya ukaguzi vilivyovunjwa hivi karibuni uongozi wa serikali nchini Somalia kwa jumla.
"Sio siku zote serikali ambayo inategwa na matishio bali ni watu, wananchi ambao ndio wanaoteseka sana," Shirdon alisema. "Watu wanapaswa kuiunga mkono serikali kikamilifu ili tuweze kushinda juu ya wale wachache ambao ni waharibifu, watu wanaotaka kutokuwepo na utawala ambao wanajificha miongoni mwa watu na kutenda maovu yao."
Shirdon pia alitembelea maeneo ya Mogadishu ambayo hivi karibuni kuliondolewa vituo haramu vya upekuzi, akifuatana na Waziri wa Mambo ya Ndani na Usalama wa Taifa Abdikarim Hussein Guled. Alisifia kazi za usalama kwa kuzifanya barabara za mji kupitika.

No comments:

Post a Comment