Sunday, February 10, 2013

Watu 100 wauwawa Sudan Kusini

Wakuu wa Sudan Kusini wanasema watu zaidi ya 100 wameuwawa kwenye wizi wa mifugo.
Vijana wa Lou Nuer na bunduki mwaka wa 2011
Wanasema kuwa watu wa kabila la Lou Nuer waliviziwa na kushambuliwa Ijumaa katika jimbo la mashariki la Jonglei - walishambuliwa na watu wa kabila la Murle.
Umoja wa Mataifa unasema shambulio hilo ndio kubwa kabisa tangu mwaka wa 2011 ambapo wa-Murle mia kadha waliuliwa na vijana wa Lou Nuer.
Wadadisi wanasema tangu Sudan Kusini kupata uhuru mwaka huo, nchi hiyo imekuwa na shida ya kudhibiti maeneo hayo ya mbali ambayo yana silaha nyingi baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miongo miwili.

No comments:

Post a Comment