Feb
12
2013
WAZIRI wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe amesema kuwa atasitisha
mikataba yote ya magari yanayohusika kubeba mafuta na kusambaza katika
Shirika la Reli Tanzania (TRL) kutokana na hasara inayopatikana badala
yake kutumia usafiri wa shirika hilo.
Mwakyembe alisema hayo mjini Morogoro alipofanya ziara ya kushtukiza
kwenye stesheni ya reli iliyopo mjini Morogoro na kudai kuwa hatakuwa
tayari kuendelea kufumbia macho suala hili la usafirishaji wa mafuta kwa
magari wakati shirika hilo lina uwezo wa kusafirisha mafuta kwa kutumia
usafiri wao.
Alisema endapo shirika litatumia mabehewa yake kusafirishia mafuta
shirika halitapata hasara kama inayoendelea kupata kutokana na kutumia
magari binafsi kusambaza mafuta kwenye stesheni zote nchini. Kwa upande
wa wafanyakazi wa shirika hilo Kituo cha Morogoro, Taferi Dimisheni na
Ramadhani Dalueshi, walisema kuwa wanafanya kazi katika mazingira magumu
licha ya kuwa taifa linategemea pato kupitia shirika hilo.
Walisema kumekuwa na tatizo la mabehewa ya mizigo kukaa muda mrefu
kituoni hapo kutokana na kukosekana kwa mafuta katika kituo hicho.
“Inafikia wakati mafundi injini wanashindwa kutengeneza injini za treni
kutokana na kukosekana kwa mafuta na kusababisha msongamano wa mabehewa
ambayo yana mizigo ya wateja wao,” alisema Taferi
Kwa upande wake, dereva wa treni inayofanya safari zake kati ya Dar es
Salaam na Morogoro, Rango Mboma alisema kuwa madereva wamekuwa wakifanya
kazi katika mazingira magumu hali inayowasababisha kuwa na madeni mengi
kutokana na kutegemewa na familia zao.
Alisema kuwa kipato wanachopata wao hata dereva wa boda oda wanawazidi
kwa kipato hivyo Serikali inatakiwa kuwaboreshea masilahi wafanyakazi wa
kituo hicho.
Akitoa ufafanuzi wa madai hayo Meneja wa Karakana ya Morogoro, Mhandisi
Nejo Ngosomwile alikiri kuwapo kwa matatizo hayo likiwamo la mafuta.
hivyo kusababisha mabehewa ya mizigo kukaa kwa mudamrefu.Hivyo aliiomba Serikali kuboresha masilahi ya wafanyakazi wakiwamo madereva kwani wao ndiyo wanaotegemewa katika kusafirisha abiria
No comments:
Post a Comment