Monday, April 1, 2013

CUF yapinga wajumbe mabaraza ya katiba

 
 
 
 
 
 
Rate This

bimani
Chama Cha Wananchi (CUF ), kimetaka uchaguzi wa wajumbe wa Mabaraza ya Katiba usimamishwe na kufanyika upya kwa madai kuwa viongozi wa serikali za mitaa (masheha) wamelivuruga zoezi lililofanyika jana Zanzibar.Tamko hilo limetolewa na Mkurugenzi wa Haki za Binadamu, Habari, Uenezi na Mahusiano ya Umma, Salim Bimani, katika taarifa yake aliyoisambaza kwa vyombo vya habari mjini hapa.Bimali alisema kuwa zoezi hilo limetawaliwa na ukiukwaji wa sheria na kuwanyima haki wakazi halali kushiriki uchaguzi huo huku wakipewa nafasi wakazi wasiokuwa na sifa. Alisema kuna kasoro 13 zimejitokeza katika uchaguzi huo ikiwamo masheha kutoa vipande maalum vya kuwatambua wakazi na wengine kunyimwa licha ya kudaiwa kuwa ni wakazi halali katika shehia husika.
Akitolea mfano katika shehia ya Migombani uchaguzi uliahirishwa kwa madai watu waliojitokeza ni wengi na kupangwa kufanyika siku nyingine, wakati shehia ya Meya wagombea watatu wamefukuzwa katika kituo cha uchaguzi na kutumika karatasi za kupigia kura ambazo si za kituo hicho.
Bimani alisema katika shehia ya Nyerere vitambulisho vya uzanzibari ukaazi vimetumika kama shahada ya kushiriki uchaguzi huo kinyume na muongozo wa Tume ya mabadiliko ya katiba.
Alisema baadhi ya shehia masheha wamejipa jukumu la kuteua katibu wa mkutano kinyume na muongozi wa Tume ya Katiba kama ilivyojitokeza katika shehia ya Kiembesamaki.
Mkurugenzi huyo wa CUF alisema kuna vituo ambavyo taratibu za kupata wajumbe wa mabaraza ya katiba zimekiukwa hasa katika shehia ya Kihinani baada ya sheha kuwafukuza wagombea na kuchagua Mwenyekiti na Katibu wa Mkutano yeye mwenyewe kinyume na muongozo.
Hata hivyo Binami alisema kituo cha Kibweni sheha aliwaruhusu askari wa KMKM kupiga kura huku wakazi halali wakizuiwa hasa wanaoonekana kufungamana na vyama vya upinzani.
Wananchi katika shehia mbalimbali jana walijitokeza kuchagua Wajumbe wa mabaraza ya katiba huku baadhi ya shehia zikishindwa kufanya uchaguzi kutokana na kuchelewa kwa karatasi za kupigia kura pamoja na wapiga kura maamluki kupandikizwa na wanasiasa visiwani humo.

No comments:

Post a Comment