6 Mei, 2013 - Saa 17:12 GMT
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na
ambaye anatuhumiwa na mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai
anatarajiwa kukutana na waziri mkuu wa Uingereza David Cameron ndania ya
siku tatu za ziara yake mjini London.
Makundi ya haki za binadamu kutoka nchini Kenya
yameishutumu ziara hiyo ya Rais Kenyatta katika nchi za magharibi mapema
tu baada ya kushidna katika uchaguzi mkuu wan chi hiyo uliofanyika
mwezi march mwaka huu.Uingereza imesema itawasiliana na Rais Kenyatta baadhi ya mamabo ya msingi tu,akiwa katika ziara hiyo ambayo ni mwaliko wa mkutano kuhusiana na masuala ya mgogoro wa Somalia
Tuhuma za mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai ICC dhidi ya Rais Kenyatta ni kufuatia vurugu zilizotokea katika uchaguzi wa mwaka 2007 ambapo inakadiriwa kuwa takriban watu 1000 waliuawa.
Kiongozi huyo wa Kenya amepangiwa kufika katika mahakama ya ICC huko The Hague mwezi Julai ili kuanza kusikilizwa kwa kesi yake.
Bwana Kenyatta alimshinda aliyelkuwa Waziri Mkuu wa Kenya Bwana Raila Odinga kwa kupata asilimia 50.07 ya kura ikilinganishwa na asilimia 43.28% za mpinzani wake mkuu.
"Wakati wa ziara yake Rais Kenyatta atahudhuria mkutano wa Londo kuhusu Somalia na pia atafanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron kuhusu uhusiano kati ya Kenya na Uingereza".
Afisa mkuu wa shirika la Kenya la International Center for Policy and Conflict , Bwana Ndung'u Wainaina, amesema mualiko wa Bwana Uhuru Kenyatta "ni usaliti kwa ajenda ya mkutano wa Somalia" ambapo una lengo la kumaliza ukosefu wa usalama na ukiukaji wa sheria.
No comments:
Post a Comment