
Wananchi wa baadhi ya shehia hizo
hapa Zanzibar walionekana kujitokeza katika uchaguzi huo ambapo ratiba
zake kwa hapa Zanzibar zilianza mapema Jumamosi ya tarehe 30 mwezi
uliopita.
Mbunge wa Jimbo la Kitope ambae
pia ni Makamu Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa na
Mkewe Mama Ash Suleiman Iddi walikuwa ni miongoni mwa Wananchi
walioshiriki kwenye uchaguzi huo uliokuwa ukiendelea katika shehia za
Wilaya ya Kaskazini B katika Kituo chao cha Shehia ya Kitope.
Wagombea waliojitokeza katika
Kituo hicho kilichokuwa katika Skuli ya Msingi na Sekondari ya Kitope
wakiomba kuchaguliwa kwa nafasi ya Wanawake alikuwa Bibi Abeida Khamis
Mohd pekee akiwa hana mpinzani.
Nafasi ya Watu Wazima
waliojitokeza ni Mzee Juma Issa Mwangira pamoja na Mzee Abeid Haji
Abdulla wakati nafasi ya Vijana inawaniwa na Nd. Rashid Fadhil Makame na
Suleiman Fadhil Juma.
Uchaguzi kama huo pia
ulishuhudiwa kwa shehia ya Kwa Gube ndani ya Jimbo la Kitope uliopangwa
kufanyika katika Skuli hiyo hiyo ya Msingi na Sekondari ya Kitope.
Tume ya Mabadiliko ya Katiba ya
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ikiongozwa na Mwenyekiti wake Jaji
Joseph Sinde Warioba inatengeneza rasimu itakayowasilishwa katika
Mabaraza hayo ya Katiba ya Wilaya.
Utaratibu huo utaozingatia
upanuzi zaidi wa Demokrasia hapa Nchini umelenga kutoa fursa zaidi kwa
ushiriki wa wananchi katika kujadili rasimu hiyo itakayotoa uwakilishi
wa kina wa Wananchi kutoka kila Shehia Nchini.
No comments:
Post a Comment