SUZA IMEBAHATIKA KUWA MWENYEKITI MKUTANO WA OIC
Taarifa hiyo imekuja kupitia Ziara ya siku nne ya Maafisa wa Nchi ya
Omani walioambatana na Maafisa wa Jumuiya ya OIC iliyonza leo mjini
Zanzibar.
Mwenyekiti wa Mamlaka ya Kumbumbuku na Nyaraka ya
Nchi ya Oman Dkt. Hamed Mohammed Al dhawiyaniy amesema Zanzibar imepata
nafasi hiyo kutokana na kuwa na Mahusiano mema na Nchi nyingi
ulimwenguni na hasa katika nchi za kiarabu.
Amesema Historia na
Utamaduni wa Kiislamu wa Zanzibar na namna ulivyotumika katika
kusambaza Uislamu Nchi nyingine umekuwa kigezo muhimu cha Zanzibar
kupata nafasi hiyo.
“Kwa vile Zanzibar ina historia nzuri
katika kusambaza Uislamu nchi nyingine tunaimani kuwa hata malengo ya
Mkutano wetu huo yatafikiwa kwa kiasi kikubwa ” Alisema Dkt Al
dhawiyaniy ambaye pia ni Mkuu wa Msafara huo.
Kwa upende wake
Mkurugenzi Mkuu wa OIC katika Kitengo cha Utafiti na Utamaduni Dkt.
Halit Eren amesema Mkutano huo utakuwa fursa adhimu kwa Zanzibar
kujitangaza katika mataifa mbalimbali na kuendelea kujiongezea umaarufu
Kimataifa.
Amesema kwa vile Watakuja Washiriki kutoka Mataifa
mbalimbali kutoka Nchi wanachama wa Jumuiya ya OIC, Zanzibar itakuwa ni
nafasi yake muhimu kufahamika kimataifa na kujipatia nafasi za masomo
Duniani.
Amefahamisha kuwa Watoa Mada 164 kutoka Nchi
mbalimbali tayari wameshapeleka maombi yao ili kuwasilisha katika
Mkutano huo na kuwataka Wazanzibari nao kupeleka Maombi yao.
Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Chuo cha SUZA Dkt. Haji Mwevura Haji
amesema Vyuo mbalimbali kutoka nchi tofauti viliomba kuwa Mwenyeji wa
Mkutano huo lakini Chuo cha SUZA kimeamuliwa kuwa Mwenyeji kutokana na
historia ya Zanzibar.
Amefahamisha kuwa licha ya Zanzibar
kutokuwa Mwanachama wa Jumuiya ya OIC lakini kigezo hicho hakiizuii
Zanzibar kuwa Mwenyeji wa Mkutano huo wa Kimataifa.
Amegusia
kuwa Mkutano huo unaweza kuwa fursa Adhimu kwa Zanzibar kunufaika
kupitia Jumuiya hiyo kama ambavyo Nchi ya Uganda ilifaidika kwa
kujengewa Chuo Kikuu cha Mbale.
“Wenzetu Uganda walifaidika na
OIC kwa kujengewa Mbale University nasi pia tuna matarajio mengi
ilikwemo kuitangaza SUZA na kupata Scholarships duniani” Alisema Dkt.
Haji
Dkt Haji amewahakikishia Maofisa hao ushirikiano wa kutosha ili Mkutano huo uweze kutimiza malengo yaliyopangwa.
Umoja wa Nchi za Kiislam Duniani OIC unajishughulisha na mambo
mbalimbali ikiwemo kusaidia Nchi wanachama wa Umoja huo katika huduma za
kijamii ikiwemo ujenzi wa Taasisi za Kielimu, Afya na Miundombinu
ambapo Mkutano mkuu uliopita ulifanyika Nchini Omani.
No comments:
Post a Comment