WIZARA
YA AFYA NA USTAWI WA JAMII IMEKUSUDIA KUANZISHA CHANJO MPYA YA UGONJWA
WA NIMONIA PAMOJA NA UGONJWA KUHARISHA ILI KUPUNGUZA IDADI YA VIFO VYA
WATOTO VINAVYO TOKANA NA MAGONJWA YANAYO WEZA KUZUILIKA.
HAYO YAMEELEZWA NA NAIBU WAZIRI WA AFYA NA USTAWI JAMII ZANZIBAR DK,
SIRA UBWA MAMBOYA WAKATI AKIFUNGUA MKUTANO WA SIKU MOJA WA WADAU WA
CHANJO UTAKAO ZUNGUMZIA KUANZISHWA KWA CHANJO HIYO KATIKA UKUMBI WA
HOTELI YA BWAWANI.
CHANJO HIYO ITAKAYO ZINDULIWA RASMI MWEZI FEBRUARY MWAKANI INA LENGO
LA KUTOKOMWZA MAGOJWA HAYO PAMOJA NA KUPUNGUZA IDADI YA VIFO VYA WATOTO
WALIO CHINI YA UMRI WA MIAKA MITANO.
DK, SIRA AMESEMA KUWA LENGO LA WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII NI
KUTOA CHANJO KWA WATOTO HADI KUFIKIA KIWANGO CHA ASILIMIA TISINI NA TANO
KWA WILAYA ZOTE ZA UNGUJA NA PEMBA.
AMESEMA KUWA WIZARA YA AFYA KWA KUSHIRIKIANA NA WADAU WA CHANJO
YAKIWEMO NA MASHIRIKA YA KIMATAIFA IMEANZISHA CHANJO HIYO ILI KUFIKIA
MALENGO YA MILENIA KWA KUPUNGUZA IDADI YA VIFO VYA WATOTO.
DK, SIRA AMEYASHUKURU MASHIRIKA YA GAVI, WHO, NA UNCEF KWA KUISADIA
WIZARA YA AFYA JUU YA CHANJO HIYO NA KUAHIDI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA
MASHIRIKA HAYO ILI KUFIKIA MALENGO YUALIYO KUSUDIWA.
AKIFUNGA MKUTANO HUO MKUU WA MKOA WA MJINI MAGHARIBI MH, ABDALLAH
MWINYI AMEWATAKA WATAALAMU WA CHANJO KUWA KARIBU NA WAKUU WA WILAYA
PAMOJA NA MAAFISA WENGINE ILI KUFANIKISHA CHANJO HIYO.
No comments:
Post a Comment