5 Machi, 2013 - Saa 11:28 GMT

Rais Robert Mugabe na Waziri mkuu Morgan Tsvangirai
Maafisa nchini Zimbabwe
wanasema hawatakaribisha makundi ya waangalizi kutoka nchi za magharibi
kuchunguza kura ya maoni kuhusu katiba ama uchaguzi mkuu unaotarajiwa
kufanyika mwaka huu.
Waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Simbarashe
Mumbe-ngegwi amesema wachunguzi wa nchi za magharibi hawatakuwa na
malengo kwa sababu muungano wa ulaya na Marekani waliweka vikwazo dhidi
ya rais Robert Mugabe na maafisa wengine kutoka chama chake cha ZANU PF.Kura ya maoni kuhusu katiba mpya ambayo itapunguza madaraka ya rais itafanyika Jumamosi.
Wachunguzi kutoka Afrika wamealikwa kufuatilia uchaguzi huo.
No comments:
Post a Comment