18 Februari, 2013 - Saa 11:10 GMT

Kaburi la marehemu Sergei Magnitsky
Mahakama moja nchini Urusi
imesikiza kesi ya matayarisho dhidi ya marehemu wakili aliyekuwa
anapinga vikali ufisadi nchini humo. Marehemu Sergei Magnitsky,
alifariki mwaka 2009.
Mahakama ilisema kwamba kesi itaanza tarehe 4
Machi. Inaaminika kwamba hii ndiyo mara ya kwanza katika historia ya
Urusi kwa mshtakiwa kufunguliwa kesi baada ya kifo chake.Kifo chake mwaka mmoja baadaye kilizua mzozo wa kidiplomasia kati ya Urusi na Marekani.
Mwaka ulipopita Marekani ilipitisha Sheria ya Magnitsky, inayowaweka watu wasiotakikanakwenye orodha maalum.Watu hao huwa ni wale ambao wanashukiwa kuwa wamekiuka haki za binadamu.
Kwa upanda wake, Rais Vladimir Putin wa Urusi alitia saini sheria ya kuwazuia Wamarekani kuwaasili mayatima Warusi.
No comments:
Post a Comment