Friday, June 7, 2013

Maandamano sharti yakome'', Erdogan


Maandamano yamekumba mji wa Istanbul kwa zaidi ya waiki moja sasa
Waziri Mkuu wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan ametaka maandamano yanayoendelea nchini humo kumalizika mara moja.
Akiwahutubia maelfu ya wafuasi wake waliomlaki katika uwanja wa ndege wa Istanbul,kiongozi huyo amesema maandamano hayo sio halali.
Lakini alipokuwa akiongeza maelfu ya waandamanaji wanaopinga serikali walikuwa wanakusanyika mjini Istanbul katika bustani ya Taksim.
Maandamano hayo yalianza kama maandamano madogo kuhusu bustani moja mjini Istanbul ingawa yakaongezeka na kuwa maandamano makubwa.
Wafuasi 10,000 wa chama cha Bwana Erdogan, walikwenda uwanjani kumkaribisha baada ya ziara yake ya Kaskazini mwa Afrika.
Akisimama kando ya mkewe na mawaziri wa serikali, aliwaambia wafuasi wake kuwa maandamano hayo ni kinyume na sheria na lazima yakomeshwe mara moja.
"sisi hatujawahi kuunga mkono mgawanyiko katika jamii lakini hatuwezi kuunga mkono watu wenye nia ya kuwagawanya watu.''
Erdogan aliwasihi wafuasi wake kuwa watulivu baada ya kuelezea nia yao ya kutaka kulipiza kisasi.
"mmekuwa watulivu , mmeonyesha ukomavu na kutumia akili zenu, sote tutakwenda nyumabi kutoka hapa.''
Bwana Erdogan alijibu wito wa watu kutaka ajiuzulu akiwakumbusha uchaguzi wa mwaka 2011 ambapo alishinda uchaguzi huo kwa asilimia hamsini.
''Wanasema kuwa mimi ni waziri mkuu wa asilimia hamsini ya nchi. Tumewahudumia watu milioni 76 kutoka Mashariki hadi Magharibi,'' alisema Erdowan
Ilikuwa mara ya kwanza wafuasi wa Erdogan wamemuunga mkono, kufuatia wiki moja ya maandamano ambayo yamemtaka aondoke mamlakani.
Mwandishi wa BBC Mark Lowen mjini Istanbul, anasema kuwa kukaribishwa kwa waziri mkuu,kwa namna hiyo ni ishara ya uungwaji mkono alionao kutoka kwa wafuasi wake.
Hata hivyo,baadhi wanasema kuwa matamshi ya Bwana Erdogan huenda yakachochea maandamano hayo zaidi.
Migawanyiko nchini Uturuki, inaonekana kukithiri zaidi katika siku zijazo na huenda hali ikawa ya hatari kubwa.

No comments:

Post a Comment