Kamishina wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Prof. Mwesiga Baregu
Vurugu hizo zilitokea kwa mara ya kwanza tangia kuanza kwa ukushanyaji wa tume ya maoni hapa zanbar na zilitokea katika uwanja wa mzalendo kwenye jimbo la Magomeni, na katika uwanja wa mpendae Mkoa wa mjini magharib unguja.
Akizungumza jana niaba ya Tume hio, Prof. Mwesiga Baregu, alithibitisha kuvunjika kwa mkutano huo kwa mara ya pili baada ya kutokea vurugu na kusababisha mabishano baina ya wananchi wenyewe kabla tume hio haijaanza utaratibu wa ukushanyaji wa maoni.
Aidha alisema kuwa juzi katika uwanja Mzalendo Magomeni katika wilaya ya mjini watu wanaodaiwa kuwa siwakaazi halali wa maeneo hayo walikwenda kwa magari ili wakatowe maoni yao lakini watu hao hawakuweza kufanikiwa kutokana na wakaazi wa shehia hio kuwazuia kwa madai kuwa hawakuwa wakaazi halali wa maeneo hayo.
Sambamba na hayo Prof. Baregu alisema kwamba Tume baada ya kuona hali imechafuka iliamua kusitisha shghuli nzima ya ukusanyaji maoni kwa sababu za kiusalama zaidi hususani kutokana na yeye kuwa hapendi kuona wananchi wakitoa maoni huku wakiwa katika ulinzimpia alisema kuwa tume yake ilikuwa na uwezo wa kuimarisha ulinzi mkali kwa kutumia jeshi la polisi ili wananchi waendelee na utaratibu wa kukushanya maoni yao lakini isingekuwa vyema kwa wananchi kutoa maoni yao wakiwa kwenye ulinzi mkali.
Nae Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar, Azizi Juma Mohamed, alithibitisha kutokea kwa vurugu hizo na pia kuvunjwa kwa mikutano hiyo, lakini hakuwa na taarifa za kina kwa kuwa jana alikuwa ametingwa na shughuli za kukaguliwa kwa mkoa wake, ukaguzi unaofanywa na Kamishna wa Polisi Zanzibar. Aliahidi kutoa taarifa zaidi leo.
Kutokana na kuwepo kwa matokeo hayo imekisababisha chama cha wananchi cuf kupitia mkurugenzi wake wa haki za binadamu na mawasiliano ya Umma kutoa taarifa kwa vyombo vya habari katika taarifa hio cuf ilidai kuwa
mwakilishi Salmin Awadh Salmin, pamoja na Waziri Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Fatma Said Ali, ambaye pia ni Kamishna wa Tume wamevuruga zoezi na hatimaye wananchi kushindwa kabisa kutoa maoni yao,” alidai Bimani katika taarifa hiyo.
Alisema Cuf imeshtushwa na hali hiyo ambayo imelenga kuchafua zoezi hilo halali na pia kuinyima Tume nafasi yake ya kuendesha shughuli zake.
Alisema kwamba tokea Tume lilipoanza kazi yake mkoa wa Kusini Unguja Julai mwaka huu hadi Disemba 5 mwaka huu ilipomaliza katika wilaya ya Magharibi Unguja, haijawahi kutokea hali kama hiyo.
“CUF kinatoa wito kwa Tume kuchukua hatua zinazofaa kwa mujibu wa sheria ili kuondoa jeuri na kiburi kwa viongozi wanaotaka kuvuruga kazi ya kukusanya maoni ya wananchi” ilisema taarifa hiyo.
Bimani alisema kitendo kilichofanyika ni uvunjifu wa amani, kinyume na Sheria na pia kukiuka kifungu cha 21 (a) (i)(ii) cha Sheria ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba ya Muungano.
Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimeitahadharisha Tume hiyo inayoongozwa na Jaji Joseph Warioba kuwa macho na njama zinazofanywa na baadhi ya vyama vya siasa za kuandaa makundi ya vijana ambao siyo wakazi wa vituo husika vya kutoa maoni na kusababisha vurugu kutokea.
Tahadhari hiyi ilitolewa na Katibu Msaidizi Mkuu wa Idara ya Itikadi na Uenezi Makao Makuu ya CCM Kisiwanduwi Zanzibar, Ali Mwinyi Msuko, katika taarifa yake baada ya vurugu zilizotokea katika Jimbo la Magomeni na Mpendae wilaya ya Mjini Zanzibar.
Alisema kwamba vitendo vya kupandikiza watoa maoni mamluki vimesababisha vurugu na kuwanyima haki ya kutoa maoni wakazi halali, kitendo ambacho ni kinyume cha Sheria ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
“Vurugu hizo zimesababisha wananchi wa Shehia ya Mzalendo/Magomeni na Mpendae kushindwa kutoa maoni yao kitendo ambacho ni kuwanyima haki yao ya kikatiba,” alisema Msuko.
Alisema CCM imesikitishwa na kitendo cha watu kupakiwa katika magari na kwenda kutoa maoni katika maeneo ambayo hawaishi na kusababisha vurugu.
Aidha, alisema kwamba kitendo cha kutoa maoni zaidi ya mara moja kwa mujibu wa sheria ni kosa na wakati umefika kwa Tume kuchukua hatua kali dhidi ya watoa maoni mamluki.
No comments:
Post a Comment