Jan
3
2013
DARAJA la Mnung’una lililopo Kijiji cha Msisi, linalounganisha
barabara kuu ya Singida hadi Mwanza limebomoka kutokana na mvua kubwa
zinazoendelea kunyesha mkoani hapa.
Hali hiyo imesababisha foleni kubwa ya magari yaliyokwama yanayokadiriwa kufikia zaidi ya 500. Pia mawasiliano kati ya mikoa mbalimbali ikiwamo ya Kanda ya Ziwa na nchi jirani yamekatika.
Mmoja wa madereva walioathirika na kubomoka kwa daraja hilo, George Medadi, aliyekuwa akitokea Mwanza kuelekea Dar es Salaam, alisema daraja hilo limekatika kutokana na kujengwa chini ya kiwango.
Aidha, wenyeji wa kijiji hicho walisema kalavati zilizotumika kujengea daraja hilo ni zile zilizowekwa wakati wa uongozi wa Nalaila Kiula alipokuwa Waziri wa Ujenzi.
Mkuu wa Wilaya ya Singida, Queen Mlozi, alisema kwa kuanzia wameimarisha ulinzi katika eneo hilo pamoja na kufungua kituo kidogo cha kutolea huduma ya afya na kudhibiti uwezekano wa kutokea kwa magonjwa ya mlipuko.
“Pia tumefungua barabara ya Singida-Ndago–Misigiri kwa ajili ya kutumiwa na mabasi ya abiria na yale yenye uzito chini ya tani 10. Vile vile tunaangalia uwezekano wa kuangalia ni namna gani watu waliokwama wanapata chakula,” alisema.
Meneja wa TANROADS Mkoa wa Singida, Mhandisi Yustaki Kangole, ambaye alifika na wahandisi wa Kampuni ya Chico, alisema wamekubaliana wafukie shimo kwa vifusi vya mawe makubwa ili barabara hiyo ianze kutumika.
Wakati huohuo, Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Edward ole Lenga, alisema raia mmoja wa China, amefariki dunia baada ya gari lake kusombwa na maji ya Mto Kaka jirani na Kijiji cha Gumanga.
Alisema Mchina huyo ambaye hajafahamika jina, alisombwa na maji ya mto juzi, majira ya jioni wakati akikatisha katika mto huo akiwa na mtoto wake aliyenusurika kifo.
TANZANIA DAIMA.

No comments:
Post a Comment