Friday, February 8, 2013

SERIKALI YASEMA SILAHA ZINAZOTUMIKA KWA UJAMBAZI Z,BAR ZINATOKA BARA

 
 
 
 
 
 
Rate This

Imewekwa na Mhammed Khamis
Naibu Waziri wa Mambo ya ndani Tanzania Mh'Ame Silima akijibu masuali mbali mbali Bungeni
Naibu Waziri wa Mambo ya ndani Tanzania Mh

‘Ame Silima akijibu masuali mbali mbali Bungeni
BUNGE limeelezwa kuwa silaha zinazotumika kwa ajili ya ujambazi kwa upande wa Tanzania Zanzibar zinatoka Bara.

Kauli hiyo ilitolewa na Naibu Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima, ambaye alisema kuwa licha ya Wazanzibari kuonesha dalili za kuhusika moja kwa moja kwenye matukio ya ujambazi, lakini silaha wanazotumia zimethibitika kutoka Bara.

Alitoa kauli hiyo wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Chwaka, Yahya Kassim Issa (CCM), ambaye alitaka kujua ikiwa Wazanzibari hawaruhusiwi kumiliki silaha iweje ujambazi wa kutumia silaha unatokea huko.

Katika swali la msingi, mbunge huyo alitaka kujua ni sababu zipi za msingi ambazo zimesababisha Wazanzibari wasiruhusiwe kumiliki silaha hadi sasa na kwa nini serikali isiangalie raia walio wema pamoja na viongozi ili iweze kuwapa fursa ya kumiliki silaha kwa ajili ya kujilinda.

Silima alisema kwa mujibu wa Sheria ya Zanzibar na kwa kuzingatia hali ya kijiografia ya visiwa hivyo, wananchi hawaruhusiwi kumiliki silaha za moto isipokuwa taasisi za vyombo vya dola pekee.

“Jambo hili limechangia kuwapo kwa matukio machache ya ujambazi wa kutumia silaha, jambo ambalo linatoa faraja kwa visiwa hivyo,” alisema Silima.

Hata hivyo alisema kuwa serikali imepokea maoni ya mbunge juu ya kuangalia uwezekano wa kuruhusu raia wema kumiliki silaha za kujilinda wao na mali zao ingawa alisema jambo hilo ni la kisheria zaidi.

Kuhusu sheria hizo, Naibu Waziri alisema zinatakiwa kuanzia katika Baraza la Wawakilishi kwa ajili ya kupitishwa huko ili kuona kama jambo hilo linafaa kwa sasa au la.

No comments:

Post a Comment