Mbunge wa Jimbo la Wawi kupitia
Chama cha Wananchi CUF,Mh Hamad Rashid
SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar, imetakiwa kuiga Serikali ya Muungano,
kwa kuanza sasa mchakato wa kuiandika upya Katiba ya Zanzibar ambayo
inakabiliwa na upungufu kadhaa, ukiwamo wa kutowekwa vizuri muundo wa
Serikali ya Umoja wa kitaifa.
Mbunge wa Jimbo la Wawi (CUF), Hamad Rashid, alitoa wito huo jana mjini
hapa, wakati akizungumza kuhusiana na mchakato wa katiba unaoendelea
sasa na pia uwapo wa Katiba ya Zanzibar. Alisema mchakato wa
kubarekebisha ama kuandikwa upya Katiba ya Zanzibar ni wa lazima kwa
sasa ili kuepusha michanganyiko kwa watendaji na kwamba marekebisho hayo
yatakwenda sambamba na ya bara.
“Ni wakati mwafaka sasa Serikali ya Zanzibar kuona umuhimu wa kuanza
sasa mchakato wa kuibadilisha Katiba ya Zanzibar kwani pia inaweza
kuguswa sana na mabadiliko ya Katiba ya Muungano”, alisema Rashid.
Alisema miongoni mwa mapungufu yaliyopo sasa kwenye Katiba ya Zanzibar
ni Tume ya uchaguzi kuwa ndio yenye uamuzi wa mwisho baada ya kutangaza
matokeo,mfumo wa Serikali ya umoja wa kitaifa kitowekwa vizuri na pia
hakuna mpangilio mzuri wa utekelezaji wa majukumu ya Serikali na sera.
“Nadhani kuna kila sababu ya Wazanzibar kukaa na kuipitia Katiba yao na
hili ni jambo ambalo lipo wazi katika mazingira ya sasa ili kuwe na
katiba bora”alisema Rashid.
Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 imefanyiwa marekebisho kadhaa kwa sasa, ikiwamo kuongeza Serikali ya Umoja ya kitaifa na masuala ya Tume huru ya uchaguzi.
Hata hivyo, katiba hiyo, huenda ikaathiriwa na Katiba Mpya ya Muungano,
ambayo ipo katika mchakato wa kuandikwa upya na mwezi Novemba rasimu ya
katiba hiyo, inatarajiwa kufikishwa bungeni na baadaye itapelekwa katika
Baraza la Katiba na imepangwa kukamilika Aprili mwakani.
Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 imefanyiwa marekebisho kadhaa kwa sasa, ikiwamo kuongeza Serikali ya Umoja ya kitaifa na masuala ya Tume huru ya uchaguzi.
No comments:
Post a Comment