29 Machi, 2013 - Saa 13:22 GMT

Jaribio la makombora ya Korea Kaskazini
China na Urusi
zimeelezea hofu ya kukithiri kwa mzozo katika rasi ya Korea na kutaka
pande zote kujiondoa katika majibizano.
Hii inafuatia hatua ya kiongozi wa Korea
Kaskazini Kim Jong-un kuweka tayari makombora ya masafa marefu
kukabiliana na tishio la mashambulio kutoka kambi za kijeshi za marekani
na ndege zake za kivita.Agizo la rais Kim Jong-un limetokana mazungumzo kujibu hatua ya ndege za kivita za marekani kuruka katika anga ya rasi ya Korea.
Alinukuliwa akisema kuwa muda umewadia wa kumaliza mgogoro na Marekani.
Korea Kaskazini imeghadhabishwa na hatua ya Umoja wa Matifa kuiwekea vikwazo vipya.
No comments:
Post a Comment