Thursday, February 7, 2013

Iran yakataa mazungumzo na Marekani

 7 Februari, 2013 - Saa 12:24 GMT
Rais wa Iran Ahmedinejad amekuwa katika majibizano na Marekani kuhusu mpango wake wa nuklia

Kiongozi wa kiroho nchini Iran,Ayatollah Ali Khamenei, amekataa kata kata pendekezo la Marekani kwua nchi hizo mbili zifanye mazungumzo ya ana kwa ana kuhusu mpango wake wa nuklia.
Katika taarifa iliyocahpishwa kwenye mtandao wake, ,Ayatollah Ali Khamenei, alinukuliwa akisema kuwa kutano kama huo hautasuluhisha matatizo yoyote.
Aliituhumu Marekani kwa kuwa kama nchi inayoitisha Iran kwa bunduki, na kusema kuwa Iran haitatishika kwa vyovyote.
Hili ndio jibu la kwanza la Khamenei kwa wazo la Marekani kufanya mazungumzo na Iran kuhusu mpango wake wa Nuklia.
Wazo hili lilipendekezwa na makamu wa rais wa Marekani Joe Biden wiki jana.
Hata hivyo wazo hilo lilipongezwa na waziri wa mashauri ya kigeni wa Iran.
Lakini mwenye usemi wa mwisho kuhusu mambo ya kigeni ni kiongozi huyo wa kiroho.

No comments:

Post a Comment