Jan
27
2013
WATU wanane wameuawa na wengine kumi na moja kujeruhiwa kutokana na
vurugu zilizizotokea juzi siku ya J'mosi mkoani Mtwara na Itete wilayani Ulanga, mkoani
Mororgoro.
Muuguzi wa zamu katika Hospitali ya Wilaya ya Masasi, Mkomaindo,
Amima Simbo alithibitisha vifo vya watu saba waliofikishwa hospitalini
hapo.
Kwa mujibu wa muuguzi huyo, maiti zilizopokelewa hospitalini hapo
zilionekana zikiwa na matundu yanayodhaniwa kuwa ni ya risasi, baadhi
yao kichwani, begani, viunoni na tumboni.
Aidha majeruhi waliofikishwa hospitalini hapo pia walikuwa na majeraha mbalimbali ikiwamo ya risari.
Aidha majeruhi waliofikishwa hospitalini hapo pia walikuwa na majeraha mbalimbali ikiwamo ya risari.
Habari zaidi zinaeleza kuwa vurugu hizo zilizuka baada ya kundi la
waandamaji, wengi wakiwa vijana waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda
waliokuwa wakipinga mwenzao kukamatwa na kutaka kuvamia Kituo cha
Polisi ili kumwokoa.
Vurugu hizo ziliendelea kuutikisa Mkoa wa Mtwara kwa siku ya pili
mfululizo na kuutikisa Mkoa wa Mtwara, baada ya vurugu nyingine kuibuka
wilayani Masasi jana.
Habari zinasema mbali na vifo na majeruhi, nyumba za wabunge wawili
wa wilaya hiyo zimechomwa moto, ambapo pia magari, trekta, Ofisi za CCM
Wilaya na Ofisi ya Mkurugenzi wa Wilaya ziliharibiwa kwa kuchomwa moto.
Wabunge ambao nyumba zao zimemwa moto ni Mariam Kasembe wa Masasi Mjini na Anna Abdallah Mbunge wa Viti Maalumu wilayani humo.
Juzi vurugu hizo zilitokea katika Mikoa ya Morogoro kati ya wakulima
na wafugaji na kusababisha kifo cha mtu mmoja wakati mkoani Mtwara
wananchi wa eneo la Chikongola waliizingira nyumba ya diwani wa Kata ya
Mikindani, Mohamedi Chehako kwa madai ya kuwahifadhi wachawi ndani ya
nyumba yake.
Katika vurugu hizo polisi walilazimika kutumia silaha yakiwamo mabomu
ya machozi ili kupoza hali ya hewa, ambapo nyumba ya Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi),
Hawa Ghasia ilichomwa moto.
Akizungumza na Mwananchi Jumapili kuhusu vurugu hizo, Mbunge wa
Masasi Mjini, Mariam Kasembe alisema kuwa nyumba yake iliyoko Masasi
mjini imechomwa moto na kuteketea kabisa, huku mali zikiibwa na kwamba
familia yake sasa haina makazi.
Aliongeza kwamba mbali na uharibifu, vurugu hizo zimesababisha pia mama yake mzazi kukimbia na mpaka sasa hajulikani alipo.
“Wamechoma trekta na gari lililokuwepo nyumbani kwangu, watoto wangu
na mume wangu walipoona hali hiyo wakakimbia,” alisema Kasembe akieleza
kuwa hawezi kuthibitisha chanzo cha vurugu hizo, lakini anahisi kuwa
zinatokana na mgogoro wa gesi.
CHANZO MWANACHI
CHANZO MWANACHI
No comments:
Post a Comment