23 Aprili, 2013 - Saa 18:04 GMT
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta
ameanza mchakato wa kuunda serikali mpya ambapo ametangaza majina ya
mawaziri wanne. Wanne hao ni pamoja na Dkt. Fred Okeng'o Matiangi ambaye
ni waziri mteule wa Teknolojia na Mawasiliano, Henery Rotich ameteuliwa
wizara ya Fedha, James Wanaina Macharia ndiye Waziri mteule wa Afya na
Balozi Amina Mohammed ametangazwa Waziri wa mambo ya kigeni.
Ilitarajiwa kwamba Rais Kenyatta angewataja
mawaziri wote 18, lakini amesema wengine watatangazwa baadaye na kuomba
taifa kuwa na subira. Huku haya yakiarifiwa Bunge la Kenya limeidhinisha
kamati maalum ambayo itawachuja mawaziri watakaoteuliwa na Rais. kamati
hiyo inaoongozwa na Spika wa Bunge Justin Muturi.Chini ya katiba ya Kenya sharti bunge lipitishe majina ya maafisa wakuu wa serikali, wakiwemo Mawaziri, mabalozi na wakuu wa tume za kikatiba.
No comments:
Post a Comment