Wednesday, February 20, 2013

Kanisa lateketezwa Zanzibar

 20 Februari, 2013 - Saa 08:07 GMT
Duru zinasema kanisa hilo lilichomwa kufuatia mgogoro wa ardhi
Kanisa liliokuwa linajengwa kisiwani Zanzibar, limeteketezwa hapo jana, masaa 48 baada ya mauaji ya padri wa kanisa katoliki.
Lakini polisi wamesema kuwa hakuna majeruhi.
Inaarifiwa kanisa hilo la kiivanjelisti lilichomwa moto na watu wasiojulikana katika kisiwa hicho chenye waumini wengi wa kiisilamu.
Sehemu ndogo ya ya kanisa katika kisiwa cha Unguja,ilichomwa pamoja na mamia ya viti.
Washambuliaji waliiharibu kanisa hilo mwaka jana katika kile wengi walitaja kama mgogoro wa umiliki wa shamba ambako kanisa hilo lilikuwa limejengwa
Kanisa hilo lilikuwa linajengwa upya.
Hata hivyo haikujulikana mara moja ikiwa shambulizi la hapo jana lilihusika moja kwa moja na mgogoro wa wardhi au ikiwa ni kazi ya makundi yenye itikadi kali.
Kasisi Evarist Mushi alipigwa risasi nje ya kanisa lake Jumapili likiwa shambulizi la pili kama hilo katika kisiwa hicho chenye waumini wengi wa kiisilamu katika miezi ya hivi karibuni.
Jamii ya wakristo, ni ndogo sana Zanzibar ikikisiwa kuwa asilimia moja nukta mbili ya idadi ya watu kisiwani humo.
Kumekuwa na taharuki kati ya jamii hizo mbili katika miezi miwili iliyopita
Utalii ndio uti wa mgongo wa nchi hiyo uikiipatia mamilioni pesa za kigeni.

No comments:

Post a Comment