Kamisheni ya Huduma za Polisi ya Kenya (NPSC) imewasimamisha kazi
maafisa watatu kutokana na kesi ya mtu aliyeshtakiwa kwa kujifanya afisa
wa polisi, liliripoti gazeti la The Standard la Kenya hapo Jumanne
(tarehe 8 Januari).
NPSC imewataja maafisa wapya wa kuchukua nafasi ya mkuu wa polisi wa
Bonde la Ufa John M'Mbijiwe, Kamadoo wa Kikosi cha Kupambana na Wizi wa
Maghala Rimi Ngugi na kamanda wa polisi wa Njoro Peter Nthiga.
Mwenyekiti wa NPSC Johnston Kavuludi alisema kamisheni iliamua
kuwasimamisha kazi maafisa hao watatu baada ya uchunguzi wa awali kuwahusisha na kesi ya mtuhumiwa polisi laghai Joshua Waiganjo.
Kamati imeundwa kuchunguza ni vipi Waiganjo aliweza kufanya kazi kwa
zaidi ya mwaka mmoja bila kufahamika, alisema Kavuludi. Kamati hiyo
imepewa siku 21 kuripoti ugunduzi wake, alisema.
"Tumeweka mfumo wa kuhakikisha kwamba tunajua undani wa suala hili
kiasi ya kwamba uchunguzi makini unafanyika kuonesha namna gani hasa
kosa hili lilitokea na nani ndani ya kikosi cha polisi ni mkosa kwa
namna yoyote ile," Kavuludi alisema.
No comments:
Post a Comment