Katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa tarehe 26 Disemba yenye kichwa cha habari "Kuchochea na Kushawishi Jihadi: MYC mwaka 2012", kikundi hiki kinazungumza kama vile kinawakilisha wote wenye msimamo mkali katika kanda na kujivuna kuhusu mafanikio yake yanayodhaniwa.
"Kadri tunavyokaribia kufikia mwishoni mwa mwaka wa kusisimua, MYC nchini Kenya, Tanzania na Somalia inachukua fursa hii kuwakumbusha Ummah [Jumuiya ya Kiislamu] katika Afrika Mashariki na hususani, Wajahidini nchini Kenya kwa ushindi wetu mkubwa juu ya Makafiri [wasioamini] mwaka 2012," MYC ilisema.
Kikundi chenye makaazi jijini Nairobi, hata hivyo, hakina operesheni nchini Tanzania au Somalia.
Kikundi hiki kinadai kuhusika kwa kutuma "ujumbe unashambulia sana kuua …kwa makafiri kwa karibu kila wiki" kwa miezi 11.
"Kila wakati, MYC simba na watoto walikabiliana na fedheha ya makafiri kwa umadhubuti na kwa kuijiamini kwa pamoja katika uwanja wa vita nchini Kenya na mahali ambapo waliagizwa na Allah, hata kwa kutoa sadaka maisha ya ujana wao katika kulinda dini yetu ya thamani," MYC ilisema.
MYC chadai malipo kwa vitendo vya al-Shabaab
Ingawa Kikundi cha Ufuatiliaji cha Umoja wa Taifa huko Eritrea na Somalia kilikitaja MYC kama sehemu ya kuajiri, kuchangisha fedha na mafunzo ya vikosi vya al-Shabaab nchini Kenya, kikiongea kama vile viongozi na wapiganaji wa al-Shabaab walio katika MYC ni madai yasiyo na ukweli, wachambuzi walisema.MYC kilidokeza kuongoza au kuhusika na mashambulizi mbalimbali ya kigaidi ambayo yametokea nchini Kenya au Somalia mwaka mzima 2012, lakini polisi ya Kenya haijakihusisha MYC na matukio yoyote hadi sasa, kwa mujibu wa Meja Mstaafu wa Jeshi la Kenya Bashir Hajji Abdullahi.
Abdullahi alisema kundi linaizungumzia al-Shabaab kama vile hao wawili ni kitu kimoja na vinafanana ili kudai fedha kwa ajili ya vitendo vya kundi la kigaidi la Somalia.
Insha'Allah, kwa msaada wa ndugu zetu wa Mujahideen nchini Somalia, Yemen, Nigeria na sasa Mali, vita vyetu vitakatifu kama sehemu ya AQEA [al-Qaeda Afrika Mashariki] vitaendelea kushawishi mashujaa zaidi na kutoa msukumo kwa watoto ambao wameeleza mwaka wa 'neema' wa MYC wa 2012," ilisema taarifa ya MYC.
Mkuu wa Jimbo la Kaskazini Mashariki James ole Seriani alisema MYC haina itikadi yake na inajulikana tu kwa kuajiri kikosi kwa ajili ya al-Shabaab.
Wakati wa "mwaka wake wa mafanikio", kwa hakika MYC kilishindwa katika jitihada zake za kuajiri kwa kuwa vijana wengi wa Kenya kilichodai walijiunga na al-Shabaab waliamua kurudi nyumbani na kujenga upya maisha ya kawaida, alisema. "Wakati kinaajiri vijana kujiunga na vita nchini Somalia, dazeni zao waliondoka baada ya kutambua fedha walizokuwa wakiahidiwa zilipunguzwa," Seriani aliiambia Sabahi.
MYC chakosa uongozi, chaongeza umuhimu
MYC kilianza kama asasi ya kijamii mwaka 2008 na kinaongozwa na Mkenya anayeitwa Ahmad Iman Ali, ambaye pia anajulikana kama Abdul Fatah wa Kismayo. Mwezi Januari 2012, al-Shabaab ilimteua Ali kuwa kiongozi mkuu nchini Kenya kutokana na jitihada zake za kuajiri kwa ajili ya wapiganaji wa Somalia.Ali alipoonekana mara ya mwisho ni Somalia mwaka 2009, kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa. Hata hivyo licha ya mpango wa Ali kupigana pamoja na wapiganaji wa miguu wa al-Shabaab nchini Somalia, kumekuwa hakuna jitihada zinazojulikana na viongozi wa al-Shabaab kumteua katika safu yake ya viongozi.
Wapiganaji wengine wa kigeni, kwa upande mwingine, waliweza kufikia hali ya kuinuliwa ndani ya al-Shabaab na wakati mwingine hata walitokea katika matukio ya umma wakiwa pamoja na uongozi wao. Hawa walikuwa ni pamoja na mwenyeji wa Visiwa vya Comoro Fazul Abdullah Mohammed, kiongozi wa al-Qaeda katika Afrika Mashariki ambaye aliuawa mwezi Juni 2011 katika kituo cha ukaguzi huko Mogadishu, na mwanajihadi aliyezaliwa Marekani Omar Hammami, pia anajulikana kama Abu Mansoor al-Amriki, ambaye alijiunga na al-Shabaab katika uwanja wa vita.
Katika tamko lililotolewa kwa vyombo vya habari, MYC ilieleza "wafia dini wengi walizalishwa na MYC katika uwanja wa vita". Hata hivyo, baadhi ya wanaume waliwataja -- Sheikh Aboud Rogo, Sheikh Samir Khan, Mohamed Kassim na Amir Musa Osodov -- kwamba kimsingi hawakua viongozo wala wanafunzi wa MYC, lakini badala yake walijihusisha na al-Qaeda, al-Shabaab au vikundi vingine, alisema Meja Abdullahi.
"Wote ambao walikamatwa na kutuhumiwa kwa [ugaidi] makosa yanayohusiana kama vile Abdimajid Yasin Mohamed, anayejulikana kama Hussein, ambaye [alihukumiwa jela] kwa miaka 59, na Elgiva Bwire Oliacha, ambaye alihukumiwa maisha jela, walipata kiapo cha utii kwa al-Shabaab na sio MYC," alisema.
David Ochami, mwandishi wa habari huko Mombasa ambaye anafuatilia shughuli za vikundi vya wanamgambo huko Mashariki ya kati na Pembe ya Afrika, alisema MYC inajieleza yenyewe ikizungumzia harakati yote ya msimamo mkali katika eneo, bado kikundi hakina viongozi maarufu au wanaojulikana vizuri. Kwa hiyo kinakimbilia katika vyombo vya habari vya kijamii kutolea viisho.
Katika picha iliyotumwa katika akaunti ya Twita ya MYC tarehe 26 Disemba iliyokuwa na kichwa cha habari "Ukumbi wa Umaarufu wa MYC wa mwaka 2012", Mohammed na Bwire ni miongoni mwa watu ambao kikundi kinasema "MYC waliobainishwa mwaka 2012".
Simiyu Werunga, mshauri wa kitaalamu wa usalama mwenye makaazi jijini Nairobi, alisema licha ya ukosefu wa shughuli wa MYC mwaka 2012, hitaji lake la uangalizi wa vikosi vya usalama kuhalalishwa kwa umma.
"Wakati ambapo hawajafanya chochote muhimu, hawawezi kufukuzwa," Werunga aliiambia Sabahi. "Ni wakati wa matukio ya kitaifa ambapo makundi ya uhalifu yanataka kutambulika, kampeni za kisiasa na uchaguzi unaokuja unatoa fursa kwa vikundi kama MYC."
No comments:
Post a Comment