29 Januari, 2013 - Saa 07:30 GMT
Vikosi vya majeshi
vinavyoongozwa na ufaransa kaskazini mwa Mali vimeudhibiti mji wa
Timbuktu katika harakati za kukomboa eneo la kaskazini mwa Mali kutoka
mikono ya wanamgambo wa kiislamu wanaohusishwa na kundi la kigaidi la
Alqaeda.
Makamanda wa jeshi la Ufaransa wanasema kuwa
wanajeshi wanashika doria kwenye barabara za miji wakilenga kuwafurusha
wapiganaji waliosalia.Wakati huo huo mkutano wa wafadhili wa Mali unatarajiwa kufanyika katika mji mkuu wa Ethiopia -Adis Ababa hii leo kuchangisha pesa kwa ajili vikosi vya kimataifa vinavyopigana dhidi ya waasi wa Kiislam.
Gharama za kuendesha harakati za kijeshi nchini Mali zinakadiriwa kuwa kati ya dolla milioni mia tano na dola bilioni moja .
Huku ahadi za misaada zilizotolewa hadi sasa na Mataifa ya Afrika na muungano wa ulaya zikiwa ni dola milioni moja, zaidi ya wahisani sitini walioalikwa katika mkutano huo wanatarajiwa kuziba pengo hilo.
Na Mkutano mwingine unafanyika mjini Brassels kuamua juu ya kutumwa kwa kikosi cha muungano wa ulaya cha kutoa mafunzo kwa askari wa serikali ya mali.
.Tayari Uingereza itatoa wakufunzi kwa ajili ya mpango huo
Muungabno wa Ulaya ambao umekalimisha mkutano
wake mjini humo, unatumai kuwa kongamano hilo litaweza kuchangisha pesa
za kikosi cha pamoja kukabiliana na waasio hao.Wanajeshi wa Ufaransa, nchini Mali, siku ya Jumatatu, waliweza kudhibiti uwanja wa ndege katika mji muhimu wa Timbuktu.
Kwa mujibu wa afisaa majeshi hayo, waliudhubiti mji huo bila upinzani kutoka kwa wapiganaji wa kiisilamu.
Wanajeshi wa Mali na Ufaransa, wamekuwa wakipigana kuelezea Kaskazini mwa nchi dhidi ya wapiganaji wa kiisilamu.
Siku ya Jumamosi , waliuteka mji wa Gao, mji wenye idadi kubwa ya watu nchini Mali.
Maelfu ya watu walikusanyika kwenye barabara za mji kusherehekea kuwasili kwa wanajeshi hao.
Wapiganaji wa kiisilamu waliteka eneo la Kaskazini mwa nchi mwaka jana lakini wamekuwa wakishindwa tangu majeshi ya Ufaransa kuanza kuwashambulia mapema mwezi huu.
Mwandishi wa BBC nchini Mali anasema Wafaransa wanatarajiwa kuikomboa Timbuktu bila ya tatizo.
Ndege za Ufaransa piya zimeshambulia mji wa Kidal ambako ndiko wapiganaji walianza uvamizi wao mwezi Machi mwaka jana.Na Mali ndio swala muhimu linalojadiliwa kati ya viongozi wa nchi za Umoja wa Afrika, AU, wanaokutana mjini Addis Ababa, Ethiopia.
Sasa nchi zaidi za Afrika zinatarajiwa kuchangia wanajeshi katika kikosi cha kimataifa kitachokwenda Mali, mbali ya wale walioshafika nchini humo.
No comments:
Post a Comment