Tuesday, January 1, 2013

JUSSA IKIWA WATAYAKATAA MAONI YA WAZANZIBARI TUTABAKI KUWA NA UJIRANI MWEMA NA TANGANYIKA

jusaa



 
 
 
 
 
 
Rate This

Na Hamed Mazrui

Mjumbe wa baraza kuu Taifa CUF ambae pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe Mh Ismail Jussa amesema kuwa Nchi yetu ya Zanzibar katika mwaka uliopita wa  2012 imefikia hatuwa muhimu sana iliokuwa inasubiriwa  kwa kipindi cha muda   mrefu kwani imewawezesha wananchi wake kutoa maoni yao juu ya muundo  gaini wa Muungano  wanaoutaka  ndani ya nchi yao kati yake na Tanganyika.
Ameyasema hayo wakati alipokuwa akizungumzana wafuasi wa chama cha wananchi cuf pamoja na wananchi mbali mbali  katika mkutano wa hadhara uliofanyika jioni ya leo katika uwanja wa kwamzushi uliopo jimbo la mtoni wilaya ya Mjini Unguja, Mh Jussa amesema kuwa Wananchi wa Zanzibar kudai mamlaka ya nchi yao sio suala la uhizbu kama wananavosema baadhi ya watu wengine isipokuwa ni haki yao ya msingi kwani kutaiwezesha nchi yao kuwa na mamlaka kamili ambapo kutawapelekea kujiamulia wanachokitaka juu ya nchi yao hivo basi baadhi ya watu wanaosema kuwa kudai mamlaka kamili ni uhizbu wanakosea na hawapaswi kusema hivo.
Akibainisha kuhusu mambo yalioikandamiza Zanzibar ndani ya Muungano huu uliopo hivi sasa ni  pamoja na Serikali ya Jamuhuri ya Muungano kuyachukua mambo yasikuwa ya Muungano kuyafanya kua ni ya Muungano jambo ambalo limedumaza nchi yetu kiuchumi zaidi na kuonekana kuwa  ni nchi maskini sana dunian,i akibainisha mambo hayo yalioingizwa kinyemela ndani ya Muungano huo kuwa ni Masuala ya Sarafu suala hilo hapo awali halikuwemo kabisa ndani ya orodha hio nawakati lilipoingizwa hata Serikali ya  Zanzibar haikuwa na Taarifa na walikataa kabisa kuingizwa kwa jambo hilo kwani mpaka kitabu kiliandikwa kwa kuonesha kutokuridhika kwao na kitendo hicho.
Sambamba na hayo Jussa ameleza kuwa Zannzibar ni miongoni mwa Nchi za Visiwa kama zilivo nchi nyengine Duniani hivo basi kwa kawaida Nchi za kisiwa hutegemea zaidi uchumi wake kutokana na Bahari pamoja na utalii lakini hali haipo hivo kwa Zanzibar kwani upande wa pili wa Muungano huu umehodhi mamlaka ya bandari ndani ya Zanzibar pamoja na suala Zima la Utalii kwani hata ukienda huko kwenye Ofisi za Balozi za Tanzania Nje ya nchi wanaitangaza Tanzania kiutalii na sio Zanzibar jambo ambalo ni miongoni mwa sababu zakuikandamiza Zanzibar kwa makusudi.
Aidha mh Jussa ameleza kuwa kuhusu suala la elimu Nchi yetu inakandamizwa sana ni hivi karibuni tu kila mtu kati yetu aliona wazi wazi kuwa Wizara ya Elimu ya Tanzania ilishawazuia wanafunzi wa Zanzibar kutokufanya Mitihani ya  Taifa kidato cha sita kwa madai eti hawana sifa licha ya kuwa walishasoma miaka yote lakini hawakuambiwa kama hawana sifa iweje waambiwe kijuu juu tu, lakini kwa jitihada za Maalim Seif baada tu yakuliongelea jambo lile ndio siku ya pili yake wizara ya Elimu bara wakatoa tamko kuwa wanafunzi wote watafanya mtihani.
Sambamba na hayo Mh Jussa aliendelea kufahamisha kwa kumnukuu Mzee Jumbe pale aliposema   kutokana na matatizo haya yaliopo ndani ya muungano huu kushindwa  kutatuliwa basi kutapelekea hata wenzetu kutoka baadhi ya nchi jirani za Afrika kushindwa kujiunga na Muungano wetu lakini hata sisi wenyewe wahusika wakuu tutashindwa kuendelea nao,
Pamoja na yote mh Jussa alimalizia kwa kuwahakikishia Wazanzibar wote kwa pamoja kuwa wao kama wajumbe wa Baraza la Wawakilishi watahakikisha wanayainda kwa hali yoyote maoni yao waliotoa ya kutaka Zanzibar yenye mamlaka kamili kitaifa na kimataifa na ikitokezea upande wapili wa Muungano huu wakayakataa Maoni yao basi watawaambia kuwa sasa tubaki kuwa marafiki na ujirani mwema tu lakini hatutoendelea tena na Muungano huo tena.
Kwa upande wake Mkurugeni wa Hababri uenezi na Mawasiliano ya Umma kupitia chama hicho Mh Salim Biman amewataka wananchi wa Zanzibari hususani vijani kutokukubali kuchokozeka kwa sasa katika kipindi hichi muhimu cha kuipelekea nchi yetu kuwa huru badala yake wawe watulivu wa hali ya  juu pia amewaasa kufichua vitendo viovu popote pale wanapoviona na kutoa taarifa kwa sehemu zinazohusika kutoka na hali iliopo sasa ya kushamiri kwa matendoo ya uhalifu nchini kwetu.

No comments:

Post a Comment