"Kizuizi hicho kilichowekwa na Umoja wa Mataifa cha kuagiza silaha nje kuingia nchini Somalia kinazuia serikali kuwa na kiwango cha juu kabisa cha silaha kuimarisha jeshi la taifa, ambalo lina uhaba wa vifaa vya kijeshi inavyohitaji," alisema Mohamed Farah, ofisa wa jeshi mstaafu.
Kuna mahitaji ya haraka ya kujenga jeshi la taifa ili liwe na uwezo wa kutimiza majukumu yake ya usalama badala ya kutegemea vikosi vya nje, kama vile Misheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia, alisema. "[kwa kipindi cha muda mrefu] ni jeshi la taifa tu litaweza kushughulikia hali ya usalama katika nchi [lakini iwapo tu] litakuwa na silaha za kutosha," Farah aliiambia Sabahi.
Serikali ya Somalia imeongeza juhudi zake katika miezi ya hivi karibuni kushinikiza jumuiya za kimataifa kuondoa vikwazo vya silaha ambavyo iliwekwa kwa Somalia kutoka mwaka 1992.
Mwezi Oktoba 2012, Umoja wa Afrika ilitoa wito kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kupitia upya vikwazo vya silaha ambavyo vimewekwa kwa Somalia.
Katika hotuba aliyoitoa katika mkutano wa wakuu wa nchi wa Umoja wa Afrika huko Addis Ababa tarehe 27 Januari, Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud alielezea umuhimu wa kuondoa vikwazo hivyo.
"Somalia imetoka mbali na sasa inahitaji msaada wa dunia," alisema. "Tunaomba vikwazo vya silaha viondolewe ili tuweze kujenga tena vikosi vya nchi yetu na kulinda uhuru wa nchi yetu," alisema.
Katibu Mkuu wa UN Ban Ki-moon baadaye aliwasilisha pendekezo kwa Baraza la Usalama tarehe 1 Februari.
"Kuongeza jitihada ... kunahitajika kwa haraka ili kuendeleza Vikosi vya Ulinzi vya Taifa vya Somalia," Ban alisema katika taarifa. "Kuhusiana na hilo, Baraza la Usalama linaweza kutaka kuzingatia maombi yaliyoombwa tena na serikali ya kuondoa vikwazo vya silaha."
Katika taarifa iliyotolewa na ofisi yake tarehe 6 Februari, Waziri Mkuu wa Somalia Abdi Farah Shirdon aliikaribisha kauli ya Ban.
"Leo hii Somalia ina msimamo imara kuliko ilivyokuwa zaidi ya miaka 20 iliyopita na dunia yote inatambua hilo," Shirdon alisema. "Bado tuna safari ndefu na ninatilia mkazo kwamba ripoti hiyo ina matokeo mazito, ambayo tutaichunguza kwa makini."
Siku ya Alhamisi (tarehe 14 Februari), Waziri wa Mambo ya Nje wa Somalia Fowsiyo Yusuf Hajji Aadan alilihutubia baraza, akiagiza tena kwamba vizuizi viongezwe ili kuruhusu vikosi vyenye silaha vya Somalia kupigana na al-Shabaab. "Kusafisha mabaki ya al-Shabaab ndiyo kipaumbele yetu," alisema.
"Somalia kimetoka katika kipindi cha mpito na kuwa nchi huru, lakini inahitaji kuimarisha vikosi vyake ili kuweza kuilinda nchi yake huru," alisema kanali mstaafu Hassan Rage, ambaye alitumikia Jeshi la Taifa la Somalia chini ya utawala wa Mohamed Siad Barre. Hali ya sasa ni fursa kubwa ambayo serikali ya Somalia inapaswa kuitumia ili ifanikiwe, alisema.
Kuhakikisha silaha haziangukii katika mikono isiyohusika
Omar Dahir, ambaye anasimamia Kituo cha Usuluhishi na Mazungumzo kilichopo Mogadishu, alisema serikali ya Somalia inahitaji kununua silaha ili kushinda mapigano dhidi ya al-Shabaab, lakini pia inahitaji kuonyesha kwamba inaweza kuzifuatilia vizuri silaha hizo."Serikali mpya inatakiwa kuihakikishia jumuiya ya kimataifa kwamba silaha hizo hazitaangukia mikononi mwa vikundi vya kigaidi katika hali ambayo kizuizi kimewekwa," aliiambia Sabahi.
"Jumuiya ya kimataifa inatakiwa kujua kwamba jeshi la Somalia linapambana na adui ambaye anamiliki silaha ambazo zinaweza kuwa na nguvu kuliko walizonazo," alisema. "Kwa sababu hiyo, sio rahisi kumpiga adui huyu isipokuwa kama jeshi litajiandaa kwa silaha kubwa kama vile vifaru, magari ya kutunzia silaha na vifaa vingine vya kijeshi kama hivyo. Hili halitatokea kwa sababu ya vizuizi vya silaha vilivyowekwa."
Serikali ya Somalia bado haijatangaza mpango wala mfumo wowote maalumu itakaotumia kutafuta na kudhibiti kuingia kwa wingi silaha mpya kama vizuizi vitaondolewa.
No comments:
Post a Comment