26 Februari, 2013 - Saa 10:23 GMT

Jeshi la Ivory Coast linatuhumiwa kwa ukiukwaji wa haki za binadamu
Ripoti kutoka katika
shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limesema
kuwa mpango wa amani na maridhiano nchini Ivory Coast umelemazwa na visa
vya ukiukaji wa haki za binadamu vinavyotekelezwa na wanajeshi.
Zaidi ya miezi sita shirika hilo limeandaa
ripoti kuhusu mateso, mauaji ya kiholela na kukamatwa kinyume cha sheria
na jeshi la nchi lililobuniwa na rais Allassane Ouattara.Jeshi hilo lilitakiwa kuchanganywa na lile la mtangulizi wa , Laurent Gbagbo, baada ya ghasia ya baada ya uchaguzi ya 2010.
Duru zinasema kuwa jeshi pamoja na wapiganaji wanafanya uhalifu bila kujali sheria.
No comments:
Post a Comment