Wednesday, February 13, 2013
MAADHIMISHO YA SIKU YA RADIO DUNIANI YAFANYIKA Z,BAR
Kuwepo kwa Mapinduzi ya Vyombo vya Habari Nchini ikiwemo Radio ni moja kati ya sababu inayopelekea kukuza kiwango cha Maendeleo na hatimae kuleta uwelewa kwa jamii na Taifa kwa ujumla.
Kauli hio imetolewa na Bi Maryam Hamdan katika maadhimisho ya Siku ya Radio Duniani, ambae ni Mjumbe wa Baraza la Habari Tanzania(MCT)katika ukumbi wa watu wenye Ulemavu kikwajuni wilaya ya Mjini Unguja, katika maadhimisho hayo yaliyoandaliwa na Barazaa la Habari Tanzani.
Bi:Maryam amesema uanzishwaji wa Radio hapa Nchini ulikuwa ni wa hali ngumu uliojulikana kwa jina la Publick audio service ambao ulianza mnamo mwaka 1933.
Aidha amesema kuwepo kwa huduma za Radio kipindi hicho ilikuwa ni hali ngumu ukilinganisjh
a na hivi sasa kwani walikuwa wakitumia magari kwa ajili ya usambazaji wa habari na utangazaji mwengine wa matangazo tofauti.
Bi:Maryama amesema mnamo mwaka 1948 Zanzibar ilikuwa ina Radio moja tu ambayo ilikuwa ikimilikiwa na Serikali na iliweza kuendesha matangazo yake kwa saa moja tu kwa siku nzima hali ambayo ilikuwa haikidhi mahitaji ya Wananchi wa Zanzibar.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Tume ya Utangazaji Zanzibar Chande Omar amezitaja baadhi ya changamoto zinazokabili vyombo vya habari vya private hapa Zanzibar ikiwa ni Pamoja na kukosa ushindani wa Vyombo vya Habari kutokana na kufanana kwa vipindi vyao pamoja na kubaguliwa kwa baadhi ya waandishi wa Habari ikiwemo na kupata maslahi madogo jambo ambalo linawarudisha nyuma na kutokuwa na uendaji mzuri wa kazi zao.
Nae mtangazaji wa Chuchu Fm Radio Mulhat Yussuf amesema kuwa miongoni mwa changamoto zinazozikabili vyombo vya habari hapa Zanzibar kutokuwezeshwa kwa waandishi wa habari na waajiri wao kuweza kwenda kuandika habari za vijijini na badala yake vyombo vya habari hulalia upande a mjini tu na kusahau maeneo yaliyo nje ya mji wa Zanzibar.
Siku ya maadhimisho ya Radio Duniani huadhimishwa kila mwaka mara moja mnamo tarehe 13/2
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment