Wednesday, May 22, 2013

UKICHECHE WAMFANYA MR. NICE AZOMEWE NCHINI KENYA

Mtandao wa ghafla kutoka Kenya umeripoti kuwa, msanii Mr Nice, amejikuta akizomewa na umati wa watu waliokuwa katika Club moja inayoitwa I club, ambapo wachekeshaji Fred Omondi na Mc Antonio hufanya show zao pale kila siku za jumapili.

Inasemekana Mr Nice alikua ameenda pale kwa ajili ya kula good time tu, na kufurahisha nafsi yake, lakini matokeo yake hayakuwa kama alivyotarajia....

Aibu  ilianza pale mchekeshaji Mc Antonio alipomuona Mr Nice katikati ya watu, na kwakuwa ni mtu maarufu, Mc akamuambia awapungie mikono watu waliokuwepo pale...


Mr Nice hakufanya hivyo wala kusimama akidai kuwa yeye ni msanii ambae amesainiwa na mtu mwingine na Mc huyo hawezi kumlipa yeye, na akipanda jukwaani hapo atashitakiwa na magement yake.
 
 " Hamnilipi ninyi... nikipanda hapa kwenye jukwaa, nitashtakiwa mimi"..Mr.Nice

Baada ya kusema maneno hayo mashabiki walianza kumzomea huku wakipiga kelele wakisema Mac "Muga" wimbo  wa Ally Kiba, ambao unasemekana kuwa unamdiss yeye. na dj hakuwa na hiyana aliupiga wimbo huo maana mashabiki waliutaka.

No comments:

Post a Comment