28 Januari, 2013 - Saa 09:13 GMT
Wanajeshi wa Ufaransa, nchuini Mali, wameweza kudhibiti uwanja wa ndege
katika mji muhimu wa Timbuktu.
Kwa mujibu wa afisaa majeshi ya hayo, waliudhubiti mji huo bila upinzani kutoka kwa wapiganaji wa kiisilamu.Siku ya Jumamosi , waliuteka mji wa Gao, mji wenye idadi kubwa ya watu nchini Mali.
Maelfu ya watu walikusanyika kwenye barabara za mji kusherehekea kuwasili kwa wanajeshi hao.
Wapiganaji wa kiisilamu waliteka eneo la Kaskazini mwa nchi mwaka jana lakini wamekuwa wakishindwa tangu majeshi ya Ufaransa kuanza kuwashambulia mapema mwezi huu.
Mwandishi wa BBC nchini Mali anasema Wafaransa wanatarajiwa kuikomboa Timbuktu bila ya tatizo.
Ndege za Ufaransa piya zimeshambulia mji wa Kidal ambako ndiko wapiganaji walianza uvamizi wao mwezi Machi mwaka jana.
Jumamosi wanajeshi wa Ufaransa na Mali waliukomboa mji wa Gao uliokuwa ngome ya wapiganaji.
Na Mali ndio swala muhimu linalojadiliwa kati ya viongozi wa nchi za Umoja wa Afrika, AU, wanaokutana mjini Addis Ababa, Ethiopia.
Sasa nchi zaidi za Afrika zinatarajiwa kuchangia wanajeshi katika kikosi cha kimataifa kitachokwenda Mali, mbali ya wale walioshafika nchini humo
No comments:
Post a Comment